UNATAKA KUWA NANI?
Kama kuna swali rahisi
kujibiwa na watu wengi pasipo kujali umri, rika na hata jinsia ni pindi
utakapotaka kujua MTU anataka KUWA NANI? Ni swali ambalo watu wengi upenda
kusikia kutoka kwa mtu japo wakati mwingine mtu anaweza asiwe radhi kuzungumzia
ndoto zake au matarajio yake hadharani. Japo WEWE UNATAKA KUWA NANI? Ni swali
kwa hakika utapata majibu mengi kwakua kila mtu upenda kuwa mtu fulani katika
jamii ya sasa hili,kwa uhalisia, swali hili
alitajibiwa na watu wa aina fulani tu bali itakuwa ni watu wa rika zote si
watoto ,vijana wala watu wazima kila mtu anakuwa na shauku ya kuwa mtu fulani
katika kipindi fulani kijacho.
Kwa vijana wamekuwa na
muamko wa kipekee katika kutaka kuwa sawa na ndoto zao zilivyo na wakati
mwingine wamekuwa wakipenda kuwa na wenza ambao utaendana na ndoto zao au
unaweza kukuta kijana anataka aolewe au aoe mwanasheria,daktari,muhasibu,engineer,mwalimu
na wengine mengi wako vijana wameenda
mbali sana wakitaka aina fulani ya wenza wao atakama anataaluma anayoitaka pia
upenda kuona awe na muonekano fulani,rangi fulani ili aweze kuwa na mvuto zaidi
katika maisha yake.
Kuna swali ambalo ni
rahisi zaidi ya swali la mwanzo lakini ugumu unakuwa katika kusimami katika
yale unayo yataka….. swali lenyewe unaweza kuulizwa JE! UNAYAPENDA MAISHA YAKO? Hili swali ambalo
ukimuuliza mtu, kwa haraka haraka anaweza kuona kama unamdharau au unamkejeli
ikiwa rafiki yako utafanya awe na swali lingine pindi utakapoamua kumuuliza
swali hilo kwanini kaamua kuniuliza swali hili je! Kunautofauti gani kati ya
mwanzo na sasa. Lakini wako wengine watapuuzia tu na kusema naona kuwa hauna
swali la maana.
Ni ukweli usiopingika
kuwa unataka kuwa nani na namna unavyoishi vinaenda sambamba japo najua
kunauwezekano(exception) utendaji unaweza kuendelea ambao utakuwa nje ya akili
za kawaida yaani pasipo mipango yako, viko vitu vitatokea na kujikuta unafanya
jambo na linatokea sawa na vile linapaswa kutokea mathalani daudi Mungu
alipomuandaa kuwa mkombozi wa Israel alijikuta anapambana na dubu , mwanasimba
na wanyama wengine na anajikuta anawashinda na hatimae mwisho anakuja
kupambambana na Goliathi na hatimae kuwa mkombozi wa Israel.
1
Samweli 17:37 Daudi akasema, Bwana aliyeniokoa na
makucha ya simba, na makucha ya dubu, ataniokoa na mkono wa Mfilisti huyu.
Sauli akamwambia Daudi, Enenda, na Bwana atakuwa pamoja nawe.
Kuyapenda maisha yako
hilo ni jambo la kawaida sana lakini kubwa sana ni kweli unayaweka mwingiliano
na vile wewe unataka kuwa au kunamuachano wa vitu viwili vilivo na mwelekeo tofauti
lakini vina shabaha moja,ni seme wazi kuna kuyapenda maisha na kuyathamini
maisha japo kwa uhakika unapozungumzia kukipenda kitu hakuna utofauti na
kukithamini hicho kitu lakini katika uhalisia wake wake utofauti upo mtu
anaweza kuyapenda maisha yake lakini asiyathamini mathalani mtu anaweza kupenda
maisha yake lakini ukakuta bado anavuta sigara,bangi na madawa ya kulevya na
mengine mengi lakini katika moyo wake anasema anayapenda maisha yake.
Wapo wengine watasema
mimi maisha yangu nayapenda lakini sinauwezo wa kuyahudumia ipasavyo kwani
baadhi ya vitu sina uwezo wa kuvipata hivyo yanipasa ni ishi kwa shida
hivyohivyo mathalani mtu anakula mlo moja kwa siku tu na tena chakula kilekile
na sio kwamba anapenda bali ni hali halisi anayoiona katika macho yake kuwa
hivi ndivyo ninavyopaswa kuishi.
Na ni ukweli watu wengi
wamekuwa wakiishi tofauti na ndoto zao japo mtu huyo anapenda kutimiza ndoto
zake mathalani unaweza kukuta mtu mwimbaji anataka kuwa mwimbaji katika hatua
kubwa hata ya kimataifa lakini utakuta afuati utaratibu wa kufika hapo kama
vile uvutaji wa sigara, unywaji wa pombe, matumizi makubwa ya vitu vya mafuta,
kutopata muda mzuri wakumzika ,kutofanya mazoezi katika kupata pumzi ya kutosha
,kutojua namna sahihi ya kutumia sauti yake katika kuifanya izidi kuwa bora
siku hadi siku. Na wakati mwingi mtu kwakutokizingatia katika hatua za
kukufanya kuwa hatua bora uweza sasa kuwa laumu watu na kusema awapendi
maendeleo yake.
Baadhi ya matarajio ya
watu wengi ni kuwa na familia bora na kuheshimiana, na mtu uweza kuamasika
zaidi pindi anapoona watu wengine wakiwa katika furaha katika ndoa zao pamoja
na hayo mtu anashindwa kujua hivi vitu vina maandalizi yake toka matumizi ya
ujana wao, katika starehe zako uweza
kusababisha maisha yako ya ndoa kuwa na raha au kuwa na shida, wako watu
wameharibu maisha yao ya ujana kwa kiasi kwamba uwezi kushika mimba tena au
mwingine kupata magonjwa yakawa ndio maisha yake.
Niseme tu uwezi kuwa
unatakata kuwa mcheza mpira maalufu katika dunia ya sasa na huku ukijibidisha
zaidi sana katika kujifunza staili za kucheza muzuki………. unaweza kuishi maisha
ya katikati usijione kama unaenda mbele au unarudi nyuma hama uko hapohapo.
Unataka kuwa nani sio
swala la kusema tu ni swala lakuruhusu na kuamua kuwa humo siku zote katika ufanisi
na ubora unaotakiwa sio kujaribu tu na baadae ukaacha.
Swali
ambalo na kuacha nalo ni hili tu unataka kuwa nani na unaishi maisha gani?
Imeandaliwa
na;
Cothey
Nelson………………………………………0764 018535