TATHMINI NA
MUNGU
Unaishije
na Mungu…..?
Namna
unavyoishi na Mungu inaweza ikakusababishia baraka au laana.
TATHMINI hili sio jambo geni kwa watu wengi kwani ni
jambo linalo fanyika katika mazingira na hatua mbalimbali mathalani ndani ya
familia wanatathmini maisha yao kwa ujumla na kuona kesho yao ina mwanga mzuri
na kama haina na nini kifanyike? Katika makampuni,kijamii na hata katika ngazi
ya kitaifa pia ufanya tathimini kuupata mstakabali wa kesho.
Lakini leo ningependa tushirikiane katika kufanya
tathmini ya pamoja kati Mungu na sisi (wanadamu), katika kufikia hapo yako
mambo kadha kujiuliza au maswali machache yanayo pelekea au kuleta maana ya
tathimini yenyewe?
a) Wewe ni nani kwake na yeye ni
nani kwako?
b)Mungu ni kielelezo namba ngapi
kwako (mnaishi maisha yenu au yana fanana na wengine)?
c)Ni kweli yeye anafurahia maisha
nawe nawe unafurahia maisha naye?
d)Unajua vile ulivyo ni matokeo ya
wewe unavyoishi na Mungu (utofauti wenu na mtu mwingine inategemea sana
mnavyoishi na Mungu)?
e)Ni kweli ile nguvu iliyo ndani ya
Mungu iko ndani yako (lazima wote mfanane)?
f)Ni kweli maisha unayoishi nae
yanafanya aone maana ya kukupa siku nyingine kwa furaha?
g)Unafikiri kitu gani unmfanyia
Mungu hata kuona ile kazi ya msalaba haikua bure anapata faraja kwa wewe kuona
unafanya vitu amabavyo yeye angekuwepo angevifanya?
h)Unatambua wewe hauwezi fika bila
yeye ila yeye anaweza pasipo wewe?
Anaweza kuyainua mawe usiyotarajia.
i)Unaitambua nafasi aliyo kupa
Mungu na ile unayompa katika mawazo yako.
k)Unatambua kuwa wewe ndio mwenye
wajibu wakufanya Mungu afurahi kupitia maisha yako.
Imeandaliwa na ;
Nelson, Cothey – 0764 018
535 or cotheyn@yahoo.com
Katiti, James - 0713 398 042 or james.adili19@gmail.com
KILA LA KHERI…………..RAFIKI