USTAWI WA MTI UTEGEMEA
MIZIZI;
MAFANIKIO YA MKRISTO UTEGEMEA SANA MUUNGANIKO WAKE NA MUNGU
Ukiona kitu kina nguvu au kiko imara basi jua nyuma
ya hicho kitu kimeshikwa na chenye nguvu kinachoishikilia. Unapoona jambo la
kifahari na la ajabu analolifanya mtu ujue nyuma kunauwezesho wenye nguvu.
Kila mtu anayependa kufanya mambo ambayo watu
wanapoona watashangaza na kustajabu na kumpa pongeza na kuonyesha kuwa amefanya
jambo la maana sana lakini matarajio yako yanabebwa sana na kile
ulichoshikiliwa sana.
Hakuna mtu upenda kuvaa masazo( out of fashion) au
kukaa mahali ambapo hapampi heshima au apafurahie bali utegemea kile alicho
ungamanishwa nacho kinauwezo wa kumweka hapo au akiwezi, hivyo matarajio ulio
nayo yanabebwa sana na uwezo uliokushikilia.
Ukisikia huyu anasoma uingereza, nchi tofauti
anapozaliwa (Africa) na huyu anasoma shule iliyo jirani yake lakini yote haya
ubebwa na nguvu iliyo nyuma yake yenye uwezo wa kukufikisha hapo ulipo.
Mafanikio
ya mkristo utegemea sana na jinsi alivyo imarisha misuli yako katika yeye
( nguvu ya muunganiko katika yeye)
Kutoka
19: 5
Kama vile uimara wa mti utegemea sana uwezo wa
mizizi ndivyo ustawi utegemea sana jinsi uliimarisha mizizi yako katika yeye.
Lazima ujue kuwa bila ya kusimika mizizi yako katika
wewe hauwezi kuwa imara katika yeye na hatimae ukapate mafanikio yake.
Ni vizuri utambue kuwa kunamafanikio na
kufanikishwa, hivi ni vitu viwili ambavyo haviwezi kuchangamana hata chembe kwa
kila kitu kina kitu kimeshikiliwa kinaweza kuwa na nguvu au hakina nguvu.
Ninapozungumzia mizizi katika Mungu ninazungumzia
nguvu ya kumsikia Mungu na kumwelewa na hatimae kuingiza katika utendaji.
Kumwelewa kunadhihirika katika utendaji maaana ndio ishara ya kuonyesha kuwa
umemwelewa na unamwamini na kumtegemea.
Bila kuishi na Mungu na kumsikia wewe binafsi ni
ngumu sana kwa wewe kufanikishwa na Mungu kwani yeye amebeba utoshelevu wako
kwa ukamilifu.
Mungu ndio anakupa utajiri na kukustarehesha kwakua
vyote viko kwake, usitafute kujistarehesha bali tafute akustareheshe kwakua
starehe yake haina majuto wala maswali iko na amani iliyostahiki iliyo jaa
utoshelevu wake.
Hauhitaji kutafuta wapi mali zipo bali mtafute
mwenye mali ili yeye akufanikishe kwa kuwa vyote ni mali yake na vinatoka
kwake.
Ukifanikiwa katika kumsikia yeye kuliko chochote
basi unakuwa katika nafasi iliyo sahihi ya kuwa vile anavyotaka.
Usivitegemee vya Mungu kuwa vyako kama wewe ujawa wa
Mungu kwanza ndivyo vyake moja kwa moja vinakuwa vyako.
Imeandaliwa na ;
Cothey Nelson,
0764018535, cotheyn@yahoo.com
Sina maneno mengi zaidi ya kusema
Asante!!!