Jumanne, 4 Agosti 2015

KILA KIU KINA UJAZO WAKE



KILA KIU KINA UJAZO WAKE!!!


 Sote tunafahamu kuwa kunywa maji wakati unakiu ni burudiko la nafsi inaloleta usawa wa akili… ingawa wako watu wanapenda kutumia maji ya moto (maji yasiyo ya baridi) na wengine watapenda kutumia maji ya baridi lakini katika yote la msingi ni kazi ya hayo maji katika kuleta burudiko katika mwili wa binadamu na afya………….japo wataalamu wa afya wanasisitiza kuwa kunywa maji sio mpaka uone kiu bali ijengeke kama utaratibu wa maisha yako!

Ni kweli hata kama utaamua kunywa maji kwa kufuata utaratibu wako au kunywa maji kwa kufuata utaratibu wa wataalamu lakini hauta kunywa zaidi ya kiu yako, na kwa kufanya hivyo itakuwa tofauti katika ujazo kati yako na mwingine japo wote mnaweza kuwa na kiu lakini bado mtakuwa tofauti katika utoshelevu au katika kukidhi matakwa ya kiu.

Na pindi unapojua ujazo wa maji utakao tosheleza kiu yako basi bila shaka utachukua maamuzi sahihi katika kujipimia ujazo unaostahili na wakati mwingine hali hii inaweza ikaokoa upotevu wa fedha, muda na hata matumizi mabaya ya maji kama vile kiasi kinachobaki ukawaza kuyamwaga na wakati ungejipimia kiasi chako hicho kiasi kitakachobaki kingewafaa wengine.

►Ninapozungumzia kiu na zungumzia jambo lilo zaidi ya hili, sio kiu cha maji tu bali hali sahihi katika utekeleza wa jambo liwe gumu au jepesi  hama liwe jema au baya basi tunapaswa kuangalia na kulitatua katika hali stahiki au katika mazingira stahiki.

Pindi unapoamua kuukata mti na ukaweka bidii katika kuyakata matawi yake tu ukijua utauangusha huo mti na hatimae usiote tena pasipokuangalia tabia za huo mti na uwezo wa mizizi katika kujikita katika ardhi…………….unaweza kuonekana kuwa unaakili sana pindi utakapo kuwa unaukata matawi ya mti lakini pindi matawi yatakapo anza kuota tena basi utaonekana kumbe juhudi yako yote ilikuwa bure!

Ni wazi jambo linaloumiza kichwa na hata moyo pindi utakapoona tatizo ulilonalo hakuna njia sahihi katika kutoka hapo baada ya kujaribu kila njia ya kutoka pale ulipo……tatizo kama tatizo uwa hakuna mtu analipenda na lipo katika kila mazingira na katika maeneo mbalimbali mathalani kanisani,shuleni na katika familia.

►Tatizo lolote liwe mahali popote ukubwa wake na udogo wako utegemea nguvu maarifa yako na zaidi sana utayari wa ufahamu kukubali kuenenda na wimbi la kimbingu ambalo Mungu atakuagiza katika utekelezaji katika kuliondoa tatizo.

Watu wengi wanapenda kuchukulia kuwa tatizo na kuona kuweza kulitatua kwa njia moja mathalani ukali, ukimya au kupotezea hasa jambo linapokuwa uwezo wa akili yako!! Niseme kuwa hali hii sio stahiki kwa kila utatuzi wa kila tatizo.

Yako matatizo ambayo yanaisha kwa mtu kukutana na mshirika mwenzake,rafiki na mwengine kueleweshwa vizuri na mwingira kujaliwa na mwingine kukutana na uongozi wa kanisa na mwingine kukutana na mchungaji wake!

Lazima kila tatizo lipatiwe utekelezaji unao stahili ukikosea kufuata utaratibu wa kulitatua tatizo ni wazi kabisa alitaisha litadumu kwa muda wote hata tatizo lilikuwa dogo au kubwa…..kama ilivyo katika hesabu nyingi uwezi kupata jibu sahihi kwanza formulary (kanuni) iwe sahihi na uweze kuitumia iyo kanuni basi bila shaka utapata jibu lililo sahihi.

►Yapo matatizo kutokana na namna lilivyo linahitaji kiongozi au mchungaji fulani ajishushe au amue tu kuwa mkweli alafu mambo mengine yatakuwa sawa hata bila kuomba sana au kuwaza vibaya.

Yako matatizo mengine ni lazima upoteze thamani yako kwanza ili uweze kuungamanika tena na hatimae kulitatua tatizo.
Ni pende kusema kwamba tatizo lolote lina sifa kuu mbili

i.kukua
usipoamua kulichukulia kwa umakini na kutaka liishe kabisa kwa gharama yeyote bila shaka litakuwa kubwa na hatimae unaweza kushindwa hata kulitatua na ukajuta hata kusema kwamba ningelijua ningelimaliza mapema.
Tatizo linaachwa pasipo kuangalia kuwa jambo hili linaisha au linaendelea kuwa kubwa kwa kutokua makini unaweza ukakuta jipu likapusa hata usijue limepasukia wapi na namna ya kulitibu lisiwezekane tena.
Ushauri wangu kila tatizo linategemea utatuzi sahihi ili liweze kuisha na sio bora utatuzi tu kwakua sio kila tatizo linatatulika katika njia moja!

ii. kupungua
hili ni jambo jema sana tatizo linaweza kuisha kwa ukimya, kuongea au kupeana zawadi na ndio hatua nzuri ambayo inahitajika kwa waliotofauti katika jambo lolote.

Lazima ujue kuwa tatizo linapungua kwa kudhamiria kulipunguza na hatimae kulimaliza kabisa hilo ni jambo jema kuwa mnaweza kulimaliza japo katika kulimaliza mnaweza msiendelee katika kufanya jambo moja.

Kwa Mungu ni jambo la hatari sana……..ole wake akwazikae na ole wake asabishae makwazo!!!

Tatizo linakuwa sio tatizo tu ukiipata njia sahihi ya kulimaliza tatizo na sio kila njia inatakiwaitumike katika kutatua maadam ni njia! Sio kweli.

Kutafuta njia sahihi ya kumaliza tofauti zenu hapo ndipo tunasema hapo ndipo kutafuta kwa bidii kuwa na amani na watu wote.

►Tatizo kubwa linakuwa pale ambapo hakuna mtu anajihesabu kuwa ni mkosaji wote wanaona wamefanya vizuri hivyo wanapaswa kuombwa msamaha.

Kiu ya maji haiwezi kumalizwa na juisi!! Hizi kiu mbili tofauti kamwe hazina mbadala……!!!!

Tafuta njia sahihi huku ukiwa tayari kujishusha na kukubali kosa na hakika utakuwa salama katika yeye………….zaidi sana Roho mtakatifu atakujulisha moyo watu na kukupa utatuzi wake bila ya kukosea.
Nikisema siku njema nitakuwa sijakosea!!!
Imeandaliwa na;
Cothey Nelson…………………………………….0764 018535