Jumanne, 26 Aprili 2016

NAIKABILI VIPI VITA DHIDI YA LENGO LANGU



NAIKABILI VIPI VITA DHIDI YA LENGO LANGU



Unaweza kukosa jina la kupewa pindi utakapoongea mbele za watu kuwa mimi sina malengo/lengo lolote katika maisha yako………….lakini utakuwa ni mwanadamu wa kawaida pindi utakaposema kuwa unamalengo/lengo katika maisha yako! Nikubaliane kuwa kuna kuwa na malengo/lengo na kukamilisha au kutimiza lengo………mbali na hapo pia kuna kiwango cha kutimiza hazima yako unaweza ukatimiza lengo kwa asilimia 100%, 80%, 50% au 0%. 

Nauhakika kila mtu unuia na kutamani kutimiza lengo lake kwa asilimia zote, lakini kutamani na kutimiza kunaweza kuwa kusini na kaskazini kwa maana rahisi ukaishia katika mawazo tu! Kwakua hakuna mtu anaweza kukuzuia kuwaza ila anaweza kuwa mchango mkubwa katika kukuzuia kufikia au kutimiza lengo lake.

Lengo ni tarajio lako katika jambo unalolifanya! Au jumla ya matarajio yako katika kutimiza jambo Fulani au kufikia katika hatua fulani. Nipende kutenganisha vitu hivi hatima na lengo, napozungumzia hatima hapa na zungumzia lengo kuu(kusudi) na ninapozungumzia lengo na zungumzia mimikakati midogomidogo inayoweza kukusaidia kukufikisha kwenye hatima yako au kukustawisha zaidi katika hatima yako.

Kukumbuka leo nazungumzia vita dhidi ya LENGO lako, kama nilivyosema kuwa lengo ni kitu kimoja na ni kitu kizuri lakini kutimiza lengo hapa nazungumzia kitu kingine na katika kutimiza lengo sio kama safari kuwa kutoka nyumbani kwenda sokoni kuwa hunawasiwasi kuwa nitafika kweli maadam umeshapanda gari basi bila shaka unajua utafika  hapo ni nitanunua nini nikikuta nini?( kutimiza hazima yako).

Hakuna kama kitu kibaya kuona mtu ametumia nguvu sana lakini mwisho anashindwa kutimiza ndoto zake! Niseme uhitaji kulia pindi unapoona vita inakukabili bali iruhusu hiyo vita ije ili upite hapo katika hiyo njia kufika katika hatua nyingine.

-mambo ya msingi katika lengo lako;

i.liwe nilengo lililo na msukumo wa kimungu ndani yako

sio kila lengo zuri bali unataka kulipata kwakua kila lengo linakuwa limebeba kusudi fulani kwa mtu fulani na linakuja kwakua linaukamilisho uliojaa hatua inayoifuata.
Lisiwe limebeba maslahi binafsi ambayo kwa uhalisia hayana faida sana katika ufalme wa Mungu……kwa kiasi kikubwa linakuwa limekosa msaada wa Mungu katika kukufanikisha kutimiza lengo hilo.
Kuwa na lengo ni jambo nzuri lakini utambue kuna malengo yanahitaji nguvu za mbingu katika kukusaidia kufika hatua iliyobora zaidi.

ii.ishi kama hakuna vita

iangalie vita kama njia yakupita na sio kama kizuizi kwakua hakuna kizuizi kinachoweza kumzuia Mungu asiweze kutendekazi kwa kua yeye pekee ndiye hitimisho la kila kitu.

Mungu ili kutenda anatarajia sana imani yako na namna unavyomuangalia kwakua yeye amekuapa nyezo za kushinda na sio za kushindwa na hakuna sababu utayotoa kwa Mungu itakayo mshawishi Mungu na kuona kule ulipaswa kushindwa.

Lazima umuone Mungu uwa anafanya njia mahali ambapo kiukweli macho yako ya nyama hayajaona njia katika ufasaha wake.

iii.ona kufikia lengo lako inawezekana

katika yote endelea kutia bidii na juhudi katika maarifa na huku ukizidi kumpenda Mungu kwakua vile unavyoona ndivyo imani itazaliwa hapo na hatimae matunda kutokea.

Vile unavyoona ni ishara tosha kuona kama kuna uwezekano kufika kule unakotaka hata kama mazingira yote hayakuangalii katika picha unayoitaka, la msingi jua kuwa utafika tu katika namna yoyote utafika tu.

Imeandaliwa na:

Cothey Nelson…………………………………………………………….0764 018535

Jumanne, 12 Aprili 2016

SIRI ILIYOJIFICHA



SIRI ILIYOJIFICHA

Laiti ungejua mwelekeo wa kinyonga usingemcheka kwa mwendo wake! Laiti ungetambua mbuyu unapoanza baadae utakuwa tishio katika ukubwa wake ungechukua maamuzi mengine au hata kuhuamisha sehemu nyingine yenye nafasi zaidi, laiti mzazi angetambua kuwa mtoto huyu baadae atakuwa rais wanchi angemwangalia kwa jicho linguine, laiti tungejua chachu hii ndogo itachachua donge zima tungekuwa na umakini mwingine, laiti ungejua huu moto mwisho utatekeza mali zote au msitu mzima tungeongeza umakini………..! SIRI ILIYOJIFICHA

  Kama kitu ambacho kinaweza kumpa mtu nguvu sana katika jambo lolote ni pale anapotambua siri ya kumshinda mpizani wake uwa anajiona ameshashinda hata kabla ajapanda ulingoni, kwakua anaamini kuwa ushindi ni lazima hivyo anakuwa hana wasiwasi…………..sio jambo lakushangaza sana bali hali inaweza kutokea hata kwa wanafunzi hasa wanachuo pindi wanapotambua eneo ambalo anajua mwalimu atatoa mtihani wake uwa asumbuki sana bali uelekeza nguvu zake katika eneo mahususi na pindi anapoona ameshalimaliza hivyo uweza kujiwekea kufanya vizuri katika mtihani huo, na bila shaka mwanafunzi anakuwa na wasiwasi sana pindi anaposhindwa kutambua eneo gani hasa mwalimu atatoa mtihani wake na hivyo uweza kujipa asilimia 50 kwa 50.

Unapotaka kumsaidia mgonjwa katika ufanisi zaidi lazima uwe makini sana pale dalili zinapoanza kutokea hasa dalili za mwanzo kabla ya dalili za kuonyesha kukomaa kwa ugonjwa maana katika hatua ya awali ni hapo unaweza kufanya jambo la uhakika.

Nchi nyingi zilizoendelea uwa zinakuwa makini sana pindi zinapoona dalili ya kitu kwa mtu katika uvumbuzi wa kitu au kuleta maboresho ya kitu uweza kuwekeza kila kitu kitakachomwezesha mtu huyu aweze kufika mbali wakijua kuwa atakuwa msaada kama sio kwao basi katika jamii yake atakapokuwepo ila watalazimika mpaka wa hakikishe kinatokeza na kinaendelea.

Kwa mtindo huo nchi hizi zimekuwa ni ngumu kushuka chini kama nchi zinazoendelea katika maeneo ya teknolojia na hata katika swala la mpira katika kuwa nafasi ya juu kwani utengeneza vikosi vya baadae watu ambao watawarithi pindi itakapotokea wao wameshachoka au mauti umewakumba na matatizo mengine,

Sipendi kusema kwamba watu hawajiandai katika kufanikisha malengo yao kwenye mipira na shughuli mbalimbali za maendeleo katika ulimwengu wa sasa na hasa katika nchi zinazoendelea kama vile Tanzania katika kuhakikisha kunakuwa na watu wataendeleza mambo mazuri kwa ufanisi mkubwa lakini shida kubwa inakuwa unawaandaji hao watu katika kushika nafasi hizo mathalani katika mipira miguu watu wengi walikuwa wakicheza mpira katika nafasi kubwa hata kufikia hatua ya kuwakilisha nchi vizuri lakini pindi anapopata tatizo mathalani kuvunjika mguu basi thamani yake inapotea kabisa pasipo kujua kwa kumfanyia mnawafungia wengine kuona maana hapo si sehemu nzuri kushindwa kufanya mambo stahiki kwa mtu kwa huyo atakuwa kichocheo kizuri kwa wale mnaowandaa katika kushika nafasi.

Hakuna jambo la maana sana katika jambo lolote kama maandalizi maana linahitijika katika maeneo mengi mathalani shambani, hospitalini na maeneo mengine na ukumbuke maandalizi mazuri uleta matunda ambayo yatakuwa furaha kubwa katika maisha yako.

Unaweza kuitambua hadhina ya mtu ndani yake lakini unamwandaaji mtu huyu katika kuhakikisha anakiachilia hichi kitu kwa moyo wa furaha pasipo kinyongo, niseme tu hata ukiitambua siri kiasi gani ili uipate unahitaji maandalizi yaliyo kuwa makini sana ili uweze kufaidi kile kitu unachokitaka.
Watu wengi wanaona siri iliyo ndani ya mtu uweza kufanya maandlizi yasio kuwa kamili na hivyo kupelekea kutoona ile faidi ambayo ulikuwa unaiona au unahisi iko ndani ya mtu napengine ukahisi kama umekosea kumbe ni maandalizi mabaya.

Ni vizuri utambue pindi unapoona kitu kizuri ndani ya mtu hakikisha unapata kibali kwa Mungu kabla ujachukue hatua yoyote na muhimu ujue kuwa ni Mungu ndie amekiweka ndani ya mtu na yeye ndie anayekitunza hivyo utambue kuwa nafasi yako Mungu atakupa uifanye juu ya huyo mtu ili azidi kufaa katika katika ufalme wake.

Kibali cha Mungu ndio kiwe kiongozi ufanye yote kwakujua ni Mungu amenipa!

Luka 14:28 Maana ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara, asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama, kwamba anavyo vya kuumalizia?

Imeandaliwa na:

Cothey Nelson……………………………………………0764 018535

NIKISEMA WEWE NI WAMAANA NITAKUWA SIJAKOSEA!