Jumanne, 25 Aprili 2017

USTAWI WA NENO LA MUNGU NDANI YANGU!



USTAWI WA NENO LA MUNGU NDANI YANGU!


Duniani unaposema neno Mungu akili za binadamu wengi zinaanza kubadilisha mwelekeo na utulivu na usikivu wa muda uweza kuzaliwa hapo, japo wakati mwingi hali hii utegemea nani anasema,

Kikawaida kila mtu atasema anamuogopa Mungu na anamuheshimu sana na ndomana wakati mwingine uwasaidia watu ili Mungu amnyooshee mambo yake na hatimaye akazidi kuwa na utoshelevu katika hali zote,

Japo kuwa ishara kubwa ya kumuheshimu mtu au Mungu ni kutekeleza maelekezo yake aliyokupa katika hali stahiki yaani wakati sahihi, namna sahihi na hali sahihi, na hakuna heshima iliyobora kama haijaanzia moyoni mwako na wala sio katika sura yako inaonyesha tabasamu la muda,

Ukweli kumuheshimu Mungu na kumpenda Mungu sio kitu rahisi japo kinawezekana ni wewe kutambua na kuishi katika utendaji wa kuonyesha unamuheshimu Mungu, kwakua mfumo wa maisha yako ndio unatoa picha kamili machoni pa Mungu sio kujitahidi au kujifanyisha,

Na ni kweli kila mtu upenda kufanya jambo na aone matunda yake na pindi ikatokea asione matunda yake basi hapo bidii na kujituma zaidi uweza kupungua kabisa, zipo hatua mbili ambazo zinazo wezesha neno la Mungu kustawi ndani yako,

Ikumbukwe kuwa kustawi neno ndani yako uko ndiko kustawi kwako na kuto stawi kwa neno la Mungu ndani yako basi hali hii itapelekea na wewe kutostawi, ijulikane kuwa ninapozungumzia kustawi ni zaidi ya kuwa na pesa hama kuwa na marafiki wengi

I.KULIIFADHI NENO NDANI YAKO

Na ikumbukwe kuwa atulihifadhi neno la Mungu kwa kua na biblia kubwa nyeusi unayoitunza kama sahani ya udongo katika matumizi ya siku maalum yaani kwenda nayo jumapili hama kulala nayo ili ifanyike kuwa ulinzi na ikuepushe na ndoto mbaya hama majinamizi kutokutesa usiku,
Neno la Mungu linatakiwa lipate nafasi ndani ya moyo wako ili liweze kuendesha maisha yako kwakua lenyewe lilikujua tangu ujawa katika tumbo la mama yako, na linajua namna ya kukufikisha katika hatima ambayo Mungu amekuandalia,

Zaburi 119:11 Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi.
Kwa maana rahisi neno la Mungu likiwa ndani yako linakuwa ni ulinzi kwako dhidi ya chochote kinachoweza kuondoa ushirika wako na Mungu,

Lazima uwe unapata muda mzuri wa kulisoma neno la Mungu kwa mapana yake na sio kama unakamilisha ratiba  hama kuna mashindano la! Bali kwakua unatambua kuwa ndio dira ya maisha yako na pasipo hilo uwezi kuona uwezesho wa utendaji wa Mungu katika maisha yako.

Ifike kipindi ulitamani neno la Mungu zaidi ya kiu ya maji katika maisha yako, kama mtu alivyo na njaa na kiu namna anavyo nyong’onyea ndivyo roho yako inavyoteseka kama ikikosa neno la Mungu.
Yohana 14:23 Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake

Uwezi kulishika neno la Mungu kama ulijui na hauwezi kulijua kama ulisomi, kusoma ni muhimu sana hata kama kila baada ya lisaa unasoma hakuna shida hiyo inaweza kuwa ni akiba ya siku zingine za baadae.

II.KUTEMBEA KATIKA WITO WAKO

Hii hatua ambayo unakuwa na Mungu katika hali ya ubinafsi zaidi kwakua hapo unapewa maelekezo sawa na kusudi lako, kama neno limekuwa likitawala akili yako hali hii inakuwa nyepesi sana kwakua sehemu kubwa unakuwa umekwisha andaliwa.

Isaya 55 :10 Maana kama vile mvua ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko; bali huinywesha ardhi, na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, na mtu alaye chakula;
                 11 ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.

Ni seme ni moja kazi kubwa ya neon la Mungu kuhakikisha unatembea katika ubora wa kusudi la Mungu alilo kukusudia pasipo kuchoka wala kukata tamaa bali katika mafanikio makubwa aliyo ya kusudia,

Neno la Mungu linakuwa hapo kwa ajili ya kuhakikisha linakutia nguvu na kukupa maarifa zaidi katika wito uliopewa na Mungu ili kuhakikisha unafanikiwa kutimiza kusudi la wewe kuwepo, Hauwezi kuona matunda/matokeo ya Neno la Mungu kwa ukamilifu bila kutembea katika wito/kusudi lako.

Katika hatua hii ni kipindi Mungu anataka kukutambulisha kuwa wewe ni nani yaani upekee wako kama hauta tambua na kuendelea kuishi katika huduma za watu wengine hapo unaweza usione utendaji wa neno la Mungu kwakua neno lipo kukuwezesha katika eneo lako na sio kila eneo ili mradi upo bali ni lile tu uliokusudiwa kuwepo na mbingu tu.

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey Nelson…………………………………………0764 018535