Ubora hama uzuri wa maamuzi haupo kwenye kusema “ sasa nimeamua” la hasha! bali ni namna unavyoenenda baada ya maamuzi ni jambo la msingi kwani yanayoweza kukupa raha hama majuto!
Inawezekana ikawa rahisi kuamua maamuzi fulani katika maisha yako kwa lengo zuri tu la kuleta raha katika moyo wako lakini jasho linaweza kukutoka pindi utakapoanza kuyaishi hayo maamuzi…… Na inasemekana maisha ya mwanadamu yamebebwa na maamuzi na maisha yake yanadhihirisha maamuzi aliyo yachagua, na ikatokea mtu akasema mimi sina maamuzi katika hili kwa maana hali ya kutofanya jambo, basi hayo nayo ni maamuzi japo mtu anaweza asijue kwa yeye kuamua kuishi mtindo fulani katika maisha yake nayo ni maamuzi na hata wakati mwingine anaweza asijue.
Japo katika dunia ya sasa unaweza usishangae kuona mtu ndani ya siku amekuwa na mawazo mengi yanayoweza kupelekea maamuzi mathalani mtu aliyekuumiza au kukuuzi unaweza kuwaza mengi kama vile sijui ni mchunie tu! Au nimpe dozi! Hama nimpige mkwala/biti zito, au ni mwaribie katika mambo yake au nimfanyie kitu ambacho hata kaa akisahau ( kiweke alama katika maisha yake) na mengine mengi yako mengi mawazo yanayo sukuma kuchukua maamuzi na sababu zake.
Ukitaka kuona usumbufu wa moyo wa mtu wa hali ya juu, ni pale jambo linalo mkabili likakosa majibu katika akili likazaa teso la moyo usumbufu wake unaweza kuwa mkubwa zaidi ya uchungu wa mjamzito maana hapo panakuwa apakaliki, apaliki, mate hayamezeki, hofu + msongo wa mawazo( stress) inakuwa ni maisha yako yasiyo rasmi.
Wakati mwingine katika maamuzi uliyoyafanya nyuma unaweza kuona gharama hama kujigharimu kwingi kutokana na maamuzi uliyoyafanya awali japo yako maamuzi ukisha chukua hatua ni ngumu kuyabadili bali yanaweza kukupelekea maisha yaliyo kosa furaha.
Ina aminika kuwa maamuzi yenye kukugharimu sana basi hayo ndio yenye faida katika maisha yako ndo maana watu usema “ No pain No gain” huu msemo utakuwa na maana sana kama tu umepata kitu ulicho sumbukia hama kukigharamia.
Kuna baadhi ya watu safari inapoanza kuwa ngumu uweza kusema “ Laiti ningelijua kesho” kwa maana rahisi jambo hili limekuwa tofauti na vile alivyofikiria hama kuamini hivyo jasho jembamba linapoanza kumtoka na kutamani dunia ibadili majira yake labda utapata ahueni.
Unaweza kukuta mtu ameamua kuwa peke yake muda mwingi au muda mwingi anaangalia video au simu na wengine ujitahidi kufanya mambo yatakayo leta furaha hama kuchangamsha moyo wake na yote anafanya sio hobby au fun bali ni kujaribu kupunguza ugumu na uzito unao mkabili kutokana na maamuzi uliyoyafanya.
Ni bora uchukue muda kusema Ndiyo au Hapana kuliko kuyatamka haya maneno pasipo kuwa tayari kubeba gharama zinazotokana na maneno hayo, jiandae vizuri akili, hisia na mtazamo wako katika jambo lolote unaloliendea.
Muhimu kutambua mafanikio na kutofanikiwa kwa jambo unalolikabili linakutegemea wewe sio mtu mwingine ( sio rafiki, ndugu, mzazi), hivyo matokeo yoyote yatakayo kukabili wewe ndio mwajibikaji pekee.
Jasho linalotokana na maamuzi ni jambo jema kwani ni ishara kubwa kuwa maamuzi umedhamiria sio ya kukulupuka!
INAITWA SIKU! BARIKIWA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson………………………………………0764 018535