MUNGU ANGALII UNA NINI ILI APAE NAWE BALI KIASI GANI UMEMJAA YEYE HICHO NDICHO KIVUTIO KWAKO!
Moja ya kitu kinachoangaliwa na watu wengi ni muonekano na sio mbaya kwani hata Mungu ujali sana muonekano wako hasa wa ndani maana ndio wenye tija kwake.
Maana muonekano wa ndani ndio wenye kubeba uweza mkubwa wa kuitawala tabia yako ili uweze kutimiza kusudi lake Mungu ndani ya maisha yako.
Ni kweli ukiwa na mali hicho kinaweza kuwa ni kivutio cha watu wengi kwako, jina lako linaweza kutajwa kila mahali hata pale ambapo ukutarajia si kwasababu vile ulivyo bali kile ulichonacho.
Utofauti mkubwa uliopo kati ya binadamu na Mungu ni namna anavyoangalia mambo…………………………!
1 samweli 16:6 Ikawa walipokuja, alimtazama Eliabu, akasema, Yakini masihi wa BWANA yupo hapa mbele zake.
7 Lakini Bwana akamwambia Samweli, Usimtazame uso wake, wala urefu wa kimo chake; kwa maana mimi nimemkataa. Bwana haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali Bwana huutazama moyo.
“ mimi siangalii kama binadamu wanavyoangalia”- Mungu!
Kwa kuwa jicho la Mungu linaona hitimisho lako, kwa kila tendo unalolifanya linaweza kung’arisha hitimisho / hatma yako au kuiharibu.
Moja kati ya vitu ambavyo Mungu atingishwi nacho ni mali ulizonazo ( wealth ) japo mali ulizonazo zinaweza kuwa tishio kwa watu na hata kuwavutia wengi kwako na inaweza hata kupelekea hata kubadilisha jumbe za wachungaji/ wahubiri ili mradi tu wewe uendelee kuwepo kanisani lakini sio Mungu.
Ibrahimu na Mungu!
Mwanzo 22:9 Wakafika mahali pale alipoambiwa na Mungu, Ibrahimu akajenga madhabahu huko, akaziweka tayari kuni, kisha akamfunga Isaka mwanawe, akamweka juu ya madhabahu, juu ya zile kuni.
10 Ibrahimu akanyosha mkono wake, akakitwaa kisu ili amchinje mwanawe.
11 Ndipo malaika wa Bwana akamwita kutoka mbinguni, akasema, Ibrahimu! Ibrahimu! Naye akasema, Mimi hapa.
12 Akasema, Usimnyoshee kijana mkono wako, wala usimtendee neno; kwa maana sasa ninajua ya kuwa unamcha Mungu, iwapo hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee.
“ kama ukuweza kumzuilia mwanao wa pekee isaka hakika kukubariki nitakubariki “
Mungu sio apendi tuwe na mali ila mali bila yeye ni maangamizo maana mali inaweza kukuendesha na hata kupelekea maafa yako.
Tatizo sio kupata vitu! Kwani mtu anaweza kuwa na pesa matumizi yake yakakosa mafuta, tunajua kazi ya mafuta ni kufanya kitu kwenda pasipo ukakasi au kulazimisha kwa ugumu ndivyo mtu anaweza kuwa na pesa lakini akawa anatumia vitu avielewi mara hili au lile mambo yanatokea mengi mara huyu mgonjwa au ajali yaani mambo yamepangana tu yote yanakula hela tu mpaka zinakwisha.
Lakini hela zinazoambatana na mafuta ya Mungu zinatumika lakini haziishi sawa na yale mwanamke mjane aliyekuwa na kibaba cha unga anachota haviishi.
Kivutio cha Mungu ni moyo uliye mjaa yeye usiobadilishwa na upepo hama kushawishika na mali maana sio changamoto kwake, maana pindi utakubali kuwa chini ya himaya yake basi kukutunza ni jukumu lake.
Kwahiyo unapoenda kwa Mungu ujue hakuna kitu kitakacho mvutia kwako zaidi ya moyo uliomjaa yeye.
“ Mtu huyu ndiye nitakaye mwangalia mtu aliye mnyenyekevu, mwenye roho iliyopondeka……”
Isaya 66:2(b)….lakini mtu huyu ndiye nitakayemwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu.
INAITWA SIKU! BARIKIWA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson…………………………………….0764 018535