“ ukristo wangu ndio maisha yangu”
Uzuri wa dunia na utamu wake ni kwamba kila mtu anakitu kwake anakiona kuwa ni muhimu kwake, lakini tatizo linakuja pale tu kitu kimoja kila mmoja akakiona ni muhimu kwake na kutaka kuwa nacho kwa muda mmoja hapo ugomvi na chuki uweza kuzaliwa.
Kama binadamu kuwa na kitu cha muhimu ni jambo la kawaida, kwa kuwa kila binadamu ana mwelekeo wake hivyo upelekea hali ya mtu kuwa na kipaumbele chake, japo anaweza asijue kuwa jambo hilo kipaumbele kwake ila hicho kitu kitachukua nafasi kubwa katika moyo wake na hata hisia zake.
Japo umuhimu wa kitu (kipaumbele) ubadilika kulingana na mazingira husika na hali iliyotokea mathalani baba anaweza kuweka kipaumbele kwa mwanae lakini inapotokea mwenendo wa huyo mtoto kutoufurahisha moyo wa baba, hivyo umuhimu wake unaweza kushuka na hatimaye kipaumbele kubadilishwa.
Cha Muhimu kwangu! Ni hali ya mtu kuwa na kitu kitakacho kukuwezesha kuwa katika hali yako ya ubora na ustawi na kwa umakini wa kufuata maelekezo kwa uangalifu wa rohoni na mwilini.
Ndomana unaweza usishangae kwa kipindi cha kwanza mtu anaweza fanya kitu kilicho bora au kizuri lakini pindi unapopoteza umakini katika kipaumbele chake ( jambo la msingi katika kufanikiwa kwake) basi hapo unawezafanya kitu kilekile na kwa namna ile ile lakini matokeo yakawa tofauti na alivyotegemea.
Kuna wakati unaona kuna mambo mengi ya kufanya ukashindwa kuchukua hatua au kufanya maamuzi sahihi katika kutoa nafasi ya kwanza kwa kile kitu muhimu au kilicho kuwezesha kuwa pale.
Unaweza kukuta mtu alikuwa na huduma ilipoanza kutumika ikaleta matokeo mazuri na hatimaye kupelekea kufahamika na kuzidi kugusa maisha ya watu wengi na katika hali hiyo ukajikuta kupenda sifa na kutopenda kushuka ( kama ilivyo asili ya Mungu ndani ya mwanadamu) na hata kuanza kupelekwa na kila upepo kushoto au kulia na hatimaye kupoteza chanzo cha ubora/ ustawi wake.
Sio mara zote msingi wako ( chanzo cha ustawi) unapo poteza ukajikuta uko chini, unaweza kupoteza chanzo cha ustawi wako lakini ukakuta hakuna mabadiliko ya inje yanayoweza kukutisha hivyo ukaendelea na msimamo wako pasipo kujali mng’ao wa kesho yako.
Lakini dalili kuu ya kutambua kuwa chanzo chako kilichopelekea mng’ao wako kimepotea ni ongezeko la tabia za mwilini.( ubinafsi na kujiami zinakuwa na nguvu sana kwako ).
Kwa Yule ambaye ajapoteza chanzo japo upepo na dhoruba zinaweza kumsonga lakini hali ya uhakika wa kesho yake iliyojaa amani na tumaini la mbingu linakaa ndani yake.
Ni muhimu kuwa makini na utendaji wa mbingu katika maisha yako ( huduma/ shughuli unayoifanya).
Na mtu wa namna hii ( anayetambua chanzo na kukithamini ) uwa hana mashindano bali usimamia kwa ufasaha wajibu wake.
INAITWA SIKU! BARIKIWA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson……………………………………0764 018535