Ijumaa, 7 Juni 2019

HAKUNA UGUMU CHINI YA MAONGOZI YAKE!



“ kuna ugumu wa kupenda lakini hakuna ugumu kwa kinachopendwa”!

Unaweza kufika marekani kwa namna nyingi! Mathalani unaweza fika marekani katika mawazo yako na marekani iliyo katika uhalisia wake ( ukifika )…..ghafla unaweza kuichukia kwa kutaka kuishi marekani iliyo katika akili yako ( raha & starehe, maisha ya kifahari na ubora wa vitu na mambo yake ) pasipo kupata muongozo sahihi ya namna ya kuishi uko…………ni wazi kitu hicho kupata uharibifu ni jambo lisilo kwepeka.

Ndomana mara nyingi unaponunua kitu, bidhaa au mali fulani uwa kuna muongozo unapewa “menu book “ au karatasi kuhusu namna sahihi ya kutumia kifaa hicho.

Hata hesabu ikiwa imefumbwa kiasi gani hata ikatoa muonekano wa ugumu katika kupata jibu lake endapo ukabaini kanuni yake au namna ya kuanza na kuanza kupata mwelekeo basi hapo ugumu unaanza kupotea machoni pako, mathalani kanuni ya kufanya hesabu “ MAGAZIJUTO”
Na kuna msemo watu wanasema “ hakuna mkate mgumu mbele ya chai”

Karibu!!!

Katika maisha ya wokovu, watu wengi wanaipenda kutokana na matunda yake unapodumu katika wokovu, furaha ya Mungu, ulinzi wa Mungu pamoja na uzima wa milele, lakini kati hali hiyo unaweza kukuta watu wa aina tatu:
i.                    Wanaoacha wokovu
ii.                  Waliokosa mwelekeo
iii.                Wanaoimarika katika wokovu.

Ni jambo la kushangaza sana pindi unapoona kitu chenye manufaa kiasi hicho wapo wanatamani kuacha wokovu.

Sio furaha ya mchungaji wala kanisa katika kupunguza idadi ya watu kanisani bali ni kuwaongeza ili ufalme wa Mungu uzidi kujengeka, lakini hali hii ikitokea utokea tu kulingana na uimara ulionao katika wokovu.

Mathayo 7:24………………………………………………………
“Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba”

Usiishi katika wokovu kwa namna yako huku ukifuata hisia, matamanio pamoja na miemko yako bali tamani kuishi katika wokovu na mleta wokovu. ( unapoishi marekani usipende kuishi vyovyote bali tamani kujua wenyeji wanaishije! Wanapaswa kuishi vipi ).

Wokovu unakuwa sio mgumu pindi utakapoishi katika maongezi yake kweli ( Roho mtakatifu ), maana yeye ndiye anajua namna sahihi ya kuishi pindi unapokuwa ndani ya wokovu mengine yote yanapita. (mbwembwe, ushawishi wa maneno na mengine yote uwa kuna wakati unafika yanakosa nguvu tena)

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………………………….. 0764 018535

Jumamosi, 6 Aprili 2019

LIACHE KUSUDI LIVUTE MAMBO YAKE:



Ni jambo la fahari kwa mtu pindi anapofanya jambo akatambua kwanini anafanya hivyo au jambo hilo! Na litakuwa ni jambo la kushangaza kwa mtu awe anatia bidii sana na uku asijue kwanini anafanya hivyo.

Ni ukweli usiopingika pindi utakapoamua kulitumikia kusudi basi haki inayoambatana na hilo kusudi udhihirika au uweza kulipata.

Na ni jambo linakuwa gumu pindi utakapoanza kulitumikia kusudi uku ukiwa na matarajio yako ambayo ayaletwi na kusudi mathalani mtu unaweza ukajikuta katika shughuli za uvuvi lakini itakuwa ngumu kama moja ya kusudi lako ni kuvua swala mkubwa badala ya samaki.

Unapolitumikia kusudi uku akili yako ina mtazamo wako mbali na kusudi lilivyo ni ngumu kudumu na hilo kusudi au kuendelea na kusudi mathalani utakuta mtu anajitoa sana katika shughuli fulani akitegemea labda atapata pesa lakini pindi inapokuwa kinyume na matarajio utoshangaa kesho katoa udhuru wa kutoendelea na shughuli hiyo.

Biblia inasema “ hakuna aendaye vitani kwa gharama zake mwenyewe “.
1 Wakorintho 9:7 Ni askari gani aendaye vitani wakati wo wote kwa gharama zake mwenyewe? Ni nani apandaye mizabibu asiyekula katika matunda yake? Au ni nani achungaye kundi, asiyekunywa katika maziwa ya kundi?

Kusudi lenyewe linajua linahitaji nini ili liweze kudhihirika kwa hiyo ni muhimu ulitambue hilo na utoe nafasi lenyewe liite yaliyo yake sio swala la utendaji wa akili yako usio na uvuvio wake.
Ni muhimu kutambua kusudi lenyewe linaona kuliko macho ya nyama yanayoona, linajua chimbuko lake na hatima yake.

Uwezi kuchoka kama ukikubaliana na kusudi katika yale unayoyataka, kwa maana lenyewe kusudi linajua uhitaji wake.

Usipende kuishi katika maslahi yako pindi unapolitumikia kusudi bali ishi kwa matakwa ya kusudi bila shaka lenyewe litakutunza kukuimarisha maana ndilo matokeo au makusudi yake pindi utakapoamua kuishi katika hilo.

Kama unahitaji kuona fahari na ustawi wa familia na ukoo pamoja na watoto bila kusahau na wajukuu wako basi hunabudi kulitumikia kusudi ambalo Mungu ameliweka ndani yako.
Uzuri wa kusudi “ ukilitumikia nalo litakutumikia ila ukiliacha litakubwaga mazima “!

Nje ya kusudi uwezi kuona fahari ya wewe kuwepo duniani, kitu pekee ambacho kilicho mshawishi Mungu akuruhusu uje duniani ni kwa sababu ya hilo kusudi mbali na hilo hakuna kitu kingine.

Usiwe mjuaji sana katika kusudi maana utalitumia kwa namna yako ( kulitaka likutumikie baada ya wewe kulitumikia ) kwakuwa lenyewe lilivyoachiliwa linamaelekezo yote bali wewe kuwa mnyenyekevu na umakini wa kulisikiliza hapo utakua salama.

“ kuyapenda maisha yako ni kulipenda kusudi lililowekwa ndani yako “

INAITWA SIKU! BARIKIWA.

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson…………………………………………….0764 018535

Ijumaa, 8 Februari 2019

HUWEZI KUISEMEA KESHO KABLA UJAIONA LEO!



Ni jambo lisilo pingika kuwa “ fahari ya kesho inategemea maisha ya leo ” hivyo tunaifurahia jana kwakuwa tumeiona leo?

Karibu……….!!!

Japo zote tunahita kuwa ni siku lakini majina yao yanajitofautisha ndomana hii inaitwa KESHO na nyingine inaitwa LEO, na ujasiri wako wa kusema “ kesho tutaonana” ni kwasababu upo leo.
Mtu yeyote mwenye kiburi/ majivuno fulani, lazima pawepo na kitu kinachomfanya kuwa katika hali hiyo……hauwezi kuwa juu tu kama hakuna kitu kinacho kushikiria na kukufanya kuwa juu.

Unaweza kuipenda sana leo kwasababu ya kesho na pia unaweza kuichukia sana leo pindi utakapoifikiria kesho mathalani kijana anayejua kesho ndio siku yake ya harusi na yuko tayari uwa anaona kesho ni mbali kwa namna alivyopania na shauku iliyojaa moyoni mwake vilevile kwa mfungwa anayejua kesho ndio siku yake ya kunyongwa na anayapenda kuishi pindi atakapoifikiria kesho moyo wake utakuwa katika hali mbaya maana huzuni na simanzi vitakuwa vimeujaza moyo wake.

Ukiangalia maisha ya mkulima unaweza kujifunza kitu, unaweza kukuta mkulima anautesa mwili wake akiamka alfajiri na kwenda kulima, akihusisha na uchumi wake katika kununua vifaa bora, mbegu bora na hata mbolea lakini katika maumivu hayo bado akawa amejawa na furaha na matumaini pindi atakavyoifikiria kesho katika mavuno yake!

Kabla ujajitamba kwa ajili ya kesho ni muhimu uwe na leo imara inayoweza kukuweka katika hatua bora kesho, japo wakati mwingine ni ngumu sana kuitafsiri kesho kwasababu ya leo……….sio siku zote unapoona leo umeshiba basi ukajua kesho utashiba hivyo hivyo.

Maana wapo wanaoishi leo kanakwamba hakuna kesho na pindi leo ikianza kuyoyoma na kesho ikianza kuchomoza hapo uweza kumfanya mtu kuwa na maswali yaliyo kosa jibu kwakuwa hakujiandaa kwa ajili ya kesho.

Jifunze kuiona leo vizuri ili ije kesho iliyo nzuri, kwakuwa ukiichukia leo sio rahisi kuipenda kesho kwa maana kesho ni matokeo ya leo naam ni ngumu tu kuuchukia mwembe ukayapenda maembe kwakuwa mwembe unaotoa maembe mazuri huo utunzwa sana na wakati mwingine ata ulinzi uwekewa.

Na ni kawaida hauwezi kuyafanya makubwa kama ujaanza na madogo, kwahiyo usidharau moja ukapenda miamoja  pasipo kujua unaanza na moja ndiyo itakupeleka kwenye mia moja.
Unapoiona kesho usifikiri tu itakuwa  tu kesho ni muhimu utambue kuwa kabla ya kesho kulikuwa na juzi, jana na leo hatimaye itakupelekea kesho hivyo usione kesho kama kitu pekee kuwa unaweza kukipata pasipo kuitambua leo.

Japo usipoitambua leo ukaikulupukia kesho basi hapo utakapokuwa umeingia kesho utaanza kuona mapungufu yake na kuona kama umekosea kwakuwa ukuitendea vyema jana yake. Ni muhimu kutoitamani kesho maana kesho itakuja tu maadam leo ikisha malizika,

Ipende sana leo na uhakikishe imekaa vizuri maana ikiwa leo iko vizuri itakuwa sawa maana ni sawa na kutengeneza msingi wa ghorofa haraka haraka pasipo kuzingatia vigezo vyake ili msingi uwe imara na pindi baada ya kumaliza ujenzi muda si msingi ukalemewa na kuanza kuporomoka wewe unaweza kushangaa lakini uhalisia utazungumza.

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:
Cothey  Nelson……………………………… 0764 018535