Ijumaa, 8 Februari 2019

HUWEZI KUISEMEA KESHO KABLA UJAIONA LEO!



Ni jambo lisilo pingika kuwa “ fahari ya kesho inategemea maisha ya leo ” hivyo tunaifurahia jana kwakuwa tumeiona leo?

Karibu……….!!!

Japo zote tunahita kuwa ni siku lakini majina yao yanajitofautisha ndomana hii inaitwa KESHO na nyingine inaitwa LEO, na ujasiri wako wa kusema “ kesho tutaonana” ni kwasababu upo leo.
Mtu yeyote mwenye kiburi/ majivuno fulani, lazima pawepo na kitu kinachomfanya kuwa katika hali hiyo……hauwezi kuwa juu tu kama hakuna kitu kinacho kushikiria na kukufanya kuwa juu.

Unaweza kuipenda sana leo kwasababu ya kesho na pia unaweza kuichukia sana leo pindi utakapoifikiria kesho mathalani kijana anayejua kesho ndio siku yake ya harusi na yuko tayari uwa anaona kesho ni mbali kwa namna alivyopania na shauku iliyojaa moyoni mwake vilevile kwa mfungwa anayejua kesho ndio siku yake ya kunyongwa na anayapenda kuishi pindi atakapoifikiria kesho moyo wake utakuwa katika hali mbaya maana huzuni na simanzi vitakuwa vimeujaza moyo wake.

Ukiangalia maisha ya mkulima unaweza kujifunza kitu, unaweza kukuta mkulima anautesa mwili wake akiamka alfajiri na kwenda kulima, akihusisha na uchumi wake katika kununua vifaa bora, mbegu bora na hata mbolea lakini katika maumivu hayo bado akawa amejawa na furaha na matumaini pindi atakavyoifikiria kesho katika mavuno yake!

Kabla ujajitamba kwa ajili ya kesho ni muhimu uwe na leo imara inayoweza kukuweka katika hatua bora kesho, japo wakati mwingine ni ngumu sana kuitafsiri kesho kwasababu ya leo……….sio siku zote unapoona leo umeshiba basi ukajua kesho utashiba hivyo hivyo.

Maana wapo wanaoishi leo kanakwamba hakuna kesho na pindi leo ikianza kuyoyoma na kesho ikianza kuchomoza hapo uweza kumfanya mtu kuwa na maswali yaliyo kosa jibu kwakuwa hakujiandaa kwa ajili ya kesho.

Jifunze kuiona leo vizuri ili ije kesho iliyo nzuri, kwakuwa ukiichukia leo sio rahisi kuipenda kesho kwa maana kesho ni matokeo ya leo naam ni ngumu tu kuuchukia mwembe ukayapenda maembe kwakuwa mwembe unaotoa maembe mazuri huo utunzwa sana na wakati mwingine ata ulinzi uwekewa.

Na ni kawaida hauwezi kuyafanya makubwa kama ujaanza na madogo, kwahiyo usidharau moja ukapenda miamoja  pasipo kujua unaanza na moja ndiyo itakupeleka kwenye mia moja.
Unapoiona kesho usifikiri tu itakuwa  tu kesho ni muhimu utambue kuwa kabla ya kesho kulikuwa na juzi, jana na leo hatimaye itakupelekea kesho hivyo usione kesho kama kitu pekee kuwa unaweza kukipata pasipo kuitambua leo.

Japo usipoitambua leo ukaikulupukia kesho basi hapo utakapokuwa umeingia kesho utaanza kuona mapungufu yake na kuona kama umekosea kwakuwa ukuitendea vyema jana yake. Ni muhimu kutoitamani kesho maana kesho itakuja tu maadam leo ikisha malizika,

Ipende sana leo na uhakikishe imekaa vizuri maana ikiwa leo iko vizuri itakuwa sawa maana ni sawa na kutengeneza msingi wa ghorofa haraka haraka pasipo kuzingatia vigezo vyake ili msingi uwe imara na pindi baada ya kumaliza ujenzi muda si msingi ukalemewa na kuanza kuporomoka wewe unaweza kushangaa lakini uhalisia utazungumza.

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:
Cothey  Nelson……………………………… 0764 018535