Katika dunia tuliyonayo sasa, mambo mengi yanatokea yanakuwa yanaongeza maswali vichwani mwa watu baada ya kutoa majibu: katika dunia ya sasa kuna ongezeko kubwa la watu kujitoa uhai, kujijeruhi binafsi na matukio mengi ambayo kwa hali ya kawaida hautegemei binadamu wa kawaida kufanya hayo mambo lakini unakuta yanatokea na kuongezeka kila iitwayo leo,
Na wataalamu wengi wakifanya uchunguzi wanajikita katika kujua au kuhisi chanzo chake na kutoa utatuzi wa mambo haya yanayo wakumba wanadamu lakini bado inakuwa sio tiba ya kudumu katika jamii husika.
Naam! Moja ya kitu ambacho binadamu wa kawaida/mwenye akili timamu hawezi kufanya ni kujipinga ingawa anaweza kujikuta katika hali hiyo kwa kujua au kuto kujua.
Kama mtu unaishi haijalishi una mjua Mungu au haumjui Mungu kuna wewe katika hali ya ndani na kuna wewe katika hali ya nje! Na vyote vinakukamilisha wewe au kutoa picha yako kwa jamii.
Kwa maana rahisi kuwa wewe ulivyo hasa ( ulivyotengenezwa kuwa ) na vile unavyoona katika mtazamo wa akili baadaa ya kushawishiwa na macho yako.
Mathalani, unaweza kukuta wewe katika hali yako ya ndani wewe ni maalum kwa ajili ya kutengeneza vinyago na ukitengeneza moyo wako unakuwa burudani lakini ukakuta unaingia katika kucheza mziki hali hiyo ikakupa mpingano mkubwa katika hali ya ndani na ya nje na unaweza kufika mahali hata kushindwa kujua kuwa unaendelea mbele au upo palepale/hapohapo.
Pia katika uwanja wa uimbaji kuna vitu vitatu: performer ( mchezaji ), singer ( muimbaji ), worshiper ( mwabudu ) hawa wote wanaweza kuwa katika uwanja wa uimbaji ( music industry ) lakini hawaingiliani na pindi ikatokea mchezaji akatamani kuimba na pindi atakapoanza kuimba utaona makosa mengi kwa mtu asiyekuwa na talanta hiyo na hata akashindwa kuimba katika katika kiwaango/namna anayotakiwa.
- Japo mchezaji na mwimbaji wote hawa wanaweza kuwa waabudu katika namna zao.
Ni hatari sana pale utakapoishi maisha ya kujipinga ( kuwa/kufanya tofauti na ulivyopaswa kufanya ) kutokana na kuogopa watu au kuangalia maslahi yako zaidi na fursa inayoonekana na kujisahau wewe na uwezo ambao Mungu amekupa kutumika katika eneo gani,
- Pindi ikatokea upingamizi katika jambo hilo unalolifanya lisilo na shikama na hatma yako bila shaka hautaweza kushinda hali hiyo hata kama ukipambana vipi.
Unaweza kukuta mtu ni mbobezi wa kutengeneza script lakini ukajikuta anaingia katika uigizaji au kucheza filamu ambayo hafiti eneo hilo bila shaka anaweza kuharibu au akapoteza mvuto wa hiyo filamu kwa kuwepo mtu ambaye akupaswa kuwepo hata kama yeye yuko kwenye industry kwa miaka mingapi?
- Na tambua kuna baadhi ya watu wanahitaji maboresho au maelekezo ili waweze kuwa kitu bora au kizuri lakini ni kwa wale wenye hiyo talent sio kulazimisha talent.
Pia unaweza kukuta mtu mwenye kalama ya ufundishaji ( mwalimu ) akatamani kalama ya kutoa unabii bila shaka anaweza kujitahidi kuendana na wenye kalama ya unabii lakini muda si mrefu watu watatambua kuwa yeye hayuko na kalama ya unabii,
- Moja dalili ya kufanya kitu kisichokuwa chako upelekea hali ya juu katika matumizi makubwa ya akili ya kuhakikisha unalinda unachokifanya na wala sio kukiboresha.
Kufanya kitu ambacho sio chako ni sawa na kuvaa nguo isiyokutosha vizuri muda wote utakuwa ujiamini.
Unapotumia muda mwingi kufanya kitu kisichokuwa chako ni matumizi mabaya ya muda, maana ingekuwa bora/vyema kutumia muda huo kukiboresha na kukikuza ( kwa kuongeza maarifa yahusiyo hiyo talanta iliyondani yako ).
Ni muhimu ujivumbue ili ujiishi na uone raha ya wewe kuwepo duniani, pia inasaidia kujua nafasi ya wengine na kuwawezesha wengine kufanya.
Unapofanya kitu ambacho ni chako bila shaka makosa yatakuwa madogo sana na hata kushindwa kuonekana machoni pa watu kwa ukubwa.
Kufanya kitu ambacho akikutambulishi wewe ni sawa na mtu anayetamani kuzama kwenye maji kwa muda mrefu na huku akiwa hana pumzi ya kutosha kumudu muda huo, hivyo atakapoanza hilo zoezi kwa muda mchache sana utakuta ameinua kichwa juu huku akihema kwa harakaharaka kama mtu aliyenusirika kufa.
Ni kusudi la Mungu usijipinge hata kama kile ulichopewa akina mvuto kuliko vingine bali ishi hapo maana kwa kuishi hapo unaweza kuyafurahia maisha yako na kumshukuru Mungu kwa kukuumba na kukuweka hapo.
INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson………………………………………………………………………..0764 018535