Ijumaa, 1 Machi 2024

UBORA WA AKILI YAKO UTAKUMBULISHA:

 



Moja ya shukrani ambayo mwanadamu anayotakiwa kumpa Mungu ni kupewa akili inayomtambulisha kama binadamu, kwakuwa amemuumba kisha akampa akili ambayo inaweza kumsaidia kumtambulisha na yeye kujitambua,

Ni kweli kila kiumbe kimepewa akili ya namna yake mathalani mnyama ana akili zake, ndege na wanadudu wana akili zao na moja ya kazi kubwa ya akili ni kumuongoza mtu katika kuamua nini afanye na nini asifanye.

Kwa ujumla hakuna mtu asiye na akili bali utegemea matumizi ya mtu katika hiyo akili katika matumizi bora au mazuri na hapo anakuwa wa faida katika jamii lakini kwa matumizi mabaya basi hapo anakuwa janga  katika jamii yake.

Japo darasani ni lazima atokee mwanafunzi wa kwanza na mwisho lakini sio kweli kuwa mwanafunzi aliyekuwa wa mwisho basi hana akili kama wengine wasemavyo na kuamini atakuwa wa mwisho kila kitu.

Kila mtu anayo nafasi ya kuifanya akili yake kuwa ni kitu bora chenye manufaa kwake na kwa jamii yake.

Unapaswa kujua kuwa Mungu alikuamini ndo mana akakupa hiyo akili haijalishi unaielewa au hauielewi.

Lakini Mungu amekupa hiyo akili akijua utoshelevu wako utazaliwa na hiyo akili kupitia yeye!

Ukiitumia hiyo akili vizuri kwa hakika utaifurahia hiyo hatua uliyopo au unayoelekea mathalani ndege kuku yeye ufurahia kila kitu anachokifanya hatakama kesho atachinjwa lakini yeye uhakikisha leo yake ameitumia vizuri tena katika kiwango kikubwa cha akili yake.

Ni kweli hauwezi kuwa wa maana kama ujatambua matumizi sahihi ya akili yako,

Ni muhimu utambue ndani ya akili kuna kuona kule/pale ulipo au kule unakoelekea kunahitaji nini japo wakati mwingine unaweza usipate njia sahihi ya kufika hapo lakini tambua Mungu ameachilia hiyo neema ya kufika.

Kwa kiasi kikubwa unapomuona mtu yupo katika hatua njema/nzuri  ( nje ya utajiri wa kipepo) bila shaka ujue hayo ni matokeo ya ubora wa akili yake, kwakuwa ubora wa akili unapodhihirika katika mwili ndipo hapo mnayaona hayo matokeo.

Tatizo linakuja pale unapotaka/unapoanza kuyataka mafanikio yake pasipo kujua ubora wa akili yake ni tofauti  na akili yako, kuna upekee wake uliosababisha kuwa hapo.

Ni kweli watu wote mnaweza kuwa wafanyabiashara wa mbao na watu wote mkafanikiwa inawezekana hawa wakafanikiwa kwa kuuza mbao nje ya nchi na wengine wakafanikiwa kwa kuuza mbao ndani ya nchi hivyo uonyesha upekee wao katika matumizi ya akili lakini katika kila mtu kwa ubora wake,

Naam ni ukweli usiopingika kuwa unaweza kujifunza kwa waliofanikiwa katika matumizi sahihi ya muda, bidii, uaminifu na mengine mengi lakini usipojifunza katika ubora wa utendaji wake uliozaliwa katika akili yake kwa maana huyo ni yeye sawa na upekee ambao Mungu amemjalia,Lakini utakapoanza kutembea katika akili yake jua hapo utataka kuishi kama yeye anavyoishi na hapo ndipo makosa mengi yanaanza kutokea na hata kupelekea kuishia njiani!

Kwakua hauwezi kuishi kwenye akili ya mtu alafu ukajipata bali ukiishi kwenye akili ya Mungu hapo utajipata na kujua namna yako,

INAITWA KESHO! BARIKIWA SANA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson……………………………………………………………………………………………………..0764 018535