Ijumaa, 13 Machi 2026

AKILI NJEMA

 



Akili katika maisha ya mwanadamu imegawanyika katika sehemu tatu katika dhana ya kufikirika:

i. Akili katika hali ya kutegemea

ii. Akili katika hali ya kujitegemea

iii. Akili katika hali ya kutegemewa

Awa ni watu watatu tofauti wenye utendaji tofauti kabisa na upeo tofauti kabisa katika kuyakabili mambo/kuyaendea mambo.

Akili nayo inatabia ya kukua kutoka katika hali moja na kwenda hali nyingine ( ongezeko la ufahamu ).

Ni kama maisha ya mwanadamu uanza kwanza kwa kutegemea alafu ujikuta katika hali ya kujitegemea mwishowe anakabaliwa na majukumu ya kutegemewa hapa ndipo akili inabeba mzigo mzito.

Bila shaka usipokuwa makini unaweza kujikuta unakuwa mahali ambapo haukupaswa kuwa au haukutakiwa kuwa.

Kuna wakati akili yako isipotaka kujitegemea, mazingira yanaweza kutengeneza hali ambayo itailazimisha akili ianze kujitegemea japo mwanzoni kunakuwa na hali ya maumivu sawasawa na kuingizwa mahala ambapo hukutegemea kuwepo mpaka ukubaliane na mazingira unakuwa umeshaumia sana/vyakutosha ( mtu anapoenda uabuni kwa mara ya kwanza kusoma au kufanya kazi anakumbana na mazingira ambayo sio rafiki lakini baadae anawezakuyaelewa hayo mazingira ).

Tuangalie akili katika hali zake:

I. AKILI KATIKA HALI YA KUTEGEMEA

Ni hali ya kujua huwezi kusimama peke yako bila kushikwa mkono na mtu.

Ni sawasawa na biashara ambayo haiwezi kusimama yenyewe au kujiendesha bila usaidizi kutoka nje.

- Hali hii inapaswa kuwa ni hali ya kitambo na wala sio ya mwendelezo.

Usipokuwa makini unaweza kujikuta huko katika hali hii hata unapoingia miaka 50 na ukaona hali ya ushwari pasipo kujua hayo maisha hupaswi kukaa.

Ni maisha mazuri kimuonekano lakini ni maisha yanayo nyima pontetial yako kuonekana na kuwa faida kwa wengine ( uwezo wako wa kufanya mambo unakuwa ni mdogo au hauonekani )

- Katika hali hiii mwanamke au mwanaume anapoteza sifa ya kuwa katika ndoa, mazingira haya yanaondoa ubora wako kabisa.

Huwezi kunawiri katika akili hii

Ukiwa katika hali hii ukiachwa mahali utakutwa hapo hapo hata kama imebaki sehemu ndogo ya kufanikisha hilo jambo.

- Maisha ya utumwa yanazaliwa katika akili hii.

II. AKILI KATIKA HALI YA KUTEGEMEA

Hapa akili imeingizwa katika ulimwengu mgeni na hivyo akili imeanza kukubaliana na kutengenezwa.

Hichi ni kipindi cha kuanza kusimama mwenyewe kabla ujaanza kusimamisha wengine.

- Hiki ni kipindi ambacho unaanza kujitambua wewe ni nani hasa na unapaswa kufanya nini?

Ni kipindi ambacho kinawapa wakati mgumu  watu wengi kukuelewa kwa namna unavyoenenda.

- Kuna baadhi ya mambo yatakuwa mapya kwako na kwao na hivyo kukupelekea wao kukushangaa na wakati mwingine hata wewe kujishangaa.

Kuna mambo ulikuwa unayasikia sasa hapo wewe unaanza kuyashuhudia yakitokea katika maisha yako.

Kuna baadhi ya mambo ulikuwa unashangaa kuona watu wanafanya/kusema sasa katika hali hii au hatua hii utaanza kujua sababu ya hayo kuwa hivyo.

- Unapaswa kuwa makini sana maana katika kipindi hiki unaweza kujenga hatma yako au kuharibu maana katika kujifunza mambo mageni unaweza kuharika badala kujengeka.

Hichi ni kipindi ambacho mfumo mzima wa maisha yako unaanza kubadilika kama ulikuwa unakaa sasa unaaza kusimama na hatimaye kutembea.

Nikipindi ambacho wewe binafsi unajipa nafasi kubwa katika kujitafakari.

- Kama ulikuwa na maono basi sasa unaanza hatua ya kwanza kuelekea kutimiza maono yako.

III. AKILI KATIKA HALI YA KUTEGEMEWA

Sasa hapa akili yako inaanza kuyafanya maisha yako kuishi kwa ajili ya wengine.

- Katika hatua hii gharama kubwa unaingia sio kwa ajili yako bali kwa wale wanaokuzunguka.

Hapa ndipo hata kama mwili wako hauko sawa itakulazimu kusimama na kufanya au akili yako itakuambia jitie nguvu uende maana wako watu wanakutegemea ili maisha yao yaende.

- Hapa mtu anaweza kuwa na kikao cha peke yake hata akiwa barabarani.

Endapo utashindwa kutimiza majukumu kwa wale watakao kuzunguka huweza kuchukua maamuzi ambayo watu wanaweza kushangaa na kuanza kujiuliza hivi ni yeye yule tunaye mfahamu au mwingine.

Ni kipindi ambacho unahitaji kujielewa sana ama kuwa na akili ya ukomavu .

Ni hapa kama una makosa ukiyafanya unaweza kuhisi dunia nzima wanakuzomea, ama kuhisi huko uchi mbele za watu.

Ni akili ambayo unapaswa kuwa nayo katika kuwafanyia mema kwa wale wanaokutegemea kama wewe ulivyo fanyiwa mema ( sio wote ) na hatimaye ukawa pale ulipo, ( hata kama ujapata nafasi ya kufanyiwa mema lakini bado unayo nafasi ya kuwafanyia mema wale wakupendao )

 

INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA

 

Imeandaliwa na:

Cothey Nelson………………………………………………………………………………..0764 018535