Ijumaa, 13 Februari 2026

USIOGOPE


 

Moja ya neno nzuri ambalo linawapa hatua mpya au kuendelea zaidi pindi watu wanapolisikia ni neno USIOGOPE.

Japo kuna wakati unaweza kukosa nguvu katika mambo yanayokukabili, unaweza kuona  yanakuzidi nguvu lakini hata hapo unaambiwa USIOGOPE inakuwa sawasawa na gari lililokosa/lililopoteza mwelekeo kwa sababu ya kukosa brake likielekea kwenye maporomoko lakini hata katika hali hiyo unaambiwa usiogope, japo kuna wakati unaweza kupoteza maana halisi ya hili neno maana  unaweza kuona kama  unakikabili kifo chako.

Duniani kuna mambo mengi yanayotisha na kuogopwa sana sio yale yanayoendelea katika maisha yako binafsi tu bali hata yale yanayoendelea katika jamii yako ama duniani.

Unapaswa kujua neno pekee linaloweza kumwingiza Mungu katika utendaji ni kutoogopa ambalo linakua zao kuamini.

Hauwezi kushindwa kuogopa katika mazingira yanayotaka uyaogope isipokuwa umejua kwanini usiogope au umepata uhakika na kuwa salama katika hayo mazingira.

Moja ya mateso mengi kwa watu ni zao la kuogopa, na kuogopa ni rafiki wa hofu.

Wako watu wameshindwa kubeba ujauzito kwasababu ya hofu, kwa kuhofia je! Atakuwa salama kweli au hata hatarisha maisha yake.

Wako wameshindwa kufanya mambo makubwa kwa sababu ya hofu, nafasi zinaweza kuja na kukupa hatua nyingine au kukupa ushuhuda lakini unaweza kushindwa kufanya kwa sababu unahofia je ikishindwa kufanikiwa je! Nitakuwa mgeni wa nani? Mathalani kuna nafasi zinatokea unatakiwa uwekeze hela zako nawe unazo lakini unahisi je! Zisizoporudi nitakuwa katika nafasi ipi?

Kuthubutu kunaweza kukufanya ufanye mambo makubwa au uwe katika namna nyingine lakini hofu imekuwa kikwazo cha wewe kufika hapo.

Yakupasa kujua kwamba hakuna mabadiliko yasiyokuwa na gharama hivyo unavyoogopa kufanya mabadiliko kwa kuhofia gharama utakazoingia bila shaka kuvuka ng’ambo inaweza kuwa ni vigumu.

Wako watu wameogopa kuingia huko kutokana na yale yanayoendelea katika jamii manyanyaso, mateso na magonjwa yanayozaliwa kutokana na hali hizo.

Tambua usipobadilika maisha yako hayawezi kubadilika ufahamu wako utakuwekea mipaka.

Mambo mengi yanategemea ni utulivu wa akili yako na namna unavyomtanguliza Mungu pasipo kuweka matamanio yako mbele.

Japo kuwa nyuki wanang’ata na wanaweza kuua lakini watu hawaachi kulima asali.

 

INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA

 

Imeandaliwa na:

 

Cothey Nelson……………………………………………………………………………….0764 018535

Ijumaa, 16 Januari 2026

UKIJUA UMESHINDA

 



Neno “ KUJUA” linakupa kuweza, kufanya kitu katika usahihi na ustawi.

Hali ya kujua inakupa kufanya kitu kwa ujasiri na umakini mzuri.

“ ukijua umeshinda”

Ni muhimu utafute kujua zaidi kwanza kabla ya kutafuta ushindi maana kujua kuna kupa wepesi wa kushinda.

Mathalani. Katika maisha ya mwanafunzi unapopewa mitihani kama vile wa hesabu usipambane kuandika jibu bali tafuta kujua njia ya kufanya ili ikupeleke kwenye JIBU.

Tuna amini ukifanya jambo katika kujua makosa upungua ama ukosekana kabisa.

Unapaswa kujua siri ya kushinda imebebwa na kujua, hivyo ukifanikiwa kujua basi umefanikiwa kushinda.

Ukishinda kwa kujua unapunguza migogoro baini ya watu na watu maana kushinda kwa kujua kunakupa ulinzi dhidi ya maadui zako.

“ mfalme wa ulimwengu huu anakuja lakini hana kitu kwangu” yesu

Yohana 14:30 Mimi sitasema nanyi maneno mengi tena, kwa maana yuaja mkuu wa ulimwengu huu, wala hana kitu kwangu.

Yesu anaonyesha nguvu ya kujua inampa ujasiri wa kushinda mazingira yote.

Baada ya kujua lazima upate neema ya utatuzi bila neema hiyo  unaweza kuharibu zaidi baada ya kupata ushindi.

Wako watu baada kujua mambo magumu yaliyofichwa yamepelekea kuwa katika mazingira magumu.

Wako watu wameingia katika migogoro mikubwa, magonjwa na hata chuki zisizoisha na hata hizo chuki kupelekea kula mioyo ya watu taratibu.

Unapotambua mitego mibaya imeandaliwa kwa ajili ya kuharibu maisha yako haupaswi kufanya maamuzi ya haraka yasiyo na muelekeo sahihi.

Unapaswa kujua kwamba kutambua jambo linaloendelea ni hatua moja ya ushindi, hivyo upaswi kuamaki na kukulupuka maana unaweza kukuta unashindwa baada ya kushinda.

Maana kujua ni dalili ya ushindi hivyo hakikisha unashinda!

“ taifa lilikuwa likipigana na Israel wanajikuta kila walipangalo linajulikana na kupelekea kushindwa”

Kupitia Elisha mtumishi wa Mungu katika kujua katika yale yanayoendelea juu ya israeli, israel walikuwa salama wala hakuna shida iliendelea kuwatesa.

2 wafalme 6:1 Kisha, wana wa manabii wakamwambia Elisha, Angalia basi, mahali tukaapo mbele yako ni padogo kwetu.

 2 Basi twende mpaka Yordani, twakuomba, tutwae huko kila mtu mti mmoja, ili tujifanyie huko mahali pa kukaa. Akajibu, Haya! Nendeni.

 3 Mmoja wao akasema, Uwe radhi, basi nakusihi, uende pamoja na watumishi wako. Akajibu, Nitakwenda.

 4 Basi, akaenda pamoja nao. Nao walipofika Yordani, wakakata miti.

 5 Lakini mmojawapo alipokuwa katika kukata boriti, chuma cha shoka kikaanguka majini; akalia, akasema, Ole wangu! Bwana wangu, kwani kiliazimiwa kile.

 6 Mtu wa Mungu akasema, Kilianguka wapi? Akamwonyesha mahali. Akakata kijiti, akakitupa pale pale, chuma kikaelea.

 7 Akasema, Kiokote. Basi akanyosha mkono, akakitwaa.

 8 Basi, mfalme wa Shamu alikuwa akifanya vita na Israeli. Akafanya mashauri na watumishi wake, akasema, Kituo changu kitakuwapo mahali fulani.

 9 Yule mtu wa Mungu akapeleka habari kwa mfalme wa Israeli, kusema, Jihadhari, usipite mahali fulani; kwa sababu ndiko wanakoshukia Washami.

 10 Mfalme wa Israeli akapeleka watu mpaka mahali pale alipoambiwa na yule mtu wa Mungu, na kuhadharishwa; akajiokoa nafsi yake, si mara moja, wala si mara mbili.

 11 Basi mfalme wa Shamu moyo wake ukamfadhaika sana kwa ajili ya jambo hili; akawaita watumishi wake, akawaambia, Je! Hamtanionyesha, ni mtu yupi miongoni mwenu aliye upande wa mfalme wa Israeli?

 12 Mmojawapo wa watumishi wake akasema, La, bwana wangu, mfalme; lakini Elisha, yule nabii aliye katika Israeli, humwambia mfalme wa Israeli maneno uyanenayo katika chumba chako cha kulala.

 13 Akasema, Enendeni, mkamwangalie aliko, nipate kupeleka watu kwenda kumchukua. Akaambiwa ya kwamba, Tazama, yuko Dothani.

 14 Kwa hiyo akapeleka huko farasi, na magari, na jeshi kubwa; wakafika usiku, wakauzingira mji ule pande zote.

 15 Hata asubuhi na mapema mtumishi wake yule mtu wa Mungu alipoondoka, na kwenda nje, kumbe! Pana jeshi la watu, na farasi na magari, wameuzingira mji ule. Mtumishi wake akamwambia, Ole wetu! Bwana wangu, tufanyeje?

 16 Akamjibu, Usiogope; maana walio pamoja nasi ni wengi kuliko wale walio pamoja nao.

 17 Elisha akaomba, akasema, Ee Bwana, nakusihi, mfumbue macho yake, apate kuona. Bwana akamfumbua macho yule mtumishi; naye akaona; na tazama, kile kilima kilikuwa kimejaa farasi na magari ya moto yaliyomzunguka Elisha pande zote.

 18 Na walipomtelemkia Elisha akamwomba Bwana, akasema, Uwapige, nakusihi, watu hawa kwa upofu. Akawapiga kwa upofu sawasawa na neno la Elisha.

 19 Elisha akawaambia, Njia hii siyo, na mji huu sio, nifuateni mimi, nami nitawapeleka kwa mtu yule mnayemtafuta. Akawapeleka Samaria.

 20 Hata walipokwisha kuingia Samaria, Elisha akasema, Bwana wafumbue macho watu hawa, wapate kuona. Bwana akawafumbua macho wakaona; kumbe! Walikuwa katikati ya Samaria.

 21 Naye mfalme wa Israeli alipowaona, akamwambia Elisha, Ee baba yangu, niwapige? Niwapige?

 22 Akamjibu, Usiwapige; je! Ungetaka kuwapiga watu ambao umewatwaa mateka kwa upanga wako na uta wako? Weka chakula na maji mbele yao, wapate kula na kunywa, na kwenda kwa bwana wao.

 23 Basi akawaandalia chakula tele; nao walipokwisha kula na kunywa, akawaacha, wakaenda zao kwa bwana wao. Na vikosi vya Shamu havikuja tena katika nchi ya Israeli.

Mambo mengi yanapokusonga unapaswa kutafuta kujua utatuzi uliosalama utakao kufanya kuibuka mshindi katika mazingira yanayo kuzunguka maana ni kusudi la Mungu uwe ushuhuda ili kudhihirisha penzi la Mungu kwa wanadamu.

Lazima uwe na nia ya kuta kuwa wewe uwe salama pasipo na nia ya kumwaibisha mtu maana nia hiyo inaweza kuondoa hali ya Mungu kuwa upande wako.

 

INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA.

 

Imandaliwa na:

 

Cothey  Nelson………………………………………………………………………….0764 018535

Ijumaa, 1 Machi 2024

UBORA WA AKILI YAKO UTAKUMBULISHA:

 



Moja ya shukrani ambayo mwanadamu anayotakiwa kumpa Mungu ni kupewa akili inayomtambulisha kama binadamu, kwakuwa amemuumba kisha akampa akili ambayo inaweza kumsaidia kumtambulisha na yeye kujitambua,

Ni kweli kila kiumbe kimepewa akili ya namna yake mathalani mnyama ana akili zake, ndege na wanadudu wana akili zao na moja ya kazi kubwa ya akili ni kumuongoza mtu katika kuamua nini afanye na nini asifanye.

Kwa ujumla hakuna mtu asiye na akili bali utegemea matumizi ya mtu katika hiyo akili katika matumizi bora au mazuri na hapo anakuwa wa faida katika jamii lakini kwa matumizi mabaya basi hapo anakuwa janga  katika jamii yake.

Japo darasani ni lazima atokee mwanafunzi wa kwanza na mwisho lakini sio kweli kuwa mwanafunzi aliyekuwa wa mwisho basi hana akili kama wengine wasemavyo na kuamini atakuwa wa mwisho kila kitu.

Kila mtu anayo nafasi ya kuifanya akili yake kuwa ni kitu bora chenye manufaa kwake na kwa jamii yake.

Unapaswa kujua kuwa Mungu alikuamini ndo mana akakupa hiyo akili haijalishi unaielewa au hauielewi.

Lakini Mungu amekupa hiyo akili akijua utoshelevu wako utazaliwa na hiyo akili kupitia yeye!

Ukiitumia hiyo akili vizuri kwa hakika utaifurahia hiyo hatua uliyopo au unayoelekea mathalani ndege kuku yeye ufurahia kila kitu anachokifanya hatakama kesho atachinjwa lakini yeye uhakikisha leo yake ameitumia vizuri tena katika kiwango kikubwa cha akili yake.

Ni kweli hauwezi kuwa wa maana kama ujatambua matumizi sahihi ya akili yako,

Ni muhimu utambue ndani ya akili kuna kuona kule/pale ulipo au kule unakoelekea kunahitaji nini japo wakati mwingine unaweza usipate njia sahihi ya kufika hapo lakini tambua Mungu ameachilia hiyo neema ya kufika.

Kwa kiasi kikubwa unapomuona mtu yupo katika hatua njema/nzuri  ( nje ya utajiri wa kipepo) bila shaka ujue hayo ni matokeo ya ubora wa akili yake, kwakuwa ubora wa akili unapodhihirika katika mwili ndipo hapo mnayaona hayo matokeo.

Tatizo linakuja pale unapotaka/unapoanza kuyataka mafanikio yake pasipo kujua ubora wa akili yake ni tofauti  na akili yako, kuna upekee wake uliosababisha kuwa hapo.

Ni kweli watu wote mnaweza kuwa wafanyabiashara wa mbao na watu wote mkafanikiwa inawezekana hawa wakafanikiwa kwa kuuza mbao nje ya nchi na wengine wakafanikiwa kwa kuuza mbao ndani ya nchi hivyo uonyesha upekee wao katika matumizi ya akili lakini katika kila mtu kwa ubora wake,

Naam ni ukweli usiopingika kuwa unaweza kujifunza kwa waliofanikiwa katika matumizi sahihi ya muda, bidii, uaminifu na mengine mengi lakini usipojifunza katika ubora wa utendaji wake uliozaliwa katika akili yake kwa maana huyo ni yeye sawa na upekee ambao Mungu amemjalia,Lakini utakapoanza kutembea katika akili yake jua hapo utataka kuishi kama yeye anavyoishi na hapo ndipo makosa mengi yanaanza kutokea na hata kupelekea kuishia njiani!

Kwakua hauwezi kuishi kwenye akili ya mtu alafu ukajipata bali ukiishi kwenye akili ya Mungu hapo utajipata na kujua namna yako,

INAITWA KESHO! BARIKIWA SANA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson……………………………………………………………………………………………………..0764 018535

Ijumaa, 16 Februari 2024

UZURI WA HATUA MPYA:

 



Kwa mzazi mwenye mapenzi ya kweli kwa mwanae uwa anakuwa na furaha kubwa katika kila mabadiliko yanayofanyika katika ukuaji wa mwanae mathalani kutoka hatua ya kulala kuanza hatua ya kukaa….na moja ya hatua inayompa furaha mzazi kuona mwanae ameanza kupiga hatua au kutembea, kwani hapo anaweza kuwa msaidizi wa mahitaji madogo madogo kwake kama vile kumtuma akachukue kitu fulani ndani ya nyumba hadi dukani.

Naam hatua mpya ni shauku ya waliowengi kwa maana inaaminika katika hatua mpya kuna maongezeko, pia tunaweza sema kama uzuri wa kujifungua japo kuna maumivu lakini tunaita ni uzuri kwa sababu ya matokeo yake, kupakata mwana…………na heshima katika jamii inayokuzunguka.

Ni kama mlizi anavyoingojea asubuhi kwa hali ya shauku ndivyo ilivyo kwa mtu anayengojea hatua inayofuata kwa makamio yote.

Ni kama uzuri wa kutimiza ndoto yako ambayo ulikuwa unaitamani siku nyingi, inapotimia inageuza siku yako na kuwa hali nyingine iliyo njema.

Hatua ya juu au mpya ni kitu kinachofurahiwa na kupendwa na watu wengi kwa kuwa wanaamini katika hatua mpya uweza kuamini hadhi zao na mambo mengine uweza kubadilika.

Ni kama mwanamke anavyotamani kupakata mtoto na wakati akitambua kipindi cha kujifungua ni kuweka maisha yake rehani lakini inabidi akubaliane nayo kwasababu ndio hatua ambayo jamii inataka aelekee huko kwa maana inaaminika kuwa baada ya ndoa ni furaha kuongezeka.

Ni kama mkulima akiwa na shauku ya kuona mavuno na kuyafurahia na ikiwa anatambua kuwa kuamua kulima ni kuweka fedha yake rehani kwa kuwa inaweza kukata na kumwacha katika ndoto isiyokucha na kubaki kujuta bora asingeamua kupanda au kuingia kwenye kilimo.

Bila shaka hatua mpya ni jambo zuri linaloleta furaha kwa mtu mmoja na familia pamoja na ukoo kwa ujumla, kwakuwa wana amini kwamba kama mmoja akitoka katika kufanikiwa basi ukoo utakuwa na sehemu ya kupumulia au unafuu.

Niseme tu kwenda hatua mpya sio jambo la mchezo au la kawaida kuna hali unaweza pitia  hata usijue mara ya mwisho kulala usingizi ilikuwa lini maana inawezekana kipindi hicho kikasababisha hali ya kukosa utulivu wa akili na mwili kwa kiasi kikubwa.

Unapotaka kwenda hatua mpya ukaangalia mchakato wake usipokuwa na dhamira ya dhati unaweza kukuta umeghairisha kuingia katika hatua mpya na sio kwamba upendi hatua mpya bali ni ugumu wa mchakato unaonekana katika akili yako.

“ petro alipoamua kutembea juu ya maji alipoangalia mawimbi shaka ikaingia ndani yake na hatimaye akaanza kuzama……….”

Mathayo 14:26 Wanafunzi walipomwona akienda juu ya bahari, wakafadhaika, wakisema, Ni kivuli; wakapiga yowe kwa hofu.

 27 Mara Yesu alinena, akawaambia, Jipeni moyo ni mimi; msiogope.

 28 Petro akamjibu, akasema, Bwana, ikiwa ni wewe, niamuru nije kwako juu ya maji.

 29 Akasema, Njoo. Petro akashuka chomboni, akaenda kwa miguu juu ya maji, ili kumwendea Yesu.

 30 Lakini alipouona upepo, akaogopa; akaanza kuzama, akapiga yowe, akisema, Bwana, niokoe.

 31 Mara Yesu akanyosha mkono wake, akamshika, akamwambia, Ewe mwenye imani haba, mbona uliona shaka?

Hatua mpya unaweza kuifananisha na ng’ambo iliyojaa mema kwa ajili yako lakini kuna mto inabidi uogelee ili ufike ng’ambo na ndani kuna mamba wa kali lakini kwa namna yoyote inabdi upite katikati ya hao wanyama ili uyafikie yale mema yako yaliyo ng’ambo.

Akili ya mkulima uwa naipenda kwasbabu uwa inaangalia matokeo kabla ya kuangalia mchakato utakao sababisha matokeo hali hiyo inafanya kuukabili mchakato wote katika hali zote ugumu na kujinyima ili mradi apate matokeo anayo yataka au yale aliyokuwa anayawaza na ikiwezekana hata zaidi ya yale aliyokuwa anayawaza.

Hauwezi kupata mavuno kama ujafuata mchakato mzima wa kukupelekea hayo mavuno, kama haupendi mchakato wake basi hauko tayari kupata mavuno, ni sawa sawa mwanafunzi anataka kupenda daraja la juu huku hayuko tayari kulipa gharama ya kusoma kwa bidii.

Ni shauku ya Mungu tuingie katika hatua mpya sio hatua ileile kwa kuwa unapodumu katika hatua ya awali kwa muda mwingi kuna baadhi ya mambo hutaweza kuyapata mpaka uingie katika hatua nyingine, kila hatua ina utukufu wake hivyo ili upate utukufu mwingine basi hakikisha unaingia katika hatua nyingine.

Isaiah 1:19 Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi;

Hatua mpya unaingia kwa kuikubali na kuitii sauti ya Mungu, pindi utakapo amua kuishi sawasawa na sauti yake pasipo kuangalia nini kinaendelea nawe au gharama utajikuta upo katika hatua nyingine wenye utukufu wake.

“ kama ukuweza kunizuiliwa mwanao……………..basi sasa kukubariki nitakubariki”

Mwanzo 22:16 akasema, Nimeapa kwa nafsi yangu asema Bwana, kwa kuwa umetenda neno hili, wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee,

 17 katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao;

 

INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………………………………………………..0764 018535