Ijumaa, 13 Februari 2026

USIOGOPE


 

Moja ya neno nzuri ambalo linawapa hatua mpya au kuendelea zaidi pindi watu wanapolisikia ni neno USIOGOPE.

Japo kuna wakati unaweza kukosa nguvu katika mambo yanayokukabili, unaweza kuona  yanakuzidi nguvu lakini hata hapo unaambiwa USIOGOPE inakuwa sawasawa na gari lililokosa/lililopoteza mwelekeo kwa sababu ya kukosa brake likielekea kwenye maporomoko lakini hata katika hali hiyo unaambiwa usiogope, japo kuna wakati unaweza kupoteza maana halisi ya hili neno maana  unaweza kuona kama  unakikabili kifo chako.

Duniani kuna mambo mengi yanayotisha na kuogopwa sana sio yale yanayoendelea katika maisha yako binafsi tu bali hata yale yanayoendelea katika jamii yako ama duniani.

Unapaswa kujua neno pekee linaloweza kumwingiza Mungu katika utendaji ni kutoogopa ambalo linakua zao kuamini.

Hauwezi kushindwa kuogopa katika mazingira yanayotaka uyaogope isipokuwa umejua kwanini usiogope au umepata uhakika na kuwa salama katika hayo mazingira.

Moja ya mateso mengi kwa watu ni zao la kuogopa, na kuogopa ni rafiki wa hofu.

Wako watu wameshindwa kubeba ujauzito kwasababu ya hofu, kwa kuhofia je! Atakuwa salama kweli au hata hatarisha maisha yake.

Wako wameshindwa kufanya mambo makubwa kwa sababu ya hofu, nafasi zinaweza kuja na kukupa hatua nyingine au kukupa ushuhuda lakini unaweza kushindwa kufanya kwa sababu unahofia je ikishindwa kufanikiwa je! Nitakuwa mgeni wa nani? Mathalani kuna nafasi zinatokea unatakiwa uwekeze hela zako nawe unazo lakini unahisi je! Zisizoporudi nitakuwa katika nafasi ipi?

Kuthubutu kunaweza kukufanya ufanye mambo makubwa au uwe katika namna nyingine lakini hofu imekuwa kikwazo cha wewe kufika hapo.

Yakupasa kujua kwamba hakuna mabadiliko yasiyokuwa na gharama hivyo unavyoogopa kufanya mabadiliko kwa kuhofia gharama utakazoingia bila shaka kuvuka ng’ambo inaweza kuwa ni vigumu.

Wako watu wameogopa kuingia huko kutokana na yale yanayoendelea katika jamii manyanyaso, mateso na magonjwa yanayozaliwa kutokana na hali hizo.

Tambua usipobadilika maisha yako hayawezi kubadilika ufahamu wako utakuwekea mipaka.

Mambo mengi yanategemea ni utulivu wa akili yako na namna unavyomtanguliza Mungu pasipo kuweka matamanio yako mbele.

Japo kuwa nyuki wanang’ata na wanaweza kuua lakini watu hawaachi kulima asali.

 

INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA

 

Imeandaliwa na:

 

Cothey Nelson……………………………………………………………………………….0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni