Ili uone kitu zaidi unachokiona au uone kile ambacho wengine hawakioni unahitaji mwanga katika macho yako.
huweze kuona kile kisichokuwa na picha/muonekano mzuri kuwa na muonekano mzuri wa kuvutia ( kisichoonekana ili kionekane ).
Vile ulivyo inategemea kiasi cha jicho lako lilivyofunguliwa kuona hivyo kadili unavyofunguliwa ndivyo unavyoona.
Ukifumbuliwa kidogo utaona kidogo na ukifumbuliwa sana utaona sana.
Kuna hatma kubwa zimefichwa katika kuona.
Ni kama watu wawili wanapoutazama mti wanapata tafsiri tofauti: mmoja anapouangalia anaweza kuona kuni nzuri zitakazo mfaa katika upishi wake na mwingine anapoangalia akaona mbao zitakazo msaidia kupelekea kutengeneza vitu vya thamani.
Tatizo sio mazingira yalivyo bali ni hile tafsiri inayozaliwa katika macho yako usipofumbuliwa huwezi sababisha matokeo, mathalani unaweza okota dhahabu na ukaitupa mtoni nawe ukawa na amani kabisa maana uliona kama jiwe lisiloweza kufanya jambo lolote na mwingine akaliokota katika mto na kuona ni dhahabu hatimaye likafanyika kuwa ukombozi wa maisha yake yote.
Macho yako yasipofumbuliwa nawe ukaona hata ushauriwe vipi kufanya jambo fulani utaona ni mateso tu na utaona hakuna la maana unalolifanya hapo.
Yakupasa kujua ukombozi wako uko katika kuona sio katika macho bali katika akili iliyojaa mwanga wa kesho uliobora.
Macho yako yakifumbuliwa katika kufanya jambo fulani hautahitaji msimamizi wala msukumo mwingine wowote.
Kuchoka wala kukata tamaa hakutakuwa ndani yako utaona unaweza kesho hata kama leo haukufanikiwa.
Hali hii uwa unamuona Mungu kwa ukubwa sana kuliko jambo lolote unaloliona kama ni kikwazo kwako.
Haupaswi kuona mfano ili uweze kujitia moyo bali tayari nguvu ya kuendelea iko ndani yako na inaongezeka kadili ya magumu yanavyoongezeka nayo inaongezeka.
Utofauti wa watu wengi katika matokeo ni namna wanavyotafsiri mambo kwa jicho.
Huyu yuko hapa na yule yuko pale inategemea namna unavyoona na neema ya Mungu iliyo juu yake.
Haupaswi kuyaona mambo kikawaida yakupasa kuyaona mambo kwa jicho la pili ili uweze kujipata.
Mathalani, sio kila uchafu unausukuma mbali bali kuna aina ya uchafu unaweza pata wazo kupitia hapo unaweza pata mpenyo wako,kuna watu wamebadilisha maisha yao kwa kufanya taka kuwa kitu cha kufaa na hata kupata soko.
Ni wazi macho yako yasipofumbuliwa unawezapata nafasi na usiitumie Ipasavyo.
Hali hii ikikosekana kwako unaweza kujikuta una walaumu watu wengi na kuona wao ndio sababu ya wewe kushindwa kutoka hapo.
Macho yako yanapofumbuliwa unaweza kuiona fursa na kuiendea.
Barthomayo “ alipoona yesu anapita hakuacha fursa hii ipotee bali alitumia vizuri ndipo hatua nyingine ikazaliwa katika maisha yake” Ni lazima uone ili upate.
INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA.
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson…………………………………………………………………………0764 018535
