UPENDO;
Si neno geni masikioni mwa watu wengi hili neno PENDO,kwakua
kama ujawai sema basi umeshaambiwa na kama ujaambiwa basi umesha sikia sehemu fulani
au toka kwa mtu mmoja akizungumza na mwezake hivyo si neno geni kwako.
Ukweli upendo ni asili ya Mungu mwenyewe kwakua
ndani yake ndiko kuna asili ya neno ya UPENDO, mbali na yeye hakuna kupenda kwa
maana ya Mungu bali kuna kupenda kwa maana yetu. Hali hii uweza kupotea mara
kikatokea kitu kingine kikachukua nafasi basi hali ya kupenda upotea.
Tatizo kubwa mtu anapo kwambia ninakupenda huwa
amalizii kuwa huo upendo ni wa muda gani huwa haiko wazi unakuta yale yote
ambayo mmeahidiana yana katishwa na kukuta anakwambia umefikia mwisho au unaona
vitendo vinavyoashiria mwisho.
Kwa namna hiyo watu wameshaliondoa thamani ya neno NAKUPENDA kiasi kwamba mtu anaweza kukwambia
asubuhi nakupenda halafu jioni akasema nimeghairi, inaweza ikakusumbua baada ya
kutendwa sana unaweza kuona sasa ni kawaida hivyo halitashtua sana moyo wako.
Kwa namna hii watu wamekaa katika mausiano kwa
tahadhari kubwa sana wakijiweka sawa kwa lolote kutokea. Hivyo uhuru katika
kuhusiano umepungua sana kwani imekuwa ikileta majanga katika moyo wake.
Japo kunachangamato za neno hili UPENDO kukosa
thamani yake katika dunia ya sasa lakini bado jambo hili lina hitajika sana
kwakua katika hili mambo mengi mazuri ufanyika.
Maisha au uhusiano wowote wenye hali ya upendo ndani
yake ni mahala ambapo unapenda kuwepo siku zote. Kwa hakika UPENDO ulitakiwa
kuwa msingi wa jumuhia,familia na mahusiano yoyote ili kuleta radha ya mausiano
hayo.
Lakini upendo wa siku hizi umekuwa ni wakujisikia
tu,wakuwaza tu pasipo kujua upendo ni zaidi ya kujisikia au kufikiri.
Ki ukweli hali hii imepotea kiasi kwamba watu
wamekosa kuona mahala penye upendo wa kweli lakini hali hii imebakia katika
maneno,nyimbo na masimulizi tu yasiyo kuwa na msingi wowote.
Imefika kipindi cha kuwa watu wanatafuta namna ya
kuishi pasipo kupendwa au kupenda kwa namna alivyotenda katika mausiano
mbalimbali.
Neno hili limekuwa likiambatanishwa na mambo
yasiofaa ambayo yamekuwa kikwazo katika jamii inayotuzunguka kwa kiasi kikubwa
usemi huu uwa na nguvu PENDA UNAPO PENDEKA.
Hili neno lina nguvu sana kama likibebwa kwa namna
yake katika ukamilifu wake ili kuleta dhima iliyokusudiwa.
UPENDO ni namna moyo wako unavyozungumza na sio wewe unavyosema au watu
wanavyozungumza.
Mitazamo
tofauti ya dunia ya sasa kuhusu UPENDO;
I.hakuna maana ya kupenda pasipo kupendwa.
Huwa hatuangalii jambo kwa namna stahiki bali ni
vile tunavyoona sisi tunavyo amini sisi na kila tendo tuna itafsiri kwa
lugha/maana yetu.
Ni kweli unapo pendwa hapo nawe upenda sana lakini
haujui kwa namna gani mtu yule anakupenda kwa nini anakupenda.
Msingi wetu mkubwa umekuwa kwa vile anvyo nipenda na
mimi nita muonyesha hayo mapenzi kuwa kikisha anafurahia uwepo wangu.
Na mahali ambapo unaona ishara ya kutopendwa hapo
utafuta namna gani kuwa mbali na mazingira hayo kwani unahisi lolote laweza
kukutokea.
Tutambue sio kila mahali unapo pendwa basi unaweza
kufanikiwa vile unavyofikiri na sio kila unapochukiwa unaweza kutofanikiwa,
wakati wowote na majira yoyote mambo yanaweza badilika yale mazuri kwako yakawa
mabaya na yale mabaya yakawa mazuri.
Hali hii ni tatizo katika jamii kubwa tuliyo nayo
kwani mausiano pindi yanaposhuka watu utafuta namna kuachana zaidi na sio namna
ya kutafuta namna ya kurejesha.
II.nini alichonacho ambacho kitanifaidisha mimi!
Kwa hiyo upendo wangu unajengwa kile kitu alicho
nacho kwa uwepo wako na mtu huyo utegemea sana uwepo wa kitu hicho hicho kitu
hicho kikipotea basi upoteza.
Ni kweli unapo uhusiana na mtu lazima kutakuwa na
mbadilishano wa vitu lakini tambua kuwa mbadilishano wa vitu sio msingi wa
maisha yenu bali ni vitu vinavyoboresha urafiki/mausiano yenu.
Hali hii inapokuweka unakuwa ni mausiano ya
tahadhari sana inakuwa kama mtu anayesubiria mzigo maana fulani akisha upata
halafu haende zake/haendelee na maisha yake.
Watu wenye uhusiano huu wanakuwa na hali ya
utegemezi mmoja kuliko mwingine hali hii uhishia mahala ambapo si salama sana.
Kama hauna kitu ambacho kitamfaidia mwingine mtu wa
namna hiyo hawezi kukaa nawe kwani kile anachokitaka ajakipata.
Huu sio msingi wa kuwa na mausiano na mtu lakini
katika dunia ya sasa imekuwa ndicho chanzo cha kufamiana, ulikuwa haumuheshimu
wala hautambui maana halikuwa si kitu kwako lakini baada ya kuwa na kitu sasa
thamani yake ikawa. Uhusiano ulioshikamana na maslahi haya uwa kunatokea na
uharibufu mkubwa.
Ni vizuri kutamani mambo toka kwa mwenzako ukjifunza
na yeye akakuelewa kuliko kwenda kwake ukawa mnafiki halafu mwisho ukawa mbaya.
III.nimepungukiwa
na nini mpaka ni mpende!
Unaweza kushangaa kwanini mtu anaweza kusema maneno
kama haya hii inatokana na mambo matatu
makubwa, KUTENDWA,KIBURI NA KUKOSA UELEWA.
Mambo haya yote yanaweza kumfanya mtu kuwa katika
nafasi ya kusema maneno hayo. Hii yote inaonyesha jinsi tulivyopoteza misingi
ya UPENDO.
Kwa hakika hali ilivyo uadui utakuwa ndio urafiki maana kama mnaishi kwa tahadhari basi
hamna tofauti na maadui ambao wanamendeana.
Jamii ya watu wa namna hii ni hatari sana kwakua
upolomoka katika maangamizi makubwa kwani wanajiamini kana kwamba duniani
unaweza kuishi pasipo kuwa na UPENDO.
Ni kweli kila mtu anayo nafasi ya kujitengenezea
maisha yake kwa namna yake lakini jamii bado unahitaji hakuna njia ya kukwepa
kama usipo wahitaji leo basi utawahitaji baadae.
Hivyo mtu anapokuwa katika hali hii si vyema
kumuhukumu kwakua haujui kitu gani kimeleta hali aliyokuwa nayo. Ila inakuwa
shida pale tu kwa mtu husika asipotaka kukubali kuwa wazi.
Mtu uweza sema nisipokuwa nae kwani nitakufa na
maneno mengi ya kejeli yanayofanana na hayo usikusumbue kama kuna giza jua kuna mwanga muda si mrefu kitajulikana.
Prepared
by ;
Katiti, James - 0713 398 042 or james.adili19@gmail.com
“Kila la kheri,rafiki……….”