NGUVU YA UCHAGUZI,
Kila uchaguzi uliotokana na maamuzi uwa kuna misingi
inayojijenga ndani ya mtu yanayopelekea kufanya UCHAGUZI. Hiki ni kipindi
ambacho hakina mfano na wala hakina tabia ya kujirudiarudia kwakua matokeo yake
katika maisha ya mtu yanaweza kujenga hatima mpya ya mtu ambayo hakuwazwa wala
kufikiriwa yaani inatoa mwelekeo mwingine tofauti na kule uliko kusudia. Ila
uzuri wa uchaguzi huu uwa hakuna msukumo wa mtu unaoweza kukupelekea bali ni
MSUKUMO TOKA NDANI YA MTU HUSIKA.
Hakuna kitu kibaya duniani kama nguvu ya uchaguzi,
kwani uchaguzi ni mpasuko wa kitu kimoja na mwingiliano wa kitu kingine ambacho
knajikita kwenye misuli,nyama na hata damu na kuishi ndani ya mtu kwa utayari
wa mtu husika. Jambo hili linaleta giza katika mambo mengine na kupelekea nuru
kwa ule uchaguzi alioufanya na aijarishi nyinyi mnaona giza yeye ataona nuru
iliyo kali zaidi ya jua kali lisilo na mfano na hata ikitokea mnaona mabonde
miporomoko na mito mikubwa yaani mambo yasio na matumaini kwa macho bado yeye
ataona barabara iliyonyooka isiyo na kikwazo chochote na ikitokea watu wengi
wanaona kucheleweshwa kwa safari yao lakini yeye ataona ni karibu saaaana kama
sebuleni na chumba cha kulala.
Ukitaka kuona mtu haogopi hata kufa ni pale tu
utakapokwenda kinyume na uchaguzi wake hali hii uweza kuwa tayari kukabiliana
na chochote pasipo kuangalia nguvu alizonazo kulingana na kile kitu ambacho
anakwenda kupambana nacho uwezo aliokuwa kutokana na uchaguzi alioufanya uweza
kuona anaweza kumuua simba kwa sekunde chache.
Ni kweli watu wanafanya uchaguzi kila mara na
kubadilisha lakini hapa na zungumzia uchaguzi katika hatua ya juu saaana
mathalani maamuzi yaliyo katika kilele cha mbingu maamuzi yanafanya mtu
kubadili muonekano wake kabisa na wakati mwingine unaweza ukaona afadhari
kichaa kwakua anaweza akapona lakini si kama mtu aliyefanya maamuzi thabiti ya
kuchagua mtu huyu inakuwa bora ukutane na simba anaweza akaacha alama watu
wakajua kutoka na damu au masalio ya nyama au mifupa basi wanaweza sema kuwa
hapa kuna mtu kauwawa kuliko kusimama kinyume na mtu katika uchaguzi wake
kwakua anaweza akakumaliza asibakishe ata ishara yeyote wala watu wasijue kama
kuna tukio limefanyika.
Kusimamia jambo kwa mtu ndio ishara ya nguvu ya
uchaguzi wa mtu juu ya jambo fulani kwaiyo uchaguzi wa mtu uimara wake
unategemea kiwango cha uchaguzi. Sio kila jambo unatakiwa ufanye uchaguzi wa
kiwango cha juu kama hiki lakini ni vyema utambue kuwa uimara wa uchaguzi uweza
kukupelekea uthabiti wa mafanikio unayo yatamani na wengi wa watu uwa
tunashindwa kutimiza ndoto zetu kwakua hatuja fanya maamuzi ya kula kiapo cha
kutorudi nyuma na akili zetu pamoja na damu zetu zikakubaliana na hilo kuwa
ndio maisha yako sasa ulio ya chagua pasipo kushurutishwa na mtu yeyote. Nguvu
ya uchaguzi sio jambo la kuamua tu bali ni nguvu uliyonayo katika kuhakikisha
uchaguzi ulioufanya unakuwa wa kufanikiwa katika maana iliyo bora na iliyo ya
mwendelezo wa kudumu.
Hili ni jambo mtu anaye amua kufanya uchaguzi wa
namna hii uwa anakuwa ni mtu aliyeamua baada kukaa chini na kuhesabu gharama
zake za uchaguzi huo na kisha akachukua huo uchaguzi akiwa ana akili timamu
akijua anafanya nini na yuko tayari kupambana na chochote ambacho akitakuwa
rafiki wa kile anachokiamini au alicho kichagua muhusika. Watu wenye aina hii
ndio rahisi kuabiliana na bahari halafu bahari ikapisha njia.
Kwa maana
nyingine nguvu ya uchaguzi ndio umekuweka leo mahali ulipo kwakua uchaguzi wako
pamoja na juhudi zako zikakupelekea kuwa katika mazingira mengine ambayo ndipo
ulipo leo.
Hili swala aliitaji sana maombi bali ubinafsi wa
uliochukua uchaguzi wa kujitoa sadaka ili tu aweze kufanikisha uchaguzi wake
kama vile alivyopanga kwa uhakika zaidi pasipo kuona haina ya shaka. Uchaguzi
huu haujui asilimia ya kushindwa bali unatambua uko uwezo wa kushinda tu hivyo
faili la kushindwa uwa linakuwa limetupwa nje na wala hakuna ushawishi wowote
wa ishara ya kushindwa ni kama mnyama mkali aliyejeruhiwa saaana na baada
kutoka hapo na kuta kulipiza kisasi huwa haoni kama kunauwezekano kushindwa
kutimiza hazma yake kwakua alichokiamua anajua kuna kushinda tu wala hakuna
jambo lingine.
Kwa watu wapembeni mnaye muona mtu huyo mnaweza
kuona mtu huyu kwa uchaguzi alio ufanya ana hatarisha sana maisha yake hivyo
mngeona ni bora ahuache lakini yeye uwa haoni vile mnavyoona bali anaona vile
sawa na uchaguzi wa nafsi yake ilivyo mtuma. Na uchaguzi huu uwa haungalii
mzazi rafiki au mpenzi bali umetawaliwa na utashi wa mtu husika akiwa katika
hali ya kujiamini na akijua kile anachofanya ndicho sahihi na ndicho alichpaswa
kufanywa hivyo apaswi kuingiliwa na mtu katika yale anayoamua kuyafanya kwakua
anaamini ni sahihi sana kuliko ushauri mwingine wowote.
Haya ni maamuzi au uchaguzi uliotoka katika misuli
ya ya moyo wa mtu na huku damu ikiwa ni shahidi kwa hilo kwa maana nyingine
akiipa nguvu hali ya mwanadamu katika maamuzi aliyoyachukua kwakua kwa anaamini
ni ka ajili ya pumziko la nafsi ambayo ikipata pumziko inakuwa ni burudiko
kwao. Haya maamuzi hayafanani na mtu katika kuwa tayari katika kujitoa mwanga
bali ni haya maamuzi yanafanywa hata watu wengine hawawezijua badala yake uona
matokeo na hivyo ujua kuwa kumbe mtu huyu alikuwa anakuelekea huku hivyo upatwa
na mshangao tu lakufanya alijulikani tena kwakua limeshatendeka hivyo wako watu
watakao lia na wengine watahuzunika na wengine kutowatambua kuwa wana lia au
wanahuzunika na wengine watakuwa wa kicheka kulingana na aina ya tukio na
matokeo yake.
Katika hali hii ya uchaguzi mtu huwa haogopi kifo
bali ujali ule uchaguzi aliouchukua kwa mwendo wake utegemea tu uchaguzi wake
utakavyompeleka na sio jambo lingine mtu uweza kukabili kifo pasipo mashaka
yeyote kwakua anatambua kuwa kifo sio kizuizi kwake kutokana na uchaguzi alioamua.
Pindi utakapokutana nae mtu kama huyu ambaye ameshafanya uchaguzi wake kwa
ukamilifu basi kuwa mwangalifu sana pindi unazungumza nae kwakua ni mtu ambaye
anachokihitaji kwa wakati huo.
Mtu wa namna hii usitegemee hata siku moja hata kaa
ajutie maamuzi yake/uchaguzi wake kwa kua katika kufanya jambo hilo alikuwa la
siku moja bali mizizi ndani ya moyo wake umekuwa ukikua siku baada ya siku tena
katika utaratibu wake mpaka akachukua maamuzi hayo tayari pamesha kuwa na
majadiliano ya kutosha na tayari pamekuwa na mwingiliano ulio thabiti kwa kile
alicho kiamua yaani nyama, damu, mifupa na hata misuli hivyo tendo linalo toka
hapo linakuwa na kishindo kisicho kuwa cha kawaida ni zaidi ya anguko la mlima
everist.
Imeandaliwa
na;
Nelson, Cothey – 0764 018 535 or cotheyn@yahoo.com
TUMIA NGUVU HII KATIKA
KUJIIMARISHA NA SIO KUJIMALIZA,