NGUVU YA AGANO
Ni neno la kawaida ambalo limekuwa likitumika katika
jamii yetu kama neno ambalo linaashiria mtu kumaanisha kwa kile alichokusudia
kukisema kuwa ndio kweli na ndicho anacho maanisha na kamwe hawezi kukiuka yale
makubaliana ambayo wamekubaliana.
Ninapozungumzia neno hili AGANO lina maana zaidi
watu wanavyofikiri au watu wanavyolitumia lakini ukweli ni kwamba neno hili ni
zaidi ya kukubaliana maana hili neno lina beba kifungo kisicho onekana lakini
kina athari kubwa sana endapo tu usipozingatia hilo agano ambalo watu
wanaanzisha halafu hawalizingatii.
Ukweli katika duniani asilimia kubwa watu wanapitia
katika hali ngumu ya maisha na magonjwa tofauti
ambayo majina ya hayo magonjwa hayajagundulika
bado lakini inawathiri lakini sababu kubwa ni kutoheshima agano.
Agano linauwezo kukutengeneza kuwa katika hali njema
au mbaya kutokana vile utavyolienda hilo agano na uwezi kumlaumu mtu bali
itabidi ulilaumu hilo agano.
Tunapozungumzia huwa atuzungumzii swala ambalo lina
nafasi ndogo katika maisha ya mwanadamu bali ni jambo lenye nguvu ambalo laweza
fanya jambo ambalo uwezi kuamini kama yale yaliyo kupata ni matokeo ya agano.
Katika
jamii kuna nadharia mbalimbali zinazohusu Agano:
i.Agano la ndugu
hili agano ambalo likowazi haupangiwi bali inakuwa
kitu kilichofanyika ambacho akiitaji usaidizi wowote bali hali hiyo imewekwa na Mungu mwenyewe kuwa wewe
na ndugu namna mnavyotakiwa kuenenda.
Watu ambao hawalipa nafasi na kuliheshima hili agano
lazima matokeo yake ya taambana katika maisha yake, mathalani mtu anauwezo wa
kuwasaidia ndugu zake ataki kuwasaidia au hawatambui tena kutokana na hali
aliyokuanayo sasa. Wengine wanawakataa wazazi wao,ndugu zao hali hii itapelekea
maumivu makali katika mioyo ya ndugu zake na hivyo malipo hayo lazima ayavume
kwa mtu ambaye amekiuka agano ambalo lililokuwepo tangu kuzaliwa kwako katika
jamii hiyonayo.
Hili agano lipokwenye damu moja kwa moja halina
mjadala umeshaunganishwa ni wewe kulitendea kazi ipasavyo lasivyo litakuweka
katika mazingira usiyoyapenda.
ii.Agano la urafiki
haya ni maagano ambayo ni rahisi kuingia na pia ni
vigumu kuyasimamia,haya maagano yanakuwa nalengo la kufanya uimara wa mausiano
ya weze kudumu sikiu zote.
Na hiki tokea mwingine haonyeshi ushirikiano wa
uhakika katika uthabiti wa kutoa hayo maneno ya kuingia agano mwingine
anajisikia vibaya.
Ukweli maagano sio kitu kibaya kuingia lakini ni
jambo ambalo linawafunga katika mausiano yenu hata kama nyinyi binafsi mnaona
ni jambo kupita tu.
Japo katika jamii yetu hali hii kumaanisha katika
kuingia agano imepungua sana kiasi kwamba watu hawaoni umuhimu wa swala hili
lakini ukweli kwamba ndilo swala ambalo linawatesa wengi hata pasipo kujua
kwanini nateseka.
Maagano mnapoingia kuna vitu vinashirikilia huo
muungamaniko wenu mathalani vitu vinavyoonekana na visivyoonekana kama vile
miungu na hata hali mbalimbali ambazo zinashuhudia katika makubaliano yenu.
Watu wengi wanapovunja maagano yao kasha maisha yao
yakaendelea kuwa mazuri basi ufikiria hakuna athari yoyote lakini kumbuka
athari ziko nyingi ikiwemo hali ngumu ya uchumi,kufungwa kizazi,kutotulia na
mtu moja(mke/mme),magonjwa katika mwili wako yasio koma na hata kuibiwa
kuharibikiwa na mimba ya mara kwa mara. Wengine wanasema mikosi hivyo utaka
kwenda kwa waganga ili kuondoa hiyo mikosi na njia nyingine nyingi lakini
katika yote bado yanabakia palepale.
iii.Agano katika uchumba(ndoa)
hili agano la tofauti sana kutokana na radha yake
hili ni agano ambalo haushurutishwi ila unakwenda na kufanya mwenyewe tena bila
kuona ugumu wowote.
Katika madhara makubwa yanapotokea pindi maagano
yanapovunjika aina hii ya maagano yanakuwa na matokeo mabaya sana ambalo linawezafanyika
jambo ambalo alijawaitokea alijawaifikiriwa.
Katika hali hii mtu wa namna yoyote anaweza akafanya
jambo ambalo jamii ikabaki kushangaa na watu wengine wasione maana ya kuingia
mausiano katika aina hii ya maagano.
Katika hali ya kiuchumba mtu uingia katika maagano
ambayo hayasemeki kwenye aina nyingine kwakua kuna muungamaniko wa maisha
ilikutokeza pamoja na kuna namna ya kushirikiana ambavyo ni ngumu kushiriki na
mtu yeyote kwakua uchumba ni mahali ambapo uumbaji wa Mungu unafanyika.
Hatua hii maagano yanapovunjika ni aina hii pekee ya
mausiano ambayo mtu uweza kuona bora afe kuliko kutokua tena maagano na mtu
husika.
AGANO LA MUNGU
JUU YA MWANADAMU…
Mwanzo
9:8-17,15:18
Hili ni agano amblo limekuleta duniani ambalo lina
nguvu kubwa katika kuyafanikisha maagano yote.
Kama ilivyo kumweshimu Mungu ni kuheshimu maagano
yake juu yako na hakuna namna ya kumuheshimu Mungu nyingine mbali na kuheshimu
maagano yake, hauwezi kusema na muheshimu mtu wakati ambao uyazingatii maagano
ambayo mmekubaliana.
Japo imekuwa ni jambo ambalo mtu analiona kuwa
kawaida kulifanya pasipo kujali nini hasa ya kumweshimu na kumthamini mtu.
Wengi wanavunja maagano sio kwasababu hawataki
kuendelea na mtu au na jambo Fulani bali ni ahali yakushindwa kuyazingatia yale
makubaliano. Mathalani unapokuwa kazini pale ubora wako na uimara wako
unatakiwa uonekane pale katika kuzingatia maagano mliyokubaliana na pindi kama
ujakubali kuyatekeleza hayo makubaliano basi unafukuzwa kazi.
Hatuwezi kuishi na Mungu vizuri kama hatutekelezi
yale maagano yetu tuliyonayo na yeye kwakua yeye anayaheshimu sana maagano yake
kwa kiwango cha juu sana,
Namna
Mungu anvyoheshimu maagano aliyoyaweka;
Mwanzo
8:20-22, ..Mungu akasema moyoni mwake,sitailaani nchi tena
baada ya hayo kila kilicho hai kama nilivyofanya……muda nchi idumupo,majira ya
kupanda na mavuno,wakati wa hari,wakati wa kaskazini na wakati wa kusi,mchana
na usiku, havitakoma.
Haya ni maneno ambayo Mungu mwenyewe ameyayasema na
anayasimamia mpaka leo kama alivyosema lile ambalo alilifanya kipindi cha nuhu
baada kuachilia gharika kubwa duniani hivyo Mungu ameto nadhiri yake kuwa
hatafanya tena jambo hilo hata kama wanadamu wamemkosa kwa namna yoyote.
Dunia ilipoangamizwa makosa yaliyofanywa na wanadamu
yalikuwa si makubwa kuliko yanayofanywa na wanadamu wa sasa kwakua dunia
tuliyonayo sasa mambo yanatisha yanapoteza thamani ya utu wao,Mungu ananafasi
ndani ya mwanadamu imekuwa chafu haivutii lakini bado Mungu anaiheshimu agano
lake aliloliweka na nuhu.
Mwanzo
9:13
Kwa hakika yeye ni mwaminifu kwa lile agano na
analisimamia kwa hali yote aijalishi uchafu umezidi au la! Lakini bado
ameishikilia agano aliloliweka.
Na Mungu ameweka upinde mawinguni ili izidi
kumkumbusha yeye kwa hile agano lake, japo tunajua Mungu anatabia ya kusahau
kama wanadamu wengine lakini ameweka upinde mawinguni ili asije akaghairisha
akaiangamiza tena dunia katika maangamizi makubwa yasio elezeka.
Namna Mungu anavyolisimamia lile agano lake kwa kila
namna kuhakikisha inakuwa vile alivyokusudia ni muhimu binadamu yeyote anaweka
agano na Mungu lazima ajue kuwa huyu ni Mungu ambae anasimamia agano lake kwa
ukamilifu sana hivyo lazima roho hiyo iwe ndani yake ili kwenda pamoja kwa moyo
uliotayari kwa gharama yeyote.
Mungu ili akutendee anangalia namna unavyoweza
kulizingatia agano lake kwako hivyo usipo li heshimu agano hilo Mungu basi
usitegemee kabisa Mungu akakuangalia wewe binafsi kama uzingatii agano lake
nawe.
Na kila agano linaenda na Baraka zake hivyo
usipolitimiza agano basi sahau juu ya Baraka hizo kukuandama.
Katika dunia ya sasa watu wengi wanasema wanamuogopa
Mungu lakini hawana haja na agano lake Mungu juu ya maisha yao hii haiwezekani
kwakua hali hii ni sawa na kusema na muheshimu sana na kumpenda mtu lakini yale
mliyoweka agano nae halitilii maanani.
Na pindi agano lisipozingatiwa basi uhusiano
unavunjika pasipo shaka ni kama vile katika ndoa ikiwa wanandoa wasipozingatia
agano lao basi ndoa hiyo kinachofuata ni kuvunjika kama tu wasipokubali
kubadilika.
Ni bora umsahau mtu kuliko kusahau agano mliloweka
itakuwa mbaya na hutaamini yale ambayo yanayoweza kutokea katika maisha yako.
Ukweli mtu anaweza usione kuwa ni jambo la kawaida jua kitakachokusumbua sio
mtu bali ni hile agano(NGUVU YA AGANO).
Kuna
agano la Mungu juu ya isaka kwa ibrahimu
Mwanzo
17:15-17(1-23)
Hali hii ibrahimu na kwa sara lilikuwa ni jambo gumu
sana kukubalika kwa namna ya akili ya kibinadamu wakati mwingine unaweza
ukahisi hili jambo kufanyika litakuwa ni ngumu sana na kuona kweli Mungu
anaweza kutimiza ahadi hii.
Bado Mungu alionesha kuwa uwaminifu katika
kutekeleza lile lililokuwa gumu kwa namna ya mwili lakini yeye alifanya
mwenyewe kwa ukamilifu sana pasipo na kitu kinachoweza kumzuia.
Mwanzo
22:1-15
Mungu anapenda mtu ambae anamsikiliza kwa umakini
sana na kulifanya kwa ukamilifu sana pasipo hofu bali kwa kutii na kupenda
pamoja na moyo wa kuamini uwezo wake.
Natunzaje
Agano la Mungu;
Hapa ndipo pahali ambapo natamani sana kusema ndio
msingi wa somo hili na ukielewa hapa unakuwa katika nafasi nzuri sana.
Mwanzo
39:1-12(6,9)
Hapa tutamwangalia kijana mmoja anaitwa YUSUFU kama
kijana ambaye alifanikiwa kulitunza agano lake na Mungu kwa ukamilifu wake na
ustawi usio wakawaida.
i.Kubali
kupata aibu ili Mungu apate heshima
mambo yaliyo katika dunia hii yanataka wewe upate
heshima na Mungu aibike inategemea wewe uko upande upi kuchukua heshima kwanza
ili upate aibu au kuchukua aibu ili upate heshima.
Unahitaji kujua kwamba yusufu angeweza kufanya jambo
lolote katika kupata nafasi nzuri ambayo dunia ingempa lakini alitambua jambo
moja……..Nifanyeje ubaya huu mkubwa nimkose Mungu!!!!!!!
Japo alikuwa njia ya panda Yule mwanamke kutokana na
wadhifa alikuwa nao angeweza kufanya jambo lolote hata kumuua, ili yeye
asihabike. Pamoja na hayo yusufu alikubali yote yampate ila asimkose Mungu
kwakua alitambua hatma ilipo.
Kwa hiyo alikubali hata kufa ila atunze agano mbaele
za Mungu.
Ufunuo
2:10b
………..uwe mwaminifu hata kufa,name nitakupa taji ya
uzima.
Prepared by ;
Nelson, Cothey – 0764 018
535 or cotheyn@yahoo.com
Katiti, James - 0713 398 042
or james.adili19@gmail.com
TUNZA AGANO ILI
AGANO
LIKUTUNZE.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni