Ijumaa, 21 Machi 2014

AMANI ADIMU



AMANI ISIYO NA MIPAKA,

Amani yangu na wapa sio kama ulimwengu utoavyo…….yesu alisema!

AMANI katika maisha ya mtu yeyote ,kwa mwanadamu hiki ni zaidi ya kuwa na chochote mathalani watoto, mme au mke na hata kazi na amini hakuna madini yoyote hapa duniani yanayoweza chukua thamani ya amani ndani moyo wa mtu, ni kweli kuna wakati unaweza usione maana wa jambo lolote au mtu yeyote lakini si kama AMANI.Na unaweza kuwa na chochote lakini kama hauna AMANI utoshelevu wa hicho kitu akita kuwa na maana sana zaidi kwakua kinacholeta radha katika yote ni AMANI, wakati mwingine tunaweza fananisha AMANI kama chumvi katika chakula chochote unaweza ukaweka kila kitu lakini kama chumvi haipo jua hapo hakuna radha utakayoipata kwa ukamilifu.

Amani kama angekuwa mtu basi watu wote wangependa kuwa rafiki yao wa dhati kwani watu wote wanahitaji amani hata kama mchawi,jambazi,chizi na wengine wengi wanahitaji amani na wanapenda maisha yao yote yatawaliwe na amani.kutokana na mtazamo huu watu wengi wamekuwa wa kikiri kuwa haiwezekani kama mwanadamu kutawaliwa na amani wakati wote ungalipo hapa duniani kwani wanaamini hapa duniani sio mahali salama sana kwani kuna kukasilishwa,kuumizwa na hata kudhurumiwa hivyo watu wamekubaliana  kuwa na amani iliyo na mipaka.

Watu wengi tumekuwa tukiishi na amani kanakwamba ni haki yake kutokea halafu ikatoweka tumekubaliana na hali hii hivyo tumeona mtu kuishi pasipo amani ni jambo la kawaida, na mtu kuwa mahali fulani au kufanya jambo fulani pasipo amani basi panakuwa na mgawanyiko ulio katika mwili na akili kwa maana hii akili na mwili vinakosa ushirikiano kamilifu basi kwa hali hii mtu uweza kujigawa pasipo ridhaa yao binafsi.

Ningependa utambue kuwa amani ni haki yako ya kudumu na wala sio ya muda fulani tu au yakutokea kwa majira fulani mathalani kipindi ambacho unazo pesa za kukidhi mahitaji yako kwa wakati wako huo na sio hilo tu bali pia au wakati ambao unahisi kupendwa na kila mmoja kwa kipindi fulani.Ni kweli tunakuwa na mfano wa amani lakini sio amani yenyewe kwa kuwa kila amani huwa kuna shina au misingi yake ambayo haiwezi kubomolewa na chochote kile. Imkuwa si ajabu mtu kusema asubui nilikuwa na amani yangu ghafla imetoweka sijui kwanini? Au mtu akisema maneno haya…. mimi nilikuwa na amani zangu lakini ulipokuja tu amani yote imetoweka, amani sio kitu cha kufikirika tu ambacho kinaishia kwenye akili ni zaidi ya hapo kwani kina nguvu na uwezo mkubwa wa kumtawala mtu.

Wana amani nyingi waipendayo sheria ya bwana wala hakuna la kuwa kwaza….”

Hivyo ukifikia hatua ya kukwazika basi hiyo amani ya kweli haipo ndani yako kwa ukamilifu wake.
Wako watu wakijishughulisha na mambo fulani au kiburudisho fulani ili mradi aweze kusikia amani ndani ya moyo wake…..lakini muda mwingi imekuwa sivyo kama alivyotegemea!!!!!!

Amani za watu wengi zimekuwa ni za vipindi fulani kiasi kwamba watu uweza kusema kwamba je! Kwenye msiba kunauwezekano kuwa na amani hasa kwa mtu unaye mpenda au aliyekaribu kweli unaweza kuendelea amani iendelee kutawala ya moyo wako.Ninapozungumzia amani na zungumzia zaidi ya kuwa na furaha au utulivu huwa amani haijaishia hapo bali imepitiliza zaidi ndani sana na hakuna kipimo chake.

AMANI= MATUMAINI  + ULINZI

Hii ndio tafsiri yangu ya neno Amani katika hili neno lazima pawepo na muambatano wa matumaini na ulinzi kwa kile unachokitumaini kuwa utakipa au kifikia.Mambo haya matatu uwa yanaenda pamoja na ndio yanakamilishana yote kwa ubora sana.

Amani ubebwa na matumaini yaliyo ndani yako yanayolindwa na katika kufanikisha jambo, hivyo shina la matumaini linategemea liko wapi au limebebwa na nini? Na je uhakika wa kufikia katika yale unayoyaendea.Tunapozunguzia ulinzi uwatunatoa maana ambayo inalandana na Imani-kitu kinachokupa uhakika.Katika yote utayoyapitia amani haiwezi kuondoka kwa sababu imebebwa na vitu hivyo viwili vilivyo na ukamilisho kwa ufasaha.

Ukiwa katika misingi hii lazima itakuwa inachipuka kwa wakati wote katika hali mbalimbali iliyo ngumu au nzito unakuwa na AMANI ISIYO NA MIPAKA ambayo inachipuka ndani yako na kukupa busara katika maamuzi siku baada ya siku,kama ukiwa na amani ya kipindi tu ya ushawishi wa mwili hauwezifika mbali kwakua ni ngumu kushamiri na kuwa na uimara wa nyakati zote.

Lazima uwe na amani ambayo hakuna kinachoweza kuondoa iwe mchumba, rafiki, ndugu au wazazi bali inakuwa imeshirikiwa na nguvu ya mbingu ndani yako ambayo yeye aliyoiweka ndio mwenye uwezo wa kuiondoa na hakuna wa kuiondoa zaidi yake ukiona amani inaondolewa tu jua haijajikita katika misingi ya matumaini pamoja na ulinzi(imani).

Amani isipo kuwepo ni wazi mahala hapo uwezi ukadumu na vilevile amani isipokuwepo mahali hapo hauwezi ukapafurahia na pakaleta burudiko ndani ya moyo wako.

Usiwe na amani isiyoimarika bali yenye mabadiliko siku baada ya siku,amani inatabia ya kuongezeka pale ambapo shida inapokuwa kubwa huwa aipungui kama kawaida ya mambo ya dunia yalivyokuwa.hivyo amani yako inapotoweka pale ambapo mambo yanapokukabili basi ujue hiyo amani ujaipokea kwa kristo bali inafanana na hile ambayo kristo anaiachilia kwa watu wake.

Uwa amani hii ambayo Mungu anapoiachilia haitaji huichochee bali ipo inatawala nakutembea katika mwili mzima una kuwa mtu wa kicheko wa furaha na mawazo yaliyotulia yenye mwelekeo katika mwelekeo uliosahihi katika mwelekeo ulio na ulinzi wa ki Mungu katika kuyafanikisha yale yote yaliyo matumaini yako.
Na haiwezekani ukawa na amani ya namna hii kwa kuombewa au kutabiriwa bali katika kuliruhusu neno la Mungu katika mwili wako mzima kwa uhakika na kukufanya vile linavyotaka katika kiwango chake na sio katika fikra zako bali katika akili ya hilo neno kwa utoshelevu wake. “Mjue sana Mungu ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujiaa…    Ayubu 22:21

Hauwezi kufanikiwa katika huduma yako na mambo mengine ya kuinua ufalme wa Mungu kama tu una amani yenye mipaka(amani yenye kawaida ya dunia) kwakua yenye sio kamilifu kumudu kila hali itayojitokeza lakini amani ambayo haina mipaka hakuna jambo lililowa tokea au litakalotokea likamtingisha mtu wa namna hii.

Amani hii uwa uenda pamoja na ujasiri kwakua amani hii ndani yake hakuna hofu ndani bali inakuwa ni amani yenye uhakika kwa kila kile kilichokusudiwa kwa kua hii ni amani iliyo kuu kuliko amani yoyote(shwari kuu).Vilevile amani hiihaendani na utashi wa mwili ndani yake hakuna asila,chuki,kisasi wala dharau. Hii ni amani iliyombeba Mungu kwa utoshelevu wake hivyo matunda yaliyo ndani ya Mungu ndiyo yaliyo ndani ya amani hii katika ubora wake, kwa maana nyingine amani hii inaongozwa na Roho kwa utoshelevu wake uliosahihi zaidi hatua za Roho mtakatifu ndio hatua zake.

Vilevile amani inaenda pamoja sana na pendo la kristo uwa vinashikama pamoja sana kwakua amani ufanyakazi mahali penye pendo la Mungu kwa utoshelevu kwakua amani hii imebeba dhima ya kuujenga ufalme wake,kwakua amani yake inakuwa kwa ajili yake na sio jambo lingine.

Amani hii pia inatiwa nguvu na macho yako ya rohoni baada ya kutiwa nguvu ili kuona kama vile Mungu anavyoona na tumani lizaliwe hapo na wala sio mahala pengine kwa kua macho ya Mungu yamebeba ulinzi wa Mungu na utoshelevu wake.Na utulivu na maamuzi yenye misingi iliyo bora yanatokana sana na AMANI ISIYO NA MIPAKA!

Amani hii haina uhusiano na akili ya kibinadamu kwakua haijashikamanishwa na mwili bali na roho iliyojaa Mungu. ukiona unaihusisha na akili jua hiyo sio amani iliyombeba kristo bali itakuwa imebeba kitu kingine!



Imeandaliwa na ;
                      
                 Nelson, Cothey – 0764 018 535 or cotheyn@yahoo.com
                  
                Katiti, James       - 0713 398 042 orjames.adili19@gmail.com                                                 


KUWA NAYO AWE NAWE!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni