UHURU WA MWANADAMU
Mwanadamu katika sifa nyingi alizonazo mojawapo ni
UHURU. Japo kila rika uhuru uwa unaanza kuwa unamipaka mwisho unakuwa hauna
mipaka, kufanya vile uonavyo vyema na sio vile jamii inavyotazamia bali ni kile
unachojisikia katika matakwa yako.
Na kila mtu kila anauheshimu uhuru wake ndomana yuko
tayari kuulinda uhuru wake kwa gharama yeyote ili mradi tu anaendelea kuwa
uhuru, na wakati mwingine ukitaka kujua huyu ni nani anafanya nini basi mwingilie
katika uhuru wake basi hapo utajua namna mtu anavyodhihirisha yeye ni nani,
hama mtu mwenye asila kali, mstaharabu au mnafiki na mengine mengi. Uhuru wa
mtu tunaweza sema ni almasi ya mtu kwakua ni kitu ambacho mtu anajivunia kuwa
ni mali ya mtu binafsi. Kila mtu mtu upenda kuheshimiwa kwa uhuru wake hivyo
upelekea mtu au umlazimu mtu huyo kuheshimu watu wengine.
Na katika kutumia uhuru wa mtu binafsi basi uweza
kupeleka mahala pa zuri saaana au pabaya saaana lakini yote yamebebwa na uhuru
mtu binafsi na ni kawaida kuona kama umemuheshimu mtu ni kuheshimu uhuru wake
na sio jambo linguine kwakua kila jambo ufanywa katika mistari iliyo bebwa na
msingi wa uhuru wa mtu binafsi.hakuna kitu kinachoweza kumfurahisha mtu kama
kile ambacho umekifanya kwa uhuru wako halafu ukafanikiwa na vilevile hakuna
kitu kama hiki ambacho mtu uweza kujisikitikia sana kama jambo alilolifanya kwa
uhuru wake halafu likaleta uharibifu ndani ya maisha yake.
Uhuru
wa mwanadamu umegawanyika katika sehemu kuu tatu;
i.uhuru wa kujimiliki binafsi
ii.uhuru wa kumilikiwa na nje ya ubinafsi
iii.uhuru wa kumilikiwa na Mungu
I.UHURU
WA KUJIMILIKI BINAFSI
Hiii ni hatua ambayo mtu uwa nayo/ufikia mara baada
kutoka kwenye himaya ya wazazi huwa na uhuru wa nafsi katika kufanya yale ya ujazayo
moyo wake pasipo kuuhusisha kitu kingine kutokea kikaleta shida katika maamuzi
yake. Hali hii uwa inkuwa sauti ya muhusika kuwa na nguvu zaidi ya jambo
jingine na hii ni hatua nzuri kwa kuwa unawe kuvunja mipaka ya zaidi
unavyofahamu kwakua uhuru ulio ndani yako unakusukuma kufanya jambo fulani
kutokana na uhuru ulionao basi uwa unakupa wepesi kufanya jambo hilo katika
moyo wa kujaribu katika kufanya vyema.
Ni uhuru wa kujisikiliza sana wewe binafsi kuliko
kingine hivyo wakati mwingine uweza kufanya jambo ambalo hautajali wengine
watachukulia katika namna gani katika hali chanya au hasi.hii ni hatua
inayoweza leta msukuma nakupelekea mtu katika kufanikisha jambo ambalo watu
wengine hawakuweza kulifanikisha.
Japo hatua hii inamazuri mengi lakini katika upande
mwingine mbele za Mungu hii hatua ni kikwazo kikubwa sana katika kufanisha
mpango wa Mungu hapa duniani kwa vile anavyoona upingamiza unaotokana na
umiliki wako binafsi( kujimiliki binafsi). Ni hali ambayo Mungu inampa ugumu
katika utendaji wake kwani lolote atakalo kukwambia lazima kwanza lipate kibali
kwenye uhuru binafsi halafu litendeke hivyo kama tu alitapatakibali katika
uhuru ubinafsi halitaweza tendeka, na jambo lolote linapopita katika uhuru wa
nafsi basi nafsi uhesabu kugharimika kwake katika jambo hilo hivyo ikiona kuna
kugharimika sana kuliko kufaidika basi uweza kulizuia hilo jambo lisiweze
kutendeka kabisa na hivyo kuwa kikwazo cha mpango wa Mungu hapa duniani. Uhuru
huu wakati mwingine upelekea hali ya kujiamini sana kuliko kawaida na kupelekea
kuchukua maamuzi ambayo yataleta picha nzuri katika nafsi yake na sio katika
upande mwingine wowote.
Pia hali uweza kukupelekea kushindwa kukaa na watu
wengine hata mbele za Mungu ikawa kikwazo kikubwa sana. Katika hii hatua
unaweza kujiweka kipaumbele kiasi kwamba hata utawajali wachungaji,wazazi hata
ndugu zake hali hii inatokea sana katika jamii katika kutafuta kitu ambacho
kitanufaisha nafsi yako kuliko chochote.
II.UHURU
WA KUMILIKIWA NA NJE YA UBINAFSI
Na hali hii inawezajengwa na ushawishi wa atu au wa
vitu au utashi wa mtu binafsi pia hii ni hali inayofuata mara baada ya umiliki
wa nafsi hali ya kuwa sauti yako kuwa na nguvu lakini hatua hii ni hali ya kitu
kingine kuwa na nguvu zaidi ya nafsi yako hivyo sauti ya nafsi ya nafsi yako
haina nguvu sana kama vitu vingine hali hii uchelewesha katika kuchukua maamuzi
au kuchukua maamuzi pasipo ridhaa ya nafsi kamili. Na hali ndio iko katika
maisha ya watu wengi kwani wengi wanauliza marafiki,shemeji na hata wazazi
katika kuchukua maamuzi Fulani na mgawanyiko wake
a)kitu;
gari, mti au mlima
b)mwenzi;
mke au mume
c)wazazi
mtu anaweza kuruhusu vitu vingine viweze kuwa na
sauti katika maisha ya mtu husika kwa kukosa kwa yale uliyoyakusudia. mtu
anakuwa ametawaliwa zaidi ya maamuzi yake binafsi kwakua ndani ya nafsi yake
hakuna utoshelevu ulio sahihi katika kuchukua maamuzi. Na hali hii ya
kutoridhika katika kuitosheleza nafsi yake, uweza mfanya mtu sio jambo jambo
rahisi katika kuchukua maamuzi kwakua upima gharama zake kwa mapana sana na
hata yasiyowezekana kutokea anaweza kutoa uwezekano mkubwa wakutokea ndani yake kuna hali isiyo shwari. Na hali hii
upelekea mtu hali ya kutokua rahisi katika kuridhika na hali moja na hivyo mtu
huyu uweza kukosa msimamo wa namna ya kufanya kwa usahihi wa jambo husika, hali
hii sio inamtesa mtu husika bali hata jambo lenyewe na pia kwa lile ambalo
linasubiliwa na hata kwa wanao lisubiria jambo hilo kwakua inawezekana
kuchelewa kwao ndio upelekea maumivu kuzidi kushamiri katika maisha ya watu
hao. Japo watu wengi wanaamini kuwa katika kuchanganya mawazo mengi kunaleta
majibu yaliyo bora mimi na kataa kwani kwanza lazima uweze na hali ya binafsi
ya kile unachokiamini ndicho uweze kushirikiana na wengine ili uweze kupata
kitu kitachoboresha na kuimarisha katika kile ulichokiamini.
Hali hii pia ni kikwazo mbele za Mungu kwani kijambo
ambalo Mungu atakwambia lazima uweze kulipeleka katika mizani ili jibu sahihi
hii ni hatari sana kwani kuna mambo mengine ulivyoeleweshwa wewe ni tofauti na
wengine wanavyoelewa. Sauli katika kufuata ushauri wa watu wengine zaidi ya
agizo alilopewa na Mungu vilevile adamu katika kutekeleza sauti ya mke wake
kuliko lile agizo alilopewa na Mungu. kwa
maana hii ni jambo hili linahitaji misuli katika maamuzi yasioweza kuingiliwa
lakini yawe sahihi. Haya yote ni sawa kwa kauli ya ubinadamu lakini yamekuwa
kikwazo kikubwa katika utendaji wa Mungu ndani ya maisha ya mwanadamu
kwakushauliana hata yasiyo takiwa kushauriwa, ni muhimu uweze kujishauri kabla
ya kushauriwa.
III.UHURU
WA KUMILIKIWA NA MUNGU
Hili Mungu akumiliki anahitaji uhuru wa mtu binfsi
au utayari wa mmilikiwa na hichi ndicho kilio cha Mungu kwa wanadamu na ndio
hatua hii ambayo Mungu anatamani tuwe hapo ili yale makusudi yake yaweze
kujidhihirisha kwa ukamilifu ndani ya maisha yetu, kwa hakika dunia vile
tulivyo ni matokeo ya kupoteza uhuru wa Mungu ndani ya maisha yao watu wamekuwa
na nguvu katika maisha yao na hata ubinafsi wao umekuwa na kiasi cha juu kuliko
jambo lolote.
Katika maisha na Mungu kama hiki kisipokuwa na nguvu
inayostahili jua kwamba hakuna jambo unalolifanya likawa na la maana sana kwa
Mungu hiki kama ukipuuzia jambo hakuna ustahivu unaotakiwa . kwa maelezo ya haya Mungu anatafuta mtu
atakaye mwabudu katika roho na kweli na sio waenda kanisani au wafuata mkumbo ni
kweli unapenda uhuru binafsi lakini hata Mungu anahitaji atumie uhuru wako
ndani yako wewe kama hekalu la Mungu mluhusu yeye afanye kwa raha zake ndani
yako ili azidi kuona fahari juu yako,
Ni vizuri kwenda kwenye msingi wake na sio ya yeye
ndio kusudi kuu analolitaka ndani yenu ndomana anasema mimi ni Mungu mwenye wivu usiwe na mungu mwingine ila mimi hichi
ndicho Mungu anataka kwa mwanadamu ili uweze kuwa baba yake nawe uwe wake, na
pasipo hilo sahau tu Mungu kudhihirika kwa ukamilifu. Kwakua anajua pindi
atapokuwa akizifanya kazi zake ndani yako hauta inuka kiburi wala kujiona wewe
ni mtu saaaana kuliko wengine lakini tunakuwa KRISTO.
Imeandaliwa na ;
Nelson, Cothey – 0764 018
535 or cotheyn@yahoo.com
Katiti, James - 0713 398 042 or james.adili19@gmail.com
KILA LA KHERI…………..RAFIKI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni