UWEZA
ULIONDANI YA MUNGU;
Katika ulimwengu
tulionao sasa kila kitu kinauwezo binafsi ambao utofautiana kulingana na utendaji wake na kusudi lake,japo
viko vitu ambavyo vinaonekana kuwa vina uwezo mkubwa kuliko vingine kulingana
na udhihirisho wake pamoja na muonekano wake.
Uwezo wa mtu au kitu
ndicho kinachoamua uishi wapi/vipi au ujasiri wa mtu na uhuru wa mtu kwakua uhuru
kwa mwenyenguvu utegemea udhaifu juu ya mwingine.pindi kama wewe sio jasiri
basi ujasiri utategemea kwa kitu kingine kitakachokuzunguka ambacho kinakuwa
kama kinga katika maisha yako.
Katika dunia ya leo
kila mtu utafuta mahali au kitu cha kujistiri au cha kumwifadhi wako
wanajifunza kareti katika kujiami,wako wanaotumia pesa na wako wanatumia nguvu
za giza katika kujiami na kujiweka katika maisha ambayo wanafikiri kuwa
yanaweza kuwaweka huru lakini wewe binafsi unaweza kujiuliza umejiweka katika
kinga ipi?
Uhuru ulionao utegemea
nguvu uliyonayo pamoja na ufahamu ulionao kwakua hivi ni vitu kwa uhakika
vinategemea sana jinsi unavyojitambua na ndivyo utakavyofanya.
Unapozungumzia UWEZA
uwa unazungumzia MUNGU mwenyewe maana hakuna badala yake wala mwenye kuingia
ulingoni na kupambana nae lakini swali linakuja mbona hata wanaomwamini
Mungu
hawawezi kuutumia huu uweza ukaleta mpenyo katika maisha ya mtu husika badala
tumekuwa tukiona watu wengi wasio na Mungu wamekuwa wakifanikisha mambo
yao kuliko wale wanao mwamini Mungu.
Hivyo swali linakuja
kwanini watu wanaomwamini Mungu wa kweli hawawezi kudhihirisha kuwa Mungu
walionao ni mkuu sana kuliko kiumbe chochote duniani kwani vyote ni kazi ya
mikono yake na wala hakuna kilichojifanya chenyewe!
Japo yako mambo mengi
ambayo yanaweka kikwazo katika kudhihirisha uwezo wa Mungu;
•Kushindwa
kumfanya Mungu kuwa ni wa binafsi!
Lazima umweke Mungu ni
zaidi ya kusanyiko au kikundi chochote haijarishi hicho kikundi unakiamini au
haukiamini lakini jaribu kukitoa katika ushirika wako na Mungu japo hicho
kikundi kinaweza kuwa cha msaada sana kwako lakini kubwa lazima utofautishe
kuwa hilo kundi tu lakini maisha yako na Mungu yanategemeana sana.
Hili lolote linalotokea
lisiwe shida katika maisha yako kwakua wako watu wanaumizwa na ndugu zao katika
kristo yesu, wachungaji hivyo wanahatarisha maisha yao na Mungu na kuwa
hatarini pasipo kujua vyote vilifanyika tu ila Mungu ndio kila kitu( mtendaji
na mtoshelevu) analo likusudia ndilo linalofanyika haijarishi mawingu au mvua.
Lazima utambua kundi
linapochoka na sio Mungu amechoka au linapocheka na Mungu pia naye anacheka
hivi ni vitu viwili vilivyotofauti sana.
Tumemfanya Mungu kama
tunavyomuona katika macho ya nyama hivyo ikatupelekea kuenenda kwa jinsi ya
Mwili……maana hapo ndicho chanzo cha chuki,mateso,wivu na hata kupendelea.
Watu wengi wengi ambao
hawajaokoka uwa wanakuwa makini sana kusiliza kile ambacho wataambiwa na
utayari utendaji wa kile walichoambiwa pasipo na hata kujijengea mifano mengine
ambayo itakuwa ni mzigo katika maisha ya mtu binafsi.
Tumemweka Mungu katika
makundi na ushirikiano tukamleta Mungu kuwa ni sawa na furaha ya muda katika
kundi au kusanyiko linalomuhusu Mungu hivyo lolote linaloendelea linakuwa
linaathiri na ushirika wako na Mungu likiwa zuri basi litajenga na endapo
likiwa baya basi litaharibu ushirika wako na ndio chanzo kimoja wapo cha watu
kufungua makanisa, kuama makanisa na hata masengenyo,chuki na kisilani uanzia
hapo.
Imeandaliwa
na;
Cothey
Nelson…………………………………….0764 018535