UTULIVU WA MAJI HAINA MAANA MAJI HAYO NI
SALAMA;
Maji yaliyo salama ni
kivutio kikubwa katika kuyatumia katika shughuli za kawaida na hata kukidhi
haja ya mwili yaani kuyanywa, kwani macho yako yatatoa msukumo wa kufaa katika
mwili wako na ujumla wa afya yako itakuwa ni njema hivyo yanafanyika kuwa
msaada kwa watu wengi wakitumia maji yaliyotulia yanakuwa ni maji bora.
Ni kawaida ya watu kupenda
sana mahali penye utulivu ili kumlahisishia hazma yake au lengo lake ambalo
analikusudia, ni kweli mahali penye utulivu panavutia wengi sana lakini swali
linakuja je!usalama umeambatana mahali hapo maana mahali hapo jambo la msingi
ni usalama kuliko hali iliopo au kinachoonekana.
Hii ni moja sababu ya
vijana wengi katika harakati zao katika kumpata mwenzi wake,endapo utakapo
wauliza wote watakwambia na mtaka MTU
ambaye ni mtulivu, swala linakuja utamjuaje kuwa huyu ni mtulivu?
Na wako watu walisema
mahali hapa ni salama sana lakini baada ya muda tu akaona mahali hapa ni pa
chungu na ni pabaya sana kuliko jua la mchana jangwani.pamoja na hali hiyo kuwa
kukuta watu wengi yale waliyo yaona ni tofauti na uhalisia ulivyo…….kama ni
mnyama mkali basi ameendelea kula watu pasipo watu kujielewa au kutambua.
Ni kweli maji
yaliyotulia yanakadiliwa kuwa yana wanyama wa majini kama mamba lakini unapoona
maji lazima utambue ni aina gani ya maji kwani mamba hapatikani kila matuo ya
maji bali upatikana katika maji yasiyo na chumvi, na kila aina ya maji
kunaviumbe tofauti wanapatikana hapo mathalani maji ya chumvi utamkuta papa, na
kila aina maji maandalizi yako yatategemea aina gani ya mnyama anapatikana hapo
na pindi utakaposhindwa kubaini aina kiumbe kinachoishi mahali hapo basi
maandalizi yako hayataleta matokeo unayoyategemea.
Ni wazi katika mtego
huu anayeweza kupona ni kipofu tu na sio mtu mwingine kwakua katika hali ya
utulivu kila mtu upenda kuwepo hapo hata bila ya kujua huo utulivu ni wa kudumu
au wa muda mfupi tu kwakua kuna kuwa na ushawishi wa macho na kusikia lakini
kwa Yule kipofu kuamua kitu gani kifanyike inahitajika sana hali ya
kujiridhisha ya hali ya juu sana na sio kukupuka katika ushawishi usio kuwa na
kina katika ya ustawi wa maamuzi yake ulio na mwanga wa uhakika.
Imeandaliwa
na;
Cothey
Nelson………………………………………..0764018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni