Jumatano, 14 Januari 2015

VITA YA MAISHA

NAPENDA VITA;



Nikiwa najua wazi kuwa katika vita kuna kushinda na kushindwa lakini pamoja na hayo yote ni seme wazi napenda sana vita, kwakua ni vita pekee inaweza kunionyesha na kunifuza yale yote ambayo kwa namna ya kawaida ni singeweza kuyaelewa na hata kuyamudu lakini kupitia vita inanipa kujielewa sana, kupata ufahamu mwingine katika yale ambayo yananizunguka.

Najua kwa uhalisia kabisa kuwa vita ni mbaya kwani inaweza kuleta maafa makubwa sana katika jamii yetu….bila shaka utakuwa njia ya panda lakini sisemi vita ya kutumia vifaa vya moto kama vile bunduki mabomu la asha bali na zungumzia vita katika mapambano ya kimaisha ya kila siku na vilevile na zungumzia namna ya kukabili yale yanayotaka kukukabili pasipo kupepesa macho kwani ukipepesa macho ni wazi utatoa mwanya kwa Yule anaye kukabili kuona amekushinda.

Lakini niseme wazi kuwa vita hii ya maisha katika kupambana kutokana na mapungufu tuliyonayo wengine elimu wanatakusoma lakini uwezeshwaji unakuwa haupo, wengine wanataka kujenga kutokana na kero za nyumba za kupanga lakini uchumi bado ni changamoto nyingine, mwingine kampata mke au mme lakini vile alivyotazamia kumbe sivyo na hata vijana kukicha wako katika mausiano lakini bado kusalitiwa na kutendewa ndivyo sivyo katika ulimwengu wa kimapenzi nao umeshika kasi uwa watu hawaoni wapi kuna uwafadhali,

Katika vita hii wako watu wanaamua kujinyonga, kuachana na habari za kimausiano na wengine kuamua kuishi maisha wasiyoyataka laity wangekuwa na uwezo wangeomba wajengewe dunia ya kwao ili waishi huko pasipo buguza yoyote hile na wengi wao wanaishi kwakua amua kuwa na kinyongo katika moyo wao na wale walio tumiwa katika kufanyika kuwa jaka la moyo ndani yao.

Hautaji kuambiwa na mtu bali nikile kinachoendelea ndani yako kinachokuweka njia mbili za mkato kati ya kushoto au kulia yote yanabebwa na wewe na hivyo kusababisha kuwa ni vita kali pamoaja na mashindano yasiyoisha.

Pamoja na changamoto zote hizo katika vita unayokukabili bali tambua kuikabili ndio njia pekee katika kukufanikisha kwenda katika ustawi mwingine lakini tujiulize jambo moja je!inakabili vita katika maarifa yapi? Katika nguvu ipi? Na katika uimara upi? Mambo yote haya ni ya muhimu sana kwani katika hayo ndio uweza kukutambulisha pamoja na kukupa uhakika wa kushinda ua kushindwa.

Ni vizuri kutambua vita ipo kwakusudi lake hivyo wewe kulitambua kusudi la vita ni moja ya ufahamu wako kuweka katika njia ya ushindi pasipo udhihirisho katika ulimwengu wa macho yako, lazima utambue vita imebeba kusudi la Mungu na sio uonevu kama unaweza ukachukulia kirahisi tu.
Bali vyote vimebebwa na kusudi la Mungu haijalishi katika macho yako yamebeba makusudi gani lakini asili yake imebeba utukufu na ustawi wako usio elezeka wala usio beba tafsiri ilipata kibali kwa mwanadamu.

Na muhimu uwe mtu katika kujiandaa na vita wakati wote katika ufahamu wako na wala sio katika mazingira ya hofu bali katika mazingira yalibeba matumaini na uhakika pasipo kukata tama.

Ni ukweli ulio wazi sio wewe unayepigana bali ni Mungu mwenyewe anapigana wewe unawakilisha tu lakini vita haipigani kwa ajili ya kutaka kukumaliza bali ni kutakuua kile kilicho ndani yako ambacho kwa hicho kina kuwa ni tatizo katika utawala wao, ni seme wazi hautaji kuiogopa vita au kuikimbia kwakua kazi yako katika vita ni kufuata maelekezo tu na wala sio jambo jingine………….kwakua yeye MUNGU naujua mwisho wako kabla ya mwanzo kuanza!

Imeandaliwa na;

                        Cothey Nelson…………………………………..0764018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni