MWAKA
MPYA;
Kila mtu ujisikia vizuri anapotoka hatua moja kwenda
hatua nyingine inaweza kuwa kiuchumi, kielimu na mengine mengi, na wako watu
ufurahia sana wanapoona siku nyingine katika mwaka mwingine.........kwakua
ukianza kuhesabu tangu mwaka ulipoanza mpaka unaisha ua unaishia unaweza kusema kuwa Mungu amenisaidia japo wako watu
hawaoni tofauti ya mwaka mmoja na mwingine.
Lakini pamoja na hayo niseme kuwa tunapozungumzia
mwaka mpya ziko maana mbalimbali kutoka kwa mtu mmoja na mwingine lakini mwisho
tunamalizia kusema ni majira mengine na kipindi kingine chenye mambo ambayo
hatuwezi kuyajua mambo yataendelea vilevile au yatabadilika.
Ni kawaida kwa watu ifikapo mwisho wa mwaka ziko
kabila zingine uenda kujumuika kwa pamoja katika kupeana habari na mambo yanaendeleaje!
Na watu wengine uenda katika nyumba za ibada au mahali popote ambapo kuna
panakusanyiko la watu wanaomwabudu au watuwasiomwabudu Mungu mathalani disko na
sehemu zingine za starehe.
Hivyo niseme hatuiti mwaka mpya kwa kubadilika namba
tu na namna akili yetu inavyoelewa kuwa ni kipindi kingine tu bali tunaona mwaka mpya kama fursa amabayo Mungu ametupa
kwa kusudi lake na itakuwa ya maana sana kama tukitambua na kuanza
utekelezaji.lakini watu usherekea tu na kuishia kushukuru pasipo kujua hilo ni
deni ambalo Mungu ametupa ili tuliweze kulilipa ni kama katika biblia Mungu
kuwapa talanta moja kupewa mbili na mwingine kupewa tano,hakuna maana ya kuwa
na hizo talanta halafu ukamrudishia kana kwamba ulimtuuzia tu.
Unahitaji kuona mwaka mwingine kwa macho mengine hii
ni zaidi ya kula na kunywa na kufurahi pamoja na kushukuru kwa Mungu kwa kuwa
amekupa jambo la wewe kulifanya tambua Mungu ni mfanyabiashara anayeitaji faida
sio kutimiza utaratibu tu. Bali hali hii ni zaidi ya kusema asante kwa Mungu.....kwakua
Mungu alijua kuwa utafika na sio kufika tu bali pia kuna kzi ambayo utaifanya
itayofanya Mungu mwaka mwingine kwa furaha kwakua umeutendea haki wakati ambao
Mungu amekupa.
Ukweli dunia ya sasa Mungu anajuta kwanini watu
wengi amewapa wakati mwingine lakini vile wanavyotumia haoni faida ya kuwapa
huko wengine wanafanya vitendo vya uhalifu, ubadhilifu na vitendo ambavyo jamii
inazidi kupoteza nguvu kazi inakuwa siku ya maasi na sio siku ya tathmini yako
na Mungu katika wakati wote ulioenda na Mungu.
Tumia mwaka vizuri kiasi kwamba yeye aliyekupa mwaka
azidi kuona fahari ya wewe kukupa miaka yote kwa furaha akuone ni mtumwa mwema
na sio awe anakupa kwa sababu apendi usiangukie mikono isiyo salama. Usifurahie
mwaka mpya kwakua wengine wanafurahi tu bali furahia kwakua unaenda kuzidi
kuikabili ile kazi njema ambayo Mungu amekuamini nayo au ambayo atakuamini
nayo, ona ni mwaka wa kujenga ufalme wa Mungu ili watu waone uzuri wa Mungu na
umuhimu wa Mungu katika maisha yao.
Imeandaliwa na;
Cothey
Nelson...........................................................0764
018535
TATIZO
SIO MWAKA BALI NI WEWE KUTAMBUA NYAKATI.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni