Jumanne, 30 Desemba 2014

WIMBO WANGU!



USIYESHINDWA;




Ningependa hili NENO likawe wimbo wako, unaotawala akili yako na iliyopata nafasi katika moyo wako na udhihirisho mkuu katika maisha yako. Ni kweli tunamshukuru Mungu kutokana na namna tulivyoishi mwaka 2014 haijarishi ulikuwa upande upi kwako kama ulikuwa mwepesi au mzito katika yote bado tunamuona Mungu katika yote hasa yaliyo inje ya akili au uwezo wetu binafsi.

Naamini wapo watu katika dunia tuliyonayo watu hawaoni maana ya kumshukuru Mungu katika mwaka tunaomalizia kwa masuabu waliyo yapata na pia kuna wengine wananafasi kubwa katika kumshukuru Mungu katika mazingira ya wenye ufahamu na wasio na ufahamu unaomwezesha mtu katika kufanya jambo stahiki.

Siko hapa katika kuwaambia mfanye tathmini katika maisha yako zaidi sana ningependa uanze kuona katika muono mwingine wa kumwezesha Mungu aweze kujidhihirisha vile alivyo katika maisha yako. Hili ni neon ambalo mimi binafsi nalipenda sana kwani nimejifunza kumuona Mungu sana pindi ninapoamini kuwa yeye Mungu ajawai shindwa kutokana na muonekano wake ulivyo, japo kushindwa ni kibinadamu bali Mungu vile alivyo ajawai shindwa katika kutekeleza mpango wake.
Hili ni neno kwa watu wengi uanza kulitumia lakini kamwe hawawezi kumudu kulitumia kutokana na nguvu ya macho ya mwilini yaliyomkuta petro.........(asomaye na hafahamu).

Kweli neno hili likatoe nafasi iliyokubwa katika maisha yako na kuona fahari ya Mungu katika maisha pamoja nawe! Ni lazima umuone kuwa ashindwi ili aweze kukuwezesha katika kushinda kwasababu ukweli ni yeye anashinda kupitia wewe. Na hata kama umeshindwa mara nyingi sana lakini jua kwamba yeye Mungu ajawai kushindwa kamwe kwakua yeye ni zaidi ya chochote.........na macho yake hayawezi kuzuiliwa na chochote.

Ukweli kibinadamu kuna muda unachoka lakini tambua kitu kimoja kwamba Mungu katika uumbaji wake alikutana na mambo mengi lakini kamwe hakuona kile ambacho kinaweza kuwa ni changamoto kwake au kumzuilia yeye asiendelee na mpango wake. Vile alivyokuwa akifanya yote ndivyo hivyo ataweza kufanya yote kati ya yote yanayokukabili endapo tu ukimkubali katika maisha yako                       ( kumwamini ).

Unahitaji kumwelewa Mungu kwa mapana yake kwakua yeye jinsi alivyo anajitosheleza na hana kikwazo kwake ambacho kitamfanyaasiweze kukutosheleza zaidi sawa na uwitaji wako katika haya yote jambo kubwa ni KUMJUA MUNGU!

Lazima utofautishe kumjua Mungu na kujua habari za Mungu kwani kumjua Mungu sio kujua habari za Mungu kwakua kujua habari za Mungu hazitakusaidia zaidi sana ni kumjua Mungu mwenyewe, kwani katika yeye.

Kumjua Mungu ni namna unavyopata maongozi ya KImungu katika shughuli za kila siku kwakua tunajua kileunachojua ndicho unkiweka katika utendaji inaweza kuwa katika ujuzi mbalimbali mathalani upishi wa kisasa, namna ya kutumia bidhaa kwa ufanisi au kuendesha biashara zako kwa faida.

Kumjua Mungu akuishii kwenda kanisani tu bali MPASUKO WA UFAHAM ULIOJAA MUNGU.


Imeandaliwa na;
                          Cothey Nelson................................................................0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni