UTUMWA WA FEDHA;
Unaweza kuwa adui wa dunia nzima lakini kamwe
hauwezi kuwa adui wa fedha, fedha kila mtu ni rafiki yake na laiti tungetoa
nafasi ya watu kuchagua rafiki na fedha angekuwa ni mmoja kati ya hao watakao
chaguliwa basi sina shaka watu wengi wangeenda upande wa fedha,kwa kusema hivi
sina maana yakusema kuwa fedha ni mbaya bali na zungumzia swala zima la utumwa unausiana na fedha........ni
jambo la kawaida kusikia mtu ametoloka au amekimbia kutoka sehemu moja na
kwenda sehemu nyingine kwa sababu ya fedha na sikuacha mbali uchumba na sasa
unavunjika kwa sababu ya tatizo la fedha.
Usipokua makini sana utaona jambo kama la mzaa fulani
lakini ni kifungo kikubwa ambacho kweli kinapoteza watu katika familia, watu
kuharibu miili yao kwa sababu ya utumwa wa kifedha.................!
Si pingani na fedha hata mimi naipenda sana fedha
kwani katika maisha yangu fedha ina sehemu fulani japo sio kubwa kwani mimi
naweza ishi bila fedha ila fedha haiwezi kuishi bila mimi, kwasababu fedha
imemkuta mwanadamu na yeye ndiye aliitengeneza japo sasa hiyo fedha sasa ina
mtawala binadamu kama hauamini basi tujongee pamoja katika ujumbe huu pamoja katika kusoma......!
Ni kweli kiwango cha fedha ulichonacho ndicho
kinachoamua uishi vipi yaani uvae nguo gani! Ule chakula gani! Uishi katika
nyumba gani! Na hata usome katika shule ipi au chuo kipi..............unapokuwa
na fedha haya mawazo yaliyokithiri katika fahamu za watanzania wengi yanapungua
kama sikupotea kabisa.
Na vilevile unapokuwa kuwa na pesa inakupa hali ya
kujiamini na hata kunawiri kwa wakati fulani japo watu wanasema fedha haiwezi
kununua uzima au kukionga kifo mimi na sema fedha ni kitu kizuri kwani kuna
wakati kinakupa heshima na kuwa na staa katika jamii yako na hata katika ukoo
wako.
Pamoja na uzuri wote huo unaoletwa na fedha lakini
tambua kichwa cha somo letu kinaitwa UTUMWA
WA FEDHA sasa huu utumwa uko vipi na nitatambuaje kuwa sasa hapa fedha
inanikosesha haki yangu .........kwakusema hivi sina maana watu wasitie bidii
katika kuahakikisha wanapata mkate wao wa kila siku.
Ni seme kuwa hakuna kitu kibaya kama utumwa wa fedha
kwani utapelekea umasikini ulikithiri, kifo na hata kuharibiwa mwili wako yaani
ya mwili wako kukosa thamani ile ulio zaliwa nayo.
Mungu hafurahii hali ya sisi kuwa watumwa wa fedha bali
ufurahi kuona sisi tumekuwa watumwa wa kristo japo yesu anasema.............si
waiti tena watumwa bali ninyi ni marafiki hili ni neno ambalo limebeba moyo
wangu lakini sasa hivi imekuwa ni tofauti kabisa na vile ilivyopangwa.
Biblia inasema uwezi kuwa mtumwa wa mwa bwana wawili
lazima utaacha kimoja na kuutumikia kingine hauwezi kutumikia fedha na MUNGU.
Hii ni halisi sasa hivi utumwa uko kanisani na dunia nzima kwa wale ambao
wamekumbwa na janga hili utakuta mtu yuko tayari kuua mtu ili apate fedha na ukatiri
wowote ili mradi apate fedha tu.
Wako watu wengi sana wanakatisha ndoto zao kwasababu
ya utumwa wa fedha na mbaya sana wako
watu wengi wanaiacha imani yao japo wanaenda kanisani, hili jambo si maumivu
katika familia tu bali ni maumivu hata katika moyo wa Mungu.
Usifurahie tu kwasababu unafedha bali furahia
kwasababu unamstakabadhi mzuri katika maisha yako yaliyo mjaa Mungu kwa
ukamilifu. Tambua wakati haujirudi kwa sababu ukishapita umepita na mambo yake
baliunaweza kujifurhisha tu lakini ukweli wakati utakuambia wenyewe wakati
unalia au unacheka inakutegemea wewe.
Tambua fedha haina mahali pa kukupaleka isipo kuwa
Yule aliyekujua tangu misingi ya dunia anayo hatima njema katika maisha.
KUITUMIKIA
FEDHA NI SAWA NA KUMSALIMU MWANAO SHIKAMO............!!!
unaweza kukataa lakini ndicho unachokifanya pindi
utakapoanza kuitumikia fedha ambayo imefanywa na mwanadamu, unaweza kujiona
wewe kuwa ni wakisasa kumbe ndio unapoteza dira yako ambayo kwahiyo umelindwa
na kuwepo unafikiri gharama zote Mungu amezingia kusudi uwe mtumishi wa fedha
au wake.
THAMINI
ASILI YAKO KWA WEWE KUMPENDA MUNGU KWA DHATI........!!!
Imeandaliwa na;
Cothey
Nelson..................................................................................0764
018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni