KUITAMBUA NAFASI YA MUNGU;
Unaweza ukaishi na mtu vizuri katika kushikiliana
nae kwa kila kitu lakini pindi utakaposhindwa kuitambua nafasi yake, hauwezi
kupata kwa utoshelevu wote yaliyo ndani ya mtu unaye kaa siku zote. Mtu
kutambua nafasi yako katika maisha yako hiki ni kitu cha maana sana kuliko
chochote kwani pindi mtu anapotambuliwa katika nafasi aliyonayo basi hapo
anakuwa zaidi hata ya kumpa almasi yoyote au chochote ambacho utaona cha maana
katika maisha yako.
Ninapozungumzia kuitambua nafasi ya Mungu katika
maisha yako uwa ninazungumzia swala zima unaishije naye na Mungu katika maisha
yako yeye ana nafasi gani katika ngazi hipi anasikilizwa na katika mambo yapi
asikilizwi! Kuitambua nafasi ya Mungu ili sio swala la akili tu au lakujua na
kujibu mtihani tu bali hili ni swala zima namna unavyomfanya Mungu kuwa nguvu
katika maisha yako au kiongozi,dira na njia katika maisha yako tena wakati wote
pasipo kuangalia haya ni majira gani au ni wakati gani au niko na nani!
Ukweli ninapozungumzia swala zima uwasizungumzii
swala la kutoa Dhaka kamili, kuomba au kusoma neon hata kutii taratibu za ibada
na kuaminiwa na mchungaji wako ni zaidi ya hapo kwani mahali ambapo Mungu
anahusika katika maswali ya maisha yako kwa ujumla akibebwa na moyo wako ulio
mjaa yeye kwa ukamilifu.
Kawaida hakuna mtu atafurahi kwakua anaishi na mtu
bali furaha ya mtu ipo mahali ambapo anajua nafasi inathaminika kupewa nafasi
iliyokamilifu tena katika ubora wake............biblia inasema watu wawili wataendaji kama hawajapatana.
Mungu afurahi tu kwasababu tu unamtumikia yeye kwa
kawaida ya utaratibu katika maisha yako bali yeye uangalia sana jinsi gani
unampa nafasi katika maisha yako, pindi atakapo tambua kuwa yeye umempa nafasi
katika maisha yako basi kila jambo ukalo lifanya litapata kibali katika Mungu.
Mungu ashawishiki kwa vitu ambavyo unaweza kumpa
Mungu katika kuonyesha unampenda zaidi ya kumpa nafasi ya kweli katika maisha
yako ndicho kitu cha maana sana kwake kuliko chochote...............samweli
ana mwambia sauli je! Mungu anapendezwa na sadaka ya kuteketezwa kuliko sauti
yake!!!!!!!!!!!!!
Mathayo 7:21-24..................sio
wote wasemao bwana bwana watakao ingia katika ufalme wa Mungu bali ni yeye
afanye mapenzi yangu.....wengine watakuja kwangu na kusema bwana atukutoa kwa jina
lako au kutoa unabii bali nitawajibu siwajui nyinyi kamwe ondokeni ninyi
mtendao maovu!!!!!!!!!!! Itakuwa siku ya kilio na kusaga meno.
Hakuna mtu atayependa kuona kazi anayo ifanya harafu
ikawa haina maana yeyote.............paulo anasema nisije nikaubiri wengi
halafu mimi mwenyewe ni kawa mtu wa kukataliwa.......hata Mungu afurahi wala
ategemei ila ni wewe unasababisha mazingira haya yatokee.
Hili jambo lazima ulipe kipaumbele sana kuliko jambo
kwani kama hauta litilia mkazo linaweza kuleta madhara katika maisha yako
ambayo ukuwa kuyategemea wala kuwaza kwa kuwa kila tendo lina malipo yako.
Imeandaliwa na:
Cothey
Nelson.......................................................................0764
018535
MUNGU
AFURAHISHWI KWA VITU BALI NAFASI ULIYOMPA KATIKA MAISHA YAKO!!!!!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni