UKO WAPI USALAMA;
Hichi ni kitu ambacho kila binadamu anahitaji kuwa
nacho ili kumwezesha kuishi kwa furaha, maendeleo na amani katika maisha yake,
na endapo usalama utakapo kosekana sahau kusikia maendeleo ya mtu husika au
jamii kwa ujumla. Pia ni pende kusema wazi tu kuwa kuna usalama wan chi na
usalama wa mtu binafsi na ni wazi nchi inaweza ikawa na usalama lakini watu
wake wasiwe na usalama wa maisha yao na pia watu wanaweza wakawa na usalama
lakini nchi ikawa katika hali tete..........unaweza kushangaa lakini kubwa ni
hili hakuna la maana sana hapa duniani kama kuhakikishiwa usalama.
Ni jambo la kawaida kusikia watu wenye imani za
kidini wakiliombea taifa lao amani na usalama, wakitumaini Mungu atawasaidia na
wakati nao wakijitaidi kuimarisha vyombo vyao vya usalama LAKINI pamoja na hayo
biblia yangu inasema yeye ailindae nyumba au nchi bila yeye ni kazi bure lakini
Mungu akiilinda usalama wake ni wakudumu sana.....tuachane na hili tuje usalama
ambao watu utafuta unapatikana wapi katika dunia tuliyonayo tuna waona watu
wakitafutasana usalama wa mioyo yao kuliko wa miili yao, wapo watu walio
mwamini Mungu wakitegemea kwake Mungu kuna usalama wa kudumu wamevumilia sana
baadae wakaamua kuachana na imani zao za kumwamini
Mungu wa kweli na kwenda
katika imani zisizo za kweli.......... na katika kupata burudiko lao kwa muda
basi baadae ikawa ni mateso na hata kuitukana imani yao.
Kuna usalama wa duniani ambao mara nyingi sana
unaletwa na fedha katika kusukuma maisha ya mtu kujiimarisha kiusalama
mathalani kununua vifaa vya moto , pistol au bunduki na wengine hata kuweka
usalama wake kupitia walinzi na mitambo yakuona na pia kupitisha nyaya za umeme
katika nyumba yake na usalama wa kimbingu huu ndio usalama ulio imara sana wa
kwli uwa unatawala duniani hata mbinguni huu usalama ambao hauonekani kwa macho
ya nyama ulio imara sana na kamwe hauwezi kukosea na hauwitaji matengenezo
yoyote wala kubadilisha vifaa.
JE! KWANINI USALAMA WA MBINGU HAUWASADII WAKRISTO WA
SASA?
Ninapozungumzia wakristo sina maana wote haiwasaidii
bali na zungumzia wale watu ambao wanashindwa kudumu katika katika usalama wa
kimbingu. Biblia inasema wazi katika siku za mwisho....... manabii wengi
watajitokeza nao wakifanya ishara nyingi sana na kuwavuta walio wengi ya mkini
hata wateule wa Mungu.
Ki ukweli matatizo yamekuwa mengi sana katika dunia
tuliyonayo sasa na mabya zaidi haya matatizo yamewakumba wote wanampenda Mungu
na wanaipenda dunia na utatuzi wa matatizo haya yamekuwa ni shida katika kijua
ipi ni njia sahihi na ipi si njia sahihi pamekuwa na mvutano mkubwa sana......kiasi
kwamba hata waliokuwa na imani thabiti wameanza kuteteleka hili si jambao
ambalo Mungu analikusudia kuwa watu wake watoke chini ya mawanda yake ila shida
nini?
Zipo sababu kuu mbili ambazo mimi naziona
kama ni tatizo kwa watu waendao kanisani;
i.watu
wengi wanaishi maisha yao na sio ya kristo
kwenda kanisani na kufanya mambo ya kikristo sio
maana nzuri ya kukuita wewe ni mfuasi wa kristo bali jambo la muhimu sana ni
namna gani moyo wako unavyo kwambia au unavyo kupa picha yako na Mungu ni nzuri
au ni mbaya.
Kama kufanya mambo ya Mungu hata punda aliongea
katika kutekeleza lile jambo ambalo Mungu alitaka kumwambia nabii wake, hivyo
kwakutumika pale haina maana kuwa ataenda mbinguni katika matendo yake.
Lazima ujue maisha ya ukristo sio dini wala taratibu
za mchungaji wako bali ni vile moyo wako unavyo kushuhudia kuwa wewe ni nani
mbele za Mungu.............biblia
inasema kama dhamiri yako haita kuhukumu una ujasiri mbele za Mungu.
Ni lazima ujue Mungu hakutuita ili kwamba tuwe
watumishi wa watu bali tuwe watumishi wake kwa kusema hivi si zungumzii
msiwaheshimu wazazi wa kiroho la asha bali fanya yote ukijua aliyekuita ni
Mungu na wala si mtu.
ii.wakati
na jambo lake (majira)
usiishi maadamu siku zinaenda tu au siku zipo bali
tambua ulikuwa ulizaliwa na sasa uko hatua hiyo nab ado unaelekea hatua
nyingine. Usipoutambua wakati jua wakati utakukumbusha kwa namna yake yenyewe.
Yesu alitoa mfano huu kulikuwa na watu kumi wako
kati yao waliweka mafuta ya kutosha na wengine mafuta hayakuwa tosha sio kama
walinyimwa bali ni vile mtazamo wao ulivyokuwa kuona mambo kilahisi hata kabla
bwana harusi kuja wale waliobeba mafuta machache waliisha nabado safari ni
ndefu.........jua kama kweli umeamua kumjaza Mungu tumia wakati huo vizuri ili
usije wakati huo ukaja kukusumbua.
Unapopata wakati wa kusoma neon basi lisome sana na
unapopata nafasi ya kuomba basi omba sana vilevile nafasi ya kutumika basi tumika.........ni kama
mwanafunzi anapokuwa akisoma katika kujiandaa na mtihani wake ili hakikishe
anafanya vizuri ndivyo unaye mwamini Mungu kufanya hivyo. Mwanafunzi mjinga
ujiandaa mahali ambapo mtihani umeshawadia.............maandalizi mabaya
upelekea matokeo mabaya.
Usimlahumu
mtu bali lahumu sana matumizi ya wakati ulionao!!!
Imeandaliwa
na;
Cothey
Nelson.......................................................0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni