Jumanne, 18 Julai 2017

NEEMA IPO HATA KWA HILO




Neema! Neema! Neema!
Ni neno linaloonekana sana hama kusikika sana pindi mtu anapoona wema wa Mungu katika jambo Fulani katika maisha yake mathalani kufaulu masomo, kuoa hama kuolewa, kupata kazi na hata kupata mtoto katika hali hiyo hutoshangaa kusikia mtu akisema “ ni kwa neema ya Mungu tu” kwa maana rahisi watu wengi uhiona neema katika upande wa mashariki pasipo kujua kuna upande magharibi, kwakuwa unaposema kuna mashariki basi ni muhimu uhione magharibi. 

Neema ni jumla ya pande mbili kama hela ili itambulike lazima pawepo pande mbili mathalani shilingi mia (sh. 100) ni muhimu ionekane sura ya nyerere kwa upande mmoja na upande mwingine kuwe na picha ya swala.

Tunapozungumzia neema, kwa watu wenye uelewa wa kawaida wanajua ni uwezesho wa kimungu katika kufanikisha jambo fulani! Na ndivyo ilivyo na moja ya kazi ya neema katika maisha yako ni kufanya uzidi kuimarika katika moyo wako ukizidi kuchotwa na penzi la Mungu na hatimaye kuzidi katika yeye,

Ni muhimu kutambua neema ya Mungu iko na wewe katika hali zote na kuhakikisha unadumu katika wigo wake, hivyo kila siku ukupa neema yake kuhakikisha unakuwa salama tatizo kubwa linakuja pale unaposhindwa kuitambua na kuanza kuiruhusu ianze kushughulika na moyo wako,

Ni jambo muhimu kutambua kila jambo linalo kukumba hama kutokea katika maisha yako tambua neema ya Mungu ya kukuweza kumudu hilo jambo hipo ni wewe kuitambua na kuipa nafasi ili moyo wako uwe salama,

Unaposhindwa kuitambua neema ya Mungu katika jambo linalo kukabili hapo ndipo zaidi ya shida inaanza kujitokeza na kuwa kubwa hata kupelekea kuona dunia ipasuke na uingie ndani kuliko aibu hii………. ni muhimu kujua hakuna jambo jipya linalokutokea, wewe jua wapo lime wakuta ila tofauti inakuja pale katika utatuzi wake lakini jua kwako neema ya Mungu ipo katika kuleta utatuzi ulio sahihi.

Ni kama simba akitaka kumfundisha mwanae kuwinda umtafutia aina ya wanyama walio rika lake mathalani swala wadogo ili aone uwezo wake na ikitokea anataka kushindwa hama kuchoka umsaidia haraka, hivyo ndivyo ilivyo hata kwa Mungu wetu kila jambo anaandaa mlango wa kutokea.

Kuitambua neema ya Mungu katika yote yanayokukabili hiyo ni hatua moja ya ushindi katika hayo yote kwakua Mungu atakupa njia ya kukutoa hapo salama ila shida itakuja pale utakapo likuza jambo kuliko uweza wa Mungu…….yaani hali ya akili kufika mwisho nawe ukaikubali hali hiyo.

Mungu anayo ramani yote kuhusu maisha yako itafute ramani ya njia yako uione neema ya Mungu ikikuambata na sio swala la kuomba tu! Japo kuomba sio vibaya  ila neema ina miminika kwako kutokana na uchaguzi wako. ( kuamua kuifuata sauti ya Mungu).

Neema hipo ni wewe kuikubali katika maisha yako! Uone matunda yake,

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson……………………………………………………………..0764 018535

Jumanne, 11 Julai 2017

ISHI SASA!



ISHI SASA!

Uzuri wa dunia unauona, unatabasamu, unahuzunika hama unafurahi,na pengine pale unaona mapungufu hama apajakaa vizuri na mengine mengi…….kiburi cha haya yote ni kwasababu UNAISHI.

Kuna kuishi kuliko jikita kwa maana miaka kuongezeka, pia kuna kuishi basi tu nifanyeje maana nimejaribu njia zote lakini wapi? Hivyo sina budi kuendesha maisha yangu kwa namna hii, na wako wengine wamejiwekea kuwa kwa sababu pesa zipo basi hapo anaweza kuona anaishi.

Lakini kubwa ni kuishi na hapo utaona ufahari kwa vitu vyote unavyo vipenda na hata usivyo vipenda, ndani ya dunia wako watu wanaishi kwa maana ya kuwa na pumzi  na kuna wachache wanajali na kuzingatia namna wanavyoishi na hali sio lazima uwe na pesa nyingi bali inategemea sana uelewa wako na nidhamu yako katika kuishi, kuna watu una wafikiria wana hela nyingi lakini wanaishia katika ulevi wa kupindukia na mengine mengi japo hela ni muhimu lakini sio jibu la kila kitu.

Kama mtu unayependwa na kutunzwa kwa ajili yake ni muhimu kutambua maadam umepewa siku, masaa na sekunde za kutosha jua umepewa ili uishi basi hapo ujue umepewa fursa umepewa na Mungu iheshimu na uone umependelewa sana.

Ahuhitaji magari hama majumba ya kifahari au watu wengi wakuzunguke ndipo maisha yaanze maadamu unayo pumzi basi hapo maisha yanaweza kuanza, maisha hayajengwi na vitu vilivyo nje bali vilivyo sitirika ndani ya moyo wako ndo mana watu wengi wanaweza kucheka lakini wewe ukawa sawa nao hama vile hali iliyo ndani yako.

Kuishi kunaanza pale akili yako inapo amua kuanza maisha, maana unaweza kukuta mtu anasema” mimi hapa akili yangu imesimama naona kufakufa tu” lakini mwingine akiwa na hali kama hiyo hama zaidi ya hiyo anaweza kuona kuimarika zaidi, anaweza kusema “hata hili bado nitakuwa salama”

Katika maisha kikubwa uhai mambo mengine maadamu dunia idumupo hayo mambo yataendelea kuwepo yanayofanya au kupelekea moyo uiname au uinuke lakini katika yote maadam unapumzi ujue maisha yana kusubiri ili uishi,

Moja ya tatizo linalo wa kwamisha watu wengi ni kuwapa watu daraja, kuwapa nafasi , kuwaona na kuwapa sifa zilizopo katika kichwa chao hama kuwapa utakatifu wa muda na pindi inapotokea kufanyiwa au kufanya jambo likashangaza likakuacha katika bumbuazi ghafla ukaanza kuona kama kuishi hakupo, binadamu yeyote lazima ujue uwa kuna matendo yanatoka pindi mtu anapokuwa na furaha ya kweli na matendo yanayotoka pale mtu anapokasirika.

Amua kuishi kwa maana ya kujipenda na kujifurahia na mazingira yatakuelewa, na watu watakubali tu na zaidi Mungu atakufurahia wewe kwa kuwa umejikubali kama anavyo kukubali vile ulivyo.

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………………………………………………….0764 018535

Jumanne, 4 Julai 2017

MTU NI KITU GANI?



MTU NI NINI?


Zaburi 8:4 Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, Na binadamu hata umwangalie?
                5 Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu; Umemvika taji ya utukufu na heshima;
                6 Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako; Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake.

MTU NI KITU GANI? Hili ni swali linaloweza jitokeza miongoni mwa hali fulani…….mathalani vitu vingi vilivyopo duniani hama wanyama wasimame mbele muumba waone anawapenda sana wanadamu kuliko wao wakaamua kusema “ hivi huyu mtu ni nani? Mpaka amepewa nafasi hii

Tunaweza kukubaliana kwa hili, kwa mzazi mwenye watoto na mwenye akili timamu  na mwenye mapenzi ya dhati kwa watoto wake, hakuna kitu anachoweza kujivunia sana zaidi ya watoto wake na wala sio nyumba hama usafiri anao utumia hama chochote cha thamani kinacho onekana.

Thamani ya Mungu kwa mwanadamu haina mfano hivyo hakuna cha kufanisha ndio maana upaswi kujisikia vizuri kwa kupata tu vitu vinavyo shikika katika ulimwengu wa leo japo ni muhimu kuwa navyo  bali jivunie na kujisikia vizuri kwa kuona thamani ya Mungu isiyo na mipaka katika maisha yako,

Natambua kama kuna mahali ukajua unapendwa mahali hapo hata kama hakuna maji wala chakula unaweza kujikuta njaa na kiu inakatika na upendo unatawala ndani ya moyo wako! Hatimaye unajisikia utoshelevu na raha kuzidi, Naam unaweza kukuta mahali ambako kuna kila kitu ambacho unakipenda lakini ukatambua uwepo wako hautambuliki unaweza kula chakula kizuri sana lakini usiione radha yake, hama ukaanza kutoa mapungufu mengi yasiyo kuwapo nap engine unaweza kula chakula ukahisi kama akiingii tumboni hama kina nasa kwenye koo!

Unapotambua kuwa wewe ni asili ya Mungu na uliyetokana na mikono yake na yeye ndiye aliyeshikiria kila kitu chako na zaidi ya yote anakupenda na kukuthamini zaidi unavyofikiria huna budi kumpenda sana japo namna ya kumpenda sio kama wengi wanavyozani hama kusema OOOh Nakupenda sana Mungu! Kuna namna ukifanya yeye anatambua kuwa wewe  unampenda.
Mungu zaidi ya mfanya biashara, maana lengo biashara ni ili upate faida na Mungu anafanya yote kwa ajili yako lipo kusudi analo lengo la kusababisha afanye yote kwa ajili yako na hicho kitu kinaitwa IBADA,

IBADA ni kitu cha msingi sana kwa Mungu,na hapo ndipo atakapoona fahari yako kwake! Tunapozungumzia ibada huwa sina maana ya kwenda kwenye nyumba ya ibada (kanisani au msikitini) kwakua maeneo hayo ata wezi, wachawi, wapelelezi, waandishi wa habari na hata watafuta wachumba wanaenda,

Unahitaji kujua maana halisi ya IBADA ili uweze kutembea katika njia sahihi na kufanya ibada inayogusa moyo wa Mungu, ibada ni matokeo ya moyo wako kujaa PENZI LA MUNGU, hivyo upelekea kuishi kwa kupendeza moyo wa Mungu na sio msingi mwingine.

Kumpendeza Mungu sio kuishi kwa maadili mema, bali nikulifuata NENO LA MUNGU linavyosema ndivyo unavyoishi!

UWE NA WAKATI MZURI! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson…………………………………………………………0764 018535