MTU
NI NINI?
Zaburi 8:4 Mtu
ni kitu gani hata umkumbuke, Na binadamu hata umwangalie?
5 Umemfanya mdogo punde kuliko
Mungu; Umemvika taji ya utukufu na heshima;
6 Umemtawaza juu ya kazi za mikono
yako; Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake.
MTU NI KITU GANI? Hili ni swali linaloweza jitokeza miongoni mwa
hali fulani…….mathalani vitu vingi vilivyopo duniani hama wanyama wasimame
mbele muumba waone anawapenda sana wanadamu kuliko wao wakaamua kusema “ hivi
huyu mtu ni nani? Mpaka amepewa nafasi hii”
Tunaweza
kukubaliana kwa hili, kwa mzazi mwenye watoto na mwenye akili timamu na mwenye mapenzi ya dhati kwa watoto wake,
hakuna kitu anachoweza kujivunia sana zaidi ya watoto wake na wala sio nyumba
hama usafiri anao utumia hama chochote cha thamani kinacho onekana.
Thamani
ya Mungu kwa mwanadamu haina mfano hivyo hakuna cha kufanisha ndio maana upaswi
kujisikia vizuri kwa kupata tu vitu vinavyo shikika katika ulimwengu wa leo
japo ni muhimu kuwa navyo bali jivunie
na kujisikia vizuri kwa kuona thamani ya Mungu isiyo na mipaka katika maisha
yako,
Natambua
kama kuna mahali ukajua unapendwa mahali hapo hata kama hakuna maji wala
chakula unaweza kujikuta njaa na kiu inakatika na upendo unatawala ndani ya
moyo wako! Hatimaye unajisikia utoshelevu na raha kuzidi, Naam unaweza kukuta
mahali ambako kuna kila kitu ambacho unakipenda lakini ukatambua uwepo wako
hautambuliki unaweza kula chakula kizuri sana lakini usiione radha yake, hama
ukaanza kutoa mapungufu mengi yasiyo kuwapo nap engine unaweza kula chakula
ukahisi kama akiingii tumboni hama kina nasa kwenye koo!
Unapotambua
kuwa wewe ni asili ya Mungu na uliyetokana na mikono yake na yeye ndiye
aliyeshikiria kila kitu chako na zaidi ya yote anakupenda na kukuthamini zaidi
unavyofikiria huna budi kumpenda sana japo namna ya kumpenda sio kama wengi
wanavyozani hama kusema OOOh Nakupenda
sana Mungu! Kuna namna ukifanya yeye anatambua kuwa wewe unampenda.
Mungu
zaidi ya mfanya biashara, maana lengo biashara ni ili upate faida na Mungu
anafanya yote kwa ajili yako lipo kusudi analo lengo la kusababisha afanye yote
kwa ajili yako na hicho kitu kinaitwa IBADA,
IBADA
ni kitu cha msingi sana kwa Mungu,na hapo ndipo atakapoona fahari yako kwake!
Tunapozungumzia ibada huwa sina maana ya kwenda kwenye nyumba ya ibada
(kanisani au msikitini) kwakua maeneo hayo ata wezi, wachawi, wapelelezi,
waandishi wa habari na hata watafuta wachumba wanaenda,
Unahitaji
kujua maana halisi ya IBADA ili uweze kutembea katika njia sahihi na kufanya
ibada inayogusa moyo wa Mungu, ibada ni matokeo ya moyo wako kujaa PENZI LA
MUNGU, hivyo upelekea kuishi kwa kupendeza moyo wa Mungu na sio msingi
mwingine.
Kumpendeza
Mungu sio kuishi kwa maadili mema, bali nikulifuata NENO LA MUNGU linavyosema
ndivyo unavyoishi!
UWE NA WAKATI MZURI! BARIKIWA
Imeandaliwa na:
Cothey
Nelson…………………………………………………………0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni