Jumanne, 15 Agosti 2017

UTAMBULISHO HAUFUNIKWI.






Habari ndugu zangu!

Leo ningependa kuongelea hili neno UTAMBULISHO,………. Tukianzia katika hali hii mathalani tukimchukulia raisi katika nafasi yake katika nchi, uwa popote alipo utambulisho wake haupotei kutokana na mazingira alipo, kama ikitokea ukakutana naye katika stendi ya daladala uwezi kuondoa utambulisho wake wa kuwa yeye ni raisi ukamwita mpiga debe (teja) uku una amani zote, pia mazingira hayaondoi utambulisho wa mtu haijarishi yanaonekaje ila utambulisho utasimama, na hata kama utakutanaye katika kibanda cha mama ntilie bado utambulisho wa kuwa raisi hauta pungua.

Utambulisho ni hali kujulikana kutokana na kitu unachokifanya hama ni maelezo yanayotokana na maarifa uliyonayo yanayo elezea wewe ni nani? Imekuwa ni changamoto hasa katika dunia ya sasa watu kupenda kutambuliwa kutokana wazfa wake hama hadhi yake na inapotokea ameshindwa kuona kuheshimika katika utambulisho wake, mtu huyo kuondoka mahali hapo kabla ya muda kuisha sio jambo la kushangaza.

Watu imefika kipindi watu upenda kutambuliwa wazfa wao hata kuliko usalama wa maisha yao! Pasipo kujua uhai ni bora mara zote kuliko wazfa au nafasi anayoipigania.

Karibu katika somo!!!

Katika himaya ya Mungu kuna utendaji kazi tofautitofauti wa watu waliopewa na Mungu, kwa lengo kuu ufalme wake ujengwe na kufanikiwa sana, hivyo kila mmoja anahuduma hama karama ambayo aliyopewa na Mungu hivyo pia umtambulisha mtu mbali na UTAMBULISHO MKUU kuwa sisi ni wana na watoto wa Mungu.

Kuichochea huduma hama kipawa ilikifanye kazi ni tofauti kabisa na kupigania ili kitambuliwe na kupewa nafasi, kama kipawa amekiweka Mungu atakitambulisha tu, kwa njia yake huna haja ya kumsaidia la msingi ni wewe kufuata maelekezo yake tu, ni kama mbegu uliyoiweka katika ardhi hauhitaji kila siku kuifukua na kuifunika ili kujua itaota kweli? bali la msingi iweke katika mazingira yake timiza uhitaji wake hiyo mbegu itachomoza tu.

Inakuwa shida sana mtu kuona huduma au kipawa chake akipewi nafasi na kuendelea kutumika mahala fulani na huku anaona kuna mahali anaweza kutumia kipawa chake vizuri………. Ni muhimu kutambua kuwa kuona mazingira mazuri ya kutumia kipawa chako sio fursa ya wewe kuanza kutumika, tambua ili kitumike vizuri kinahitaji neema kubwa ya Mungu ikiambate na mazingira yake sahihi sio lazima yavutie macho ya nyama.

Ishara kubwa ya kupenda UTAMBULISHO WAKO sio kuwa na hasira bali kumsikiliza Mungu anasema nini juu ya kipawa chako, tambua asili ya SIMBA uwa haipotei haijalishi yuko katika pori lipi au hali gani ya hewa! joto sana hama baridi sana bado uwezo wake uko palepale!

Hauhitaji kuomba sana ili utendaji wa kipawa chako kidhihirike bali unahitaji ujue ratiba za Roho mtakatifu hapo amani na furaha itakuwa ni maisha yako! Wewe kila siku utaona uzuri wa Mungu na ushindi wake utakuwa  maisha yako.

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………………………………………….0764 018535

Jumanne, 8 Agosti 2017

UCHAGUZI WANGU.





Hakuna kitu kinacholeta raha kwa mtu na utulivu wa kweli na huku moyo ukijaa furaha isiyo na mipaka kama kitu alichokifanya kimetokana na UCHAGUZI WAKE BINAFSI na sasa anajisikia fahari kutokana na maamuzi aliyo yachukua, na maana nyepesi ya uchaguzi ni hali ya kufanya jambo lililobeba utashi wa moyo wako pasipo kuangalia/ kuvutiwa na kitu kingine.

Kama kuna kitu kinaweza kutawala hisia zako au jazba yako katika jambo lolote ni pale utakapo gundua hama kukumbuka kuwa maamuzi uliyo yafanya katika jambo hilo yalikuwa ni uchaguzi wako binafsi pasipo kuwa na msukumo wowote nje yako ulio shawishi macho au masikio yako na hatimaye kupelekea moyo kuchukua maamuzi.

Unapozungumzia uchaguzi katika maisha unazungumzia ustawi au uharibufu wako hivyo katika kipindi au nyakati za kuwa makini sana basi ni katika kufanya uchaguzi  maana ni kipindi cha hatari, uchaguzi naweza kulinganisha ni maamuzi ya dhati mtu anayafanya pasipo kuangalia furaha au kukubalika kwa maamuzi aliyo ya chukua ni sawa mtu anayeingia giza zito na wote wakaona kama anapotea lakini yeye anaona mwanga na kuona hapa ni sehemu sahihi ya yeye kuwepo ( kiwango cha juu cha ubinafsi).

Uchaguzi wowote unao ufanya unakutegemea wewe ili uwe bora hama usiwe bora sio watu/mtu yeyote kwahiyo kushindwa kudumu katika uchaguzi wako ni kutotendea haki maamuzi yako na ukumbuke kuwa katika dunia kila mtu ana uchaguzi wake na sio lazima watu wapende ili utekeleze bali angalia utayari wako binafsi, hivyo uchaguzi ni ubinafsi ulio kithiri,

Kila uchaguzi una gharama zake na ishara ya maamuzi ya dhati kwa uchaguzi ulio ufanya nipale utakapo zikabili gharama na kuzishinda/kuziweza hama kuzimudu hapo ndipo utaonyesha uthabiti katika uchaguzi wako, lazima ujue uzuri, ubora wa uchaguzi unauona wewe na lazima udhihirishe kwa watu wote kuwa uchaguzi ulioufanya kuwa ni bora na ulikuwa sahihi.

Sio kila uchaguzi unao ufanya lazima mazingira ya kuruhusu au yakusaidie katika kufanya hivyo lakini kila uchaguzi unakuwa/unafanyika pale moyo wako uko tayari kubeba gharama ili kuidhihirisha hazina iliyo ndani yako ambayo Mungu ameiweka.

Hatma njema ujengwa na maamuzi sahihi.

UCHAGUZI WAKO NDIO USTAWI WAKO! BARIKIWA.

SIKU NJEMA NI HAKI YAKO!
Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson……………………………………………………0764 018535

Jumanne, 1 Agosti 2017

ATAKUTUNZA.






Kama kuna kitu cha ufahari kwa mtu katika maisha yake nikuona ANAJALIWA, kwa lugha laini uitwa KUTUNZWA kwa maana palipo kujaliwa basi hapo kutunzwa ni jambo lipo tu, 

Kibinadamu kila mtu upenda kutunzwa hata yule anaye tunza naye atapenda kuona na yeye anatunzwa vizuri kwa namna ya yeye anavyopenda ( waswahili wanasema wema hau ozi), japo tunakubaliana wote kila kutunzwa kunako tokana na wanadamu uwa kuna ambatana na sababu na pindi sababu inapoisha hapo watu wengi wanaweza kuona hakuna maana ya kuendelea kutunza kitu/mtu ni sawa na kumlisha ng’ombe ili upate maziwa alafu maziwa haupati, je! Hii ni sawa? Nafikiri jibu unalo.

Watu wengi wanapotunzwa na kujaliwa sana uwa tabasamu na kicheko cha dhati akiondoki katika sura zao na faida kubwa uweza kumuongezea hata siku za kuishi hapa duniani kwakua moyo wake utakuwa umekunjuka na raha imetawala ndani ya nafsini mwake. Japo kutunzwa kuna mapana yake binadamu anaweza asikidhi uwanda wake kwakua binadamu ufanya jambo kwa kadili anavyoona au uwezo alionao  hama alivyo ambiwa kulingana na uwezo wake.

Tunaelewa kutunzwa kwa kweli kunaendana na kupendana ndo mana Mungu achoki kututunza kwakuwa anatupenda maana sisi tu kazi ya mikono yake, na yeye ndiye anayejua namna sahihi ya kukutunza maana yeye ana angalia hitimisho bora la maisha yako.

Watu wengi ujipendekeza kwa walio na ahueni ya maisha kwa kujiwekea nafasi nzuri ya kusaidiwa wakati wa shida hama wa uhitaji pasipo kujua huyu ninaye mwandalia mazingira sijajua yeye anawaza nini juu yangu! Unaweza kujipa matumaini ambayo hayapo mwisho kuumia baada ya kushukuru,

Ni muhimu kufanya yote mema kwa watu wote kama Mungu anavyotegemea utendaji wako kwa binadamu uku tegemea kuendelea kutunzwa na Mungu, na moja ya kitu kinacho zaliwa pindi unapo tambua unatunzwa na Mungu UJASIRI wa kimungu ukivika ndani yako pamoja na amani ya kutosha kutawala ndani yako. 

Na uzuri wa Mungu akutunzi kwa sababu anayo maslahi binafsi yasiyo angalia ustawi maisha yako chochote Mungu anachokifanya haijalishi kina muonekano upi? Kama kama kinafaida kwake kwa namna yoyote basi ujue kwako ni maradufu.

Unapoweka imani katika kutunzwa na Mungu usijifananishe na mwingine na kuanza kusema “ mbona mimi hivi na Yule yuko vile” hali itafanya kushindwa kumuona Mungu katika maisha yako akiwa mwema zaidi ya kuona mapungufu na kasoro zisizo kuwepo,

Unahitaji kujua kila mtu anahitaji kutunzwa na Mungu………unaye muona wa juu, wa katikati hata wa chini wote wanabidi kuweka akili zao kwa Mungu maana yeye ndiye mtoa matunzo hivyo nawe weka uko kwanza na yeye atakutunza kwa namna yake nawe utakuwa SALAMA.

INAITWA SIKU! BARIKIWA.

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson……………………………………………………….0764 018535