Hakuna kitu kinacholeta raha kwa mtu na utulivu wa kweli na huku moyo ukijaa furaha isiyo na mipaka kama kitu alichokifanya kimetokana na UCHAGUZI WAKE BINAFSI na sasa anajisikia fahari kutokana na maamuzi aliyo yachukua, na maana nyepesi ya uchaguzi ni hali ya kufanya jambo lililobeba utashi wa moyo wako pasipo kuangalia/ kuvutiwa na kitu kingine.
Kama kuna kitu kinaweza kutawala hisia zako au jazba yako katika jambo lolote ni pale utakapo gundua hama kukumbuka kuwa maamuzi uliyo yafanya katika jambo hilo yalikuwa ni uchaguzi wako binafsi pasipo kuwa na msukumo wowote nje yako ulio shawishi macho au masikio yako na hatimaye kupelekea moyo kuchukua maamuzi.
Unapozungumzia uchaguzi katika maisha unazungumzia ustawi au uharibufu wako hivyo katika kipindi au nyakati za kuwa makini sana basi ni katika kufanya uchaguzi maana ni kipindi cha hatari, uchaguzi naweza kulinganisha ni maamuzi ya dhati mtu anayafanya pasipo kuangalia furaha au kukubalika kwa maamuzi aliyo ya chukua ni sawa mtu anayeingia giza zito na wote wakaona kama anapotea lakini yeye anaona mwanga na kuona hapa ni sehemu sahihi ya yeye kuwepo ( kiwango cha juu cha ubinafsi).
Uchaguzi wowote unao ufanya unakutegemea wewe ili uwe bora hama usiwe bora sio watu/mtu yeyote kwahiyo kushindwa kudumu katika uchaguzi wako ni kutotendea haki maamuzi yako na ukumbuke kuwa katika dunia kila mtu ana uchaguzi wake na sio lazima watu wapende ili utekeleze bali angalia utayari wako binafsi, hivyo uchaguzi ni ubinafsi ulio kithiri,
Kila uchaguzi una gharama zake na ishara ya maamuzi ya dhati kwa uchaguzi ulio ufanya nipale utakapo zikabili gharama na kuzishinda/kuziweza hama kuzimudu hapo ndipo utaonyesha uthabiti katika uchaguzi wako, lazima ujue uzuri, ubora wa uchaguzi unauona wewe na lazima udhihirishe kwa watu wote kuwa uchaguzi ulioufanya kuwa ni bora na ulikuwa sahihi.
Sio kila uchaguzi unao ufanya lazima mazingira ya kuruhusu au yakusaidie katika kufanya hivyo lakini kila uchaguzi unakuwa/unafanyika pale moyo wako uko tayari kubeba gharama ili kuidhihirisha hazina iliyo ndani yako ambayo Mungu ameiweka.
Hatma njema ujengwa na maamuzi sahihi.
UCHAGUZI WAKO NDIO USTAWI WAKO! BARIKIWA.
SIKU NJEMA NI HAKI YAKO!
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson……………………………………………………0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni