Neno kupotea au kupoteza limekuwa na picha tofauti tofauti katika vichwa vya watu: wako watu baada ya kupoteza wamekuwa na furaha sana na wengine wamekuwa na huzuni sana ikitegemea nini ulichopoteza na umuhimu wa hicho kitu kilichopotea,
Mathalani kama ulikuwa na kitu ambacho kilikuwa ni teso kwako kinapoondoka/ kupotea furaha inachukua nafasi lakini kama jambo ulilokuwa unalipenda na kulitegemea hama kulitarajia kuwa bora zaidi katika majira yajayo alafu likaondoka bila shaka huzuni na mateso yata tawala kwako.
***************************************************************************
Lakini tunapozungumzia UJANA WANGU UNAPOTEA! Hii hali imebeba sura moja tu kwa mtu mwenye akili timamu, hile namna ya utendaji / muonekano kama kijana unakosa nguvu ( inakuwa haipo ).
Unapokuwa kijana unakuwa na hali iliyojaa uhuru binafsi katika mwenendo unaopelekea kuupoteza ujana wako au kuufanya kuwa wa kuheshimika au kutamanika.
Ni muhimu kutambua, hakuna mtu anaweza kuupoteza ujana wako ila wewe binafsi, na unaweza kuupoteza ujana wako kwa kujua hama kutokujua.
Ujana ni hatua ya msingi sana katika maisha ya mwanadamu hivyo unapofanikiwa kuitendea haki itapelekea hatua bora katika maisha yako.
Na ikumbukwe kwamba ukishindwa kuyafanya mambo unayopaswa kuyafanya unapokuwa kijana jua ni ngumu kuyafanya katika hatua nyingine katika maisha yako kwakua kila hatua ina mambo yake.
Kwa hiyo kama kitu cha kuwa makini sana hama cha kuzingatia basi hakikisha ujana wako haupotei kwa gharama yoyote.
Wako watu wanajilaumu katika maisha yao kwakuwa walipewa ushauri na watu walio wazidi umri katika kipindi chao cha ujana lakini walikosa kuzingatia na hatimaye yakawa kuta mambo ambayo hawakutegemea yawakute.
Sio kila kitu ambacho unaona watu wengi wanafanya hasa katika rika la ujana basi nawe ufanye ili mradi tu usionekane uko nyuma ya wakati.
Kuna mambo ya ujana ambayo ukiyafanya yataziba fulsa zako za mbele hata kama mwanzoni wakati unafanya hilo jambo wenzako walikuwa wanakushangilia.
Pia kuna mambo ukiyafanya yanaweza kukupelekea kushindwa kufanya mambo mengine mathalani unapokuwa na mtoto katika njia isiyo halali kwa Mungu, tayari unakuwa na wajibu juu ya mtoto na tayari kuanza kuwajibika kwa huyo mtoto kiakili, kimwili ( nguvu ) na hata uchumi wako na hata kama ulikuwa na mpango mzuri kiasi gani utategemea kwanza ustawi wa mtoto wako.
Kila jambo lipo tu ili mradi unaishi kwa wakati wake utapata.
TUNZA UJANA WAKO UFAIDI MATUNDA YAKE!
INAITWA SIKU! BARIKIWA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson…………………………………………………….. 0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni