Neno “ KUJUA” linakupa kuweza, kufanya kitu katika usahihi na ustawi.
Hali ya kujua inakupa kufanya kitu kwa ujasiri na umakini mzuri.
“ ukijua umeshinda”
Ni muhimu utafute kujua zaidi kwanza kabla ya kutafuta ushindi maana kujua kuna kupa wepesi wa kushinda.
Mathalani. Katika maisha ya mwanafunzi unapopewa mitihani kama vile wa hesabu usipambane kuandika jibu bali tafuta kujua njia ya kufanya ili ikupeleke kwenye JIBU.
Tuna amini ukifanya jambo katika kujua makosa upungua ama ukosekana kabisa.
Unapaswa kujua siri ya kushinda imebebwa na kujua, hivyo ukifanikiwa kujua basi umefanikiwa kushinda.
Ukishinda kwa kujua unapunguza migogoro baini ya watu na watu maana kushinda kwa kujua kunakupa ulinzi dhidi ya maadui zako.
“ mfalme wa ulimwengu huu anakuja lakini hana kitu kwangu” yesu
Yohana 14:30 Mimi sitasema nanyi maneno mengi tena, kwa maana yuaja mkuu wa ulimwengu huu, wala hana kitu kwangu.
Yesu anaonyesha nguvu ya kujua inampa ujasiri wa kushinda mazingira yote.
Baada ya kujua lazima upate neema ya utatuzi bila neema hiyo unaweza kuharibu zaidi baada ya kupata ushindi.
Wako watu baada kujua mambo magumu yaliyofichwa yamepelekea kuwa katika mazingira magumu.
Wako watu wameingia katika migogoro mikubwa, magonjwa na hata chuki zisizoisha na hata hizo chuki kupelekea kula mioyo ya watu taratibu.
Unapotambua mitego mibaya imeandaliwa kwa ajili ya kuharibu maisha yako haupaswi kufanya maamuzi ya haraka yasiyo na muelekeo sahihi.
Unapaswa kujua kwamba kutambua jambo linaloendelea ni hatua moja ya ushindi, hivyo upaswi kuamaki na kukulupuka maana unaweza kukuta unashindwa baada ya kushinda.
Maana kujua ni dalili ya ushindi hivyo hakikisha unashinda!
“ taifa lilikuwa likipigana na Israel wanajikuta kila walipangalo linajulikana na kupelekea kushindwa”
Kupitia Elisha mtumishi wa Mungu katika kujua katika yale yanayoendelea juu ya israeli, israel walikuwa salama wala hakuna shida iliendelea kuwatesa.
2 wafalme 6:1 Kisha, wana wa manabii wakamwambia Elisha, Angalia basi, mahali tukaapo mbele yako ni padogo kwetu.
2 Basi twende mpaka Yordani, twakuomba, tutwae huko kila mtu mti mmoja, ili tujifanyie huko mahali pa kukaa. Akajibu, Haya! Nendeni.
3 Mmoja wao akasema, Uwe radhi, basi nakusihi, uende pamoja na watumishi wako. Akajibu, Nitakwenda.
4 Basi, akaenda pamoja nao. Nao walipofika Yordani, wakakata miti.
5 Lakini mmojawapo alipokuwa katika kukata boriti, chuma cha shoka kikaanguka majini; akalia, akasema, Ole wangu! Bwana wangu, kwani kiliazimiwa kile.
6 Mtu wa Mungu akasema, Kilianguka wapi? Akamwonyesha mahali. Akakata kijiti, akakitupa pale pale, chuma kikaelea.
7 Akasema, Kiokote. Basi akanyosha mkono, akakitwaa.
8 Basi, mfalme wa Shamu alikuwa akifanya vita na Israeli. Akafanya mashauri na watumishi wake, akasema, Kituo changu kitakuwapo mahali fulani.
9 Yule mtu wa Mungu akapeleka habari kwa mfalme wa Israeli, kusema, Jihadhari, usipite mahali fulani; kwa sababu ndiko wanakoshukia Washami.
10 Mfalme wa Israeli akapeleka watu mpaka mahali pale alipoambiwa na yule mtu wa Mungu, na kuhadharishwa; akajiokoa nafsi yake, si mara moja, wala si mara mbili.
11 Basi mfalme wa Shamu moyo wake ukamfadhaika sana kwa ajili ya jambo hili; akawaita watumishi wake, akawaambia, Je! Hamtanionyesha, ni mtu yupi miongoni mwenu aliye upande wa mfalme wa Israeli?
12 Mmojawapo wa watumishi wake akasema, La, bwana wangu, mfalme; lakini Elisha, yule nabii aliye katika Israeli, humwambia mfalme wa Israeli maneno uyanenayo katika chumba chako cha kulala.
13 Akasema, Enendeni, mkamwangalie aliko, nipate kupeleka watu kwenda kumchukua. Akaambiwa ya kwamba, Tazama, yuko Dothani.
14 Kwa hiyo akapeleka huko farasi, na magari, na jeshi kubwa; wakafika usiku, wakauzingira mji ule pande zote.
15 Hata asubuhi na mapema mtumishi wake yule mtu wa Mungu alipoondoka, na kwenda nje, kumbe! Pana jeshi la watu, na farasi na magari, wameuzingira mji ule. Mtumishi wake akamwambia, Ole wetu! Bwana wangu, tufanyeje?
16 Akamjibu, Usiogope; maana walio pamoja nasi ni wengi kuliko wale walio pamoja nao.
17 Elisha akaomba, akasema, Ee Bwana, nakusihi, mfumbue macho yake, apate kuona. Bwana akamfumbua macho yule mtumishi; naye akaona; na tazama, kile kilima kilikuwa kimejaa farasi na magari ya moto yaliyomzunguka Elisha pande zote.
18 Na walipomtelemkia Elisha akamwomba Bwana, akasema, Uwapige, nakusihi, watu hawa kwa upofu. Akawapiga kwa upofu sawasawa na neno la Elisha.
19 Elisha akawaambia, Njia hii siyo, na mji huu sio, nifuateni mimi, nami nitawapeleka kwa mtu yule mnayemtafuta. Akawapeleka Samaria.
20 Hata walipokwisha kuingia Samaria, Elisha akasema, Bwana wafumbue macho watu hawa, wapate kuona. Bwana akawafumbua macho wakaona; kumbe! Walikuwa katikati ya Samaria.
21 Naye mfalme wa Israeli alipowaona, akamwambia Elisha, Ee baba yangu, niwapige? Niwapige?
22 Akamjibu, Usiwapige; je! Ungetaka kuwapiga watu ambao umewatwaa mateka kwa upanga wako na uta wako? Weka chakula na maji mbele yao, wapate kula na kunywa, na kwenda kwa bwana wao.
23 Basi akawaandalia chakula tele; nao walipokwisha kula na kunywa, akawaacha, wakaenda zao kwa bwana wao. Na vikosi vya Shamu havikuja tena katika nchi ya Israeli.
Mambo mengi yanapokusonga unapaswa kutafuta kujua utatuzi uliosalama utakao kufanya kuibuka mshindi katika mazingira yanayo kuzunguka maana ni kusudi la Mungu uwe ushuhuda ili kudhihirisha penzi la Mungu kwa wanadamu.
Lazima uwe na nia ya kuta kuwa wewe uwe salama pasipo na nia ya kumwaibisha mtu maana nia hiyo inaweza kuondoa hali ya Mungu kuwa upande wako.
INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA.
Imandaliwa na:
Cothey Nelson………………………………………………………………………….0764 018535