KUMBUKA ULIKO TOKA (remember where you from)
Matawi yanastawi kwa
sababu ya ustawi wa chanzo chake yaani shina, uhai wa tawi unategemea ustawi wa
shina.
Naye aliye nipeleka yu
pamoja nami, hakuniacha pekee yangu ; kwa sababu nafanya sikuzote ya upendezayo………..( yohana 8:29).
Mimi nimekutukuza
duniani, hali nimemaliza kazi ile uliyonipa nifanye……….( yohana 17:4)
Basi kumbuka wapi ni
wapi ulikoanguka ; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini usipofanya
hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahala pake,
usipotubu…….. ( ufunuo 2:4)
Alipozingatia moyoni
mwake, alisema , Ni watumishi wa ngapi wa babayangu wanaokula chakula na kuzasa
na mimi hapa nakufa na njaa. Nitaondoka, nitakwenda kwa baba yangu na
kumwambia, baba nimekosa juu ya mbingu na mbele yako, sistahili kuitwa mwana
wako tena ; nifanye kama mmoja wa watumishi wako…….(luka 15:17-19).
Hauwezi kwenda mbele
kama ujui ni wapi umetoka kwakua hauwezi kutambua tofauti iliyopo kati alipo
alipo na kule anakwenda.
Kama kikwazo kikubwa
sana ambao watu wengi wanakumbana nacho ni kusahau wapi wametoka hali hii
inapunguza uhakika wa wewe kusonga mbele.
Uwa ninapozungumzia
kukumbuka ulikotoka sina maana ukumbuke maumivu ya nyuma halafu moyo wako uwe
chini au kukumbuka yale mazuri yanayo sababisha moyo wako uchangamke la hasha
bali THAMINI ULIKOTOKA, ni kweli
unaweza usione jema lolote la nyuma ila kumbuka kuwa nyuma yako inamchango wa
wewe uwe vile ulivyo inawezekana imekutia nguvu katika jambo la kufanya au
kukataza jambo la kufanya ili kutengeneza kesho yako yenye manufaa zaidi.
Napenda kusema ikitokea
umesahau ulikotoka hauwezi kudumu katika hali njema bali utaonekana kwa muda
mfupi halafu alafu utaanguka, kwa hakika ukiisahau nayo itakusahau kabisa
pasipo kukumbuka kabisa.
Kama jambo unatakiwa
kulipa nafasi ya kutosha sana ni kuthamini ulikotoka haijalishi palikuaje
pamejenga kitu gani katika moyo wako ambacho ukikumbuka kinaleta majanga katika
moyo.
Duniani kuna watu
walisahau jana yaani vile walivyosaidiwa lakini mwisho wake waliparejea na kuwa
zaidi ya walivyokuwa jana mathalani kunamtu alikusaidia katika kupata kitu
Fulani ambacho kikafanyika sana Baraka katika moyo wako kamavile kazi na mambo
mengine yaliyoufurahisha moyo wako usipothamini kamwe hali hii haitadumu katika
maisha yako yote.
Ni wazi mtu ambaye
anatambua ametoka wapi basi ni rahisi kujua kule aendako kwakua kwa kuweka
mikakati ambayo itamfanya aendelee pasipo kuchoka.
Nanipo zungumzia kuwa
tunahitaji kutambua kule tulikotoka hatuna maana ushiishi maisha yako kuelekea
kule unakotaka bali hali ni hali ya moyo kutambua na kuheshimu na kutambua kila
hatua aliyopitia na mchango wake katika ufahamu aliokuwa nacho ni wazi kama
kile kitu kisingetokea ni wazi usingekuwa na ufahamu uliokuwa nao. ( usipo
shukuru kwa kidogo basi hautashukuru kwa kikubwa…..)
Kila mahali ulipofika
au unapotaka kwenda jua kuwa kuna hatua au ngazi na kila hatua inaitegeme hatua
nyingine hauwezi ukaruka hatua toka hatua hatua ya kwanza na kwenda hatua
yakumi ni wazi utadondoka na usalama wako unategemea umedondokea wapi?
Ni kweli kuna wakati hutataka kuwakupunguka lakini tambua kila jambo linakutokea huwa alijakosea njia
alikuja kwa bahati mbaya.
Hivyo usalama wako ulio
na mwendelezo ulio bora unategemea sana namna unathamini ya nyuma kwa kua ndio
MSINGI wa wewe kuendelea mbele na ukaenda tu pasipo kujali huo msingi wazi tu
utamoka na kamwe hautaweza hautaujua nini cha kufanya kwa kuwa ukuthamini yale
yaliyo kutengeneza.
Mwanafunzi mzuri
anayekuwa makini tangu hatua ya awali na kuendelea sio mtu mwenye kusahau
mwanzo kwakua itamtesa sana na kumnyima na kuwa uwanja hafifu wa kujibu mtihani
wake. Japo ili ufanye vizuri lazima utambue kipi ni bora na sio bora kwa kazi
hii ili ufanye jambo sahihi kwa wakati wa sahihi.
Ki ukweli kama kitu
utakiwi kusahau ni kule ulikotoka na sio katika hali mbaya au nzuri bali katika
hali ya kujifunza katika mazingira yote na kutekeleza jambo linalo kukabili kwa
ufasaha zaidi ili kukukpa hatua ya mafanikio.
Ni ombi langu na
kukusihi usisahau ulikotoka kwa ulimbukeni bali fanya kukumbuka na kujifunza
hapo ndipo utakazidi kujihimarisha pasipo hivyo utapotea tu.
Duniani asilimia nyingi
walioimarika ni wale ambao wanatambua wapi wametoka na kuheshimu kwa dhati wapi
wametoka.
“yusufu akirudi Misri ,
yeye na ndugu zake, na wote waliokwenda pamoja naye kumzika babaye,baada ya
kumzika babaye, Ndugu zake yusufu walipoona baba yao maekufa, walisema labda
yusufu atatuchukia na kutulipa maovu tuliyomtendea, wakapeleka watu kwa yususfu,
kunena…………………..yusufu akawambia, msiogope, je! Mimi ni badala ya Mungu? Ninyi
kweli mlikusudia mabaya, bali Mungu aliyakusudia mema……” mwanzo 50:7-21
imeandaliwa ;
Nelson, Cothey – 0764 018
535 or cotheyn@yahoo.com
Katiti, James - 0713 398 042 or james.adili19@gmail.com
UKIKUMBUKA ULIKOTOKA HAUPOTEZI BALI UNAJIHIMARISHA KATIKA
MWENDO WA MAISHA YAKO.