Jumanne, 24 Desemba 2013

UMASKINI NI WIMBO MBAYA










                                        UMASIKINI NI WIMBO MBAYA;                                              
  (poverty is a bad song)
 

Kabla ya kuanza somo letu kwanza tupate ushuhuda halafu tutaendelea…………..

Mama mmoja alipata bahati ya kuolewa na mme mmoja ambaye alikuwa na utajiri mkubwa sana.

Baba huyu alikuwa anafanya kazi katika taasisi moja ya kifedha katika nchi fulani na mkewe pia alikuwa mhasibu katika benki moja maarufu nchini huko.

Maisha yao yalikuwa gumzo mtaani kwani kila mtoto wao alisoma shule za nje ya nchi hiyo na pia kila waliporudi waliendesha magari tofauti ya kifahari na kutumia fedha kwa anasa.

Kila mwananchi wa mtaa huo alitamani maisha ya familia ile na kila mwisho wa mwaka familia ile ilitumia pesa nyingi kusafiri kwenda kijijini kusalimia wazazi huku kila mtu akiwa na gari lake kuanzia baba mpaka watoto

Mara nyingi yule mama alikuwa na dharau hasa akienda sokoni na buchani, alishangaa kuona mtu akinunua nyama nusu kilo badala ya mguu mzima wa ng'ombe au kisamvu ambacho yeye alidai kuwa ni mboga ya sungura.

Watu wengi walikereka na tabia ile na kumwambia ingawa yeye aliona ni sawa na alichukulia kama ni wivu dhidi ya utajiri wao.

Miaka kadhaa badae kuna wizi wa fedha ulitokea ofisini kwa baba na baba akasimamishwa kazi huku akipewa mshara nusu mpaka pale ushaidi ulipo kamilika na kuonekana kuwa alihusika na kuachishwa kazi bila kupewa haki zake.

Wakiwa sasa wanatafakari nini kinaendelea na wanatumia mshahara wa mke tu aliyebaki kazini na hawataki kuamini kuwa wanatakiwa kupunguza matumizi ya fedha mara mama naye akakumbwa na kashfa ya ubadhilifu wa fedha na kufukuzwa kazi na baadhi ya mali kama nyumba na maduka kutaifishwa na kubaki na nyumba moja waliyoijenga kwa siri maeneo fulani

Maisha yakawa magumu na wakawarudisha watoto kutoka masomoni nje ya nchi na kuwaleta nchini mwao katika shule za kawaida ingawa ilikuwa ngumu kwa watoto kuzoea mazingira haya kwank kwao ilikuwa ni kama kushuka thamani.

Mara wakaanza kusikia mtoto wao wa kike kawa changudoa ili apate fedha za matumizi kwa kuwa hadhi yake ilishuka kwa kukosa fedha kabla ya baba kupata mashtuko uliochangia kupooza mwili baada ya kusikia mtoto wao wa kiume naye kawa shoga ili aweze kupata fedha za matanuzi pia.

Miezi michache baadae baba akafariki na mama mpaka sasa anauza vitenge na nguo za kutembeza mtaani kama mmachinga na mpaka sasa watoto washaharibika.

Ndugu yangu nakusihi kamwe usidharau maisha na watu wakuzungukao kwani huwezi jua Mungu ana mpango gani na maisha yao na yako pia.

Mshukuru Mungu kwa kila baraka uliyonayo na kila mara mheshimu kila mtu na kuheshimu uwezo wake kifedha na hata mawazo kwani sote twamuomba baba mmoja ambaye ni Mungu wa watu wote na hutubariki tofauti kwa nyakati tofauti.

Sasa karibu katika somo letu………..

Huu ni aina ya wimbo ambao watu huimba huku wakiangamia kutokana na kukosa matumaini, wimbo huu hauhitaji ulazimishwe kutoa machozi kwakua yanakuwa yamesha toka sana ndani ya moyo hivyo inakuwa sio ngumu kudhihirika katika macho.

 

Huu wimbo watu wanaimba pasipo kulazishwa japo wengi wao wanaimba katika hali ya kulia kanakakwamba amelazimishwa kuimba wimbo huu…….
Huu wimbo hauhitaji ufundishwe kuimba katika ustadi au katika kufuata ala za muziki bali katika wimbo huu maneno huwa yanatoka yenyewe yakisindikwa na machozi yalibeba uwakilishi wa yale yanaendelea ndani ya moyo wa mtu.
 Wimbo huu unapoimbwa watu hawataangalia namna unavyoiimbwa bali macho yao yataelekezwa katika maneno ya wimbo na muhusika mwenyewe(mwimbaji).

Wimbo haupangwi kuwa nitaimba wakati Fulani bali wimbo huu unaimbwa mahali ambapo moyo unapoanza kutunga maneno ya wimbo huu.

Maneno ya wimbo huu huwa yanaonyesha hali ya kutothaminika tena au dunia imemwangukia mahali alipotegemea kuwa ni kivuli chake panakuwa maangamizo yake kwa maana nyingine ule mti aliokuwa akiutegemea umpe kimvuli sasa unamwangukia na kusababisha majeraha ndani ya maisha yake.

Na wimbo huu pindi utakapo kuta mtu akiimba utakiwi kumnyamazisha bali kuusikiliza hadi atapomaliza yaani machozi yake kufikia ukingo na pindi utakapoamua kumnyamazisha unaweza kusababisha machozi mengine yasiyo katika.

 

Wimbo huu unaweza kuamisha mahali ulipo na kukupeleka mahali ambapo utajifananisha na mwimbaji huyu atakua ameamishima kilio chake na kukushirikisha na wewe, napenda kusema kuwa wimbo huu hauna ufundi wala malekebisho uwa umejitosheleza unachohitaji ni wewe kuusikiliza tu.

Huu wimbo unaimbwa na jamii ya watu waliomo ndani ya jamii hiyo na wala sio wote kwakua kuna wengine wanamaliza kuimba, wengine wanaanza, wengine wako mwishoni na wapo watu waliomo ndani ya jamii hiyo hawajawai kusikia wimbo huo mbaya.

Na pindi unapoimba wimbo huu mtu yeyote mwenye akili zilizo nauelewa kamwe hauwezi kosa kujua maana ya wimbo huo na kuutafakari pamoja na anaeimba.

Wimbo wa masikini ni jumla ya maisha yake ambayo kutokana na hayo maisha moyo wake unatunga wimbo hata akili bila kushirikishwa.

Kwa mtu anayeimba wimbo huwa anamatumaini kuwa ipo siku nitaumaliza wimbo huu au nitakuwa nikiumba siku baada ya siku na kuathiri hata ngozi yangu na ulimi wangu kutoweza kutamka kitu kingine ila wimbo huu.
Wimbo huu(kilio) mara nyingi hauwi kwa ajili yake tu bali sehenu kubwa ni kwa ujumla watu wake wa karibu wanaomzunguka.

Huu wimbo mtu binafsi haupendi kuimba kwakua kadili anavyoimba ndivyo kisima cha machozi kinazidi kububujika ndani yake huwa wimbo huu unaimbwa hata pasipo uhiyari wa mtu husika bali wimbo unakuwa huko tayari kwa ajili ya kuimba…..

 

Watu wanaimba wimbo huu hawaoni fahari ya kuwepo duniani watu hawa hawaoni radha ya dunia hata kwanini bado wanaishi katika dunia ya sasa pasipo kujua uhakika wa kesho yao. Mtu wa namna hii anaweza chochote pasipo kujua nini hatma yake.

Machozi yanayotoka katika wimbo huu yanaweza kung’oa mizizi ya aina yeyote pasipo kujalisha wa hicho kitu na mizizi yake imeenda mbali kiasi gani lakini kutokana na nguvu ya machozi yatang’oa na kuacha mazingira kama hicho kitu hakikuwepo.

 

Ni vizuri kuwa wangalifu sana na huku ukimhofu sana Mungu kwakua wako watu waliofikiri hawataimba wimbo huu lakini baadae waliumba vizuri tena kwa mwendelezo usio koma.

Wimbo huu hauhitaji kujipanga katika mazingira bali moyo wako utaimba tu na huku sura yako ikionyesha hali kuitikia.

Imeandaliwa na ;
                     Nelson, Cothey – 0764 018 535 or cotheyn@yahoo.com
                    Katiti, James       - 0713 398 042 or james.adili19@gmail.com


THINK ABOUT THIS FOR YOUR FUTURE!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni