Jumanne, 31 Desemba 2013

THAMINI ULIKO TOKA



    KUMBUKA ULIKO TOKA                                                                   (remember where you from)

Matawi yanastawi kwa sababu ya ustawi wa chanzo chake yaani shina, uhai wa tawi unategemea ustawi wa shina.

Naye aliye nipeleka yu pamoja nami, hakuniacha pekee yangu ; kwa sababu nafanya sikuzote  ya upendezayo………..( yohana 8:29).

Mimi nimekutukuza duniani, hali nimemaliza kazi ile uliyonipa nifanye……….( yohana 17:4)

Basi kumbuka wapi ni wapi ulikoanguka ; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahala pake, usipotubu…….. ( ufunuo 2:4)

Alipozingatia moyoni mwake, alisema , Ni watumishi wa ngapi wa babayangu wanaokula chakula na kuzasa na mimi hapa nakufa na njaa. Nitaondoka, nitakwenda kwa baba yangu na kumwambia, baba nimekosa juu ya mbingu na mbele yako, sistahili kuitwa mwana wako tena ; nifanye kama mmoja wa watumishi wako…….(luka 15:17-19).

Hauwezi kwenda mbele kama ujui ni wapi umetoka kwakua hauwezi kutambua tofauti iliyopo kati alipo alipo na kule anakwenda.

Kama kikwazo kikubwa sana ambao watu wengi wanakumbana nacho ni kusahau wapi wametoka hali hii inapunguza uhakika wa wewe kusonga mbele.

Uwa ninapozungumzia kukumbuka ulikotoka sina maana ukumbuke maumivu ya nyuma halafu moyo wako uwe chini au kukumbuka yale mazuri yanayo sababisha moyo wako uchangamke la hasha bali THAMINI ULIKOTOKA, ni kweli unaweza usione jema lolote la nyuma ila kumbuka kuwa nyuma yako inamchango wa wewe uwe vile ulivyo inawezekana imekutia nguvu katika jambo la kufanya au kukataza jambo la kufanya ili kutengeneza kesho yako yenye manufaa zaidi.

Napenda kusema ikitokea umesahau ulikotoka hauwezi kudumu katika hali njema bali utaonekana kwa muda mfupi halafu alafu utaanguka, kwa hakika ukiisahau nayo itakusahau kabisa pasipo kukumbuka kabisa.

Kama jambo unatakiwa kulipa nafasi ya kutosha sana ni kuthamini ulikotoka haijalishi palikuaje pamejenga kitu gani katika moyo wako ambacho ukikumbuka kinaleta majanga katika moyo.

Duniani kuna watu walisahau jana yaani vile walivyosaidiwa lakini mwisho wake waliparejea na kuwa zaidi ya walivyokuwa jana mathalani kunamtu alikusaidia katika kupata kitu Fulani ambacho kikafanyika sana Baraka katika moyo wako kamavile kazi na mambo mengine yaliyoufurahisha moyo wako usipothamini kamwe hali hii haitadumu katika maisha yako yote.

Ni wazi mtu ambaye anatambua ametoka wapi basi ni rahisi kujua kule aendako kwakua kwa kuweka mikakati ambayo itamfanya aendelee pasipo kuchoka.

Nanipo zungumzia kuwa tunahitaji kutambua kule tulikotoka hatuna maana ushiishi maisha yako kuelekea kule unakotaka bali hali ni hali ya moyo kutambua na kuheshimu na kutambua kila hatua aliyopitia na mchango wake katika ufahamu aliokuwa nacho ni wazi kama kile kitu kisingetokea ni wazi usingekuwa na ufahamu uliokuwa nao. ( usipo shukuru kwa kidogo basi hautashukuru kwa kikubwa…..)

Kila mahali ulipofika au unapotaka kwenda jua kuwa kuna hatua au ngazi na kila hatua inaitegeme hatua nyingine hauwezi ukaruka hatua toka hatua hatua ya kwanza na kwenda hatua yakumi ni wazi utadondoka na usalama wako unategemea umedondokea wapi?

Ni kweli kuna wakati hutataka kuwakupunguka lakini tambua kila jambo linakutokea huwa alijakosea njia alikuja kwa bahati mbaya.

Hivyo usalama wako ulio na mwendelezo ulio bora unategemea sana namna unathamini ya nyuma kwa kua ndio MSINGI wa wewe kuendelea mbele na ukaenda tu pasipo kujali huo msingi wazi tu utamoka na kamwe hautaweza hautaujua nini cha kufanya kwa kuwa ukuthamini yale yaliyo kutengeneza.

Mwanafunzi mzuri anayekuwa makini tangu hatua ya awali na kuendelea sio mtu mwenye kusahau mwanzo kwakua itamtesa sana na kumnyima na kuwa uwanja hafifu wa kujibu mtihani wake. Japo ili ufanye vizuri lazima utambue kipi ni bora na sio bora kwa kazi hii ili ufanye jambo sahihi kwa wakati wa sahihi.

Ki ukweli kama kitu utakiwi kusahau ni kule ulikotoka na sio katika hali mbaya au nzuri bali katika hali ya kujifunza katika mazingira yote na kutekeleza jambo linalo kukabili kwa ufasaha zaidi ili kukukpa hatua ya mafanikio.

Ni ombi langu na kukusihi usisahau ulikotoka kwa ulimbukeni bali fanya kukumbuka na kujifunza hapo ndipo utakazidi kujihimarisha pasipo hivyo utapotea tu.

Duniani asilimia nyingi walioimarika ni wale ambao wanatambua wapi wametoka na kuheshimu kwa dhati wapi wametoka.

“yusufu akirudi Misri , yeye na ndugu zake, na wote waliokwenda pamoja naye kumzika babaye,baada ya kumzika babaye, Ndugu zake yusufu walipoona baba yao maekufa, walisema labda yusufu atatuchukia na kutulipa maovu tuliyomtendea, wakapeleka watu kwa yususfu, kunena…………………..yusufu akawambia, msiogope, je! Mimi ni badala ya Mungu? Ninyi kweli mlikusudia mabaya, bali Mungu aliyakusudia mema……” mwanzo 50:7-21


imeandaliwa ;
                    
                     Nelson, Cothey – 0764 018 535 or cotheyn@yahoo.com
                     
                      Katiti, James       - 0713 398 042 or james.adili19@gmail.com




UKIKUMBUKA ULIKOTOKA HAUPOTEZI BALI UNAJIHIMARISHA KATIKA MWENDO WA MAISHA YAKO.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni