AMANI ISIYO NA MIPAKA,
Amani yangu na wapa sio kama ulimwengu utoavyo…….yesu
alisema!
AMANI katika maisha ya mtu yeyote ,kwa mwanadamu
hiki ni zaidi ya kuwa na chochote mathalani watoto, mme au mke na hata kazi na
amini hakuna madini yoyote hapa duniani yanayoweza chukua thamani ya amani
ndani moyo wa mtu, ni kweli kuna wakati unaweza usione maana wa jambo lolote au
mtu yeyote lakini si kama AMANI.Na unaweza kuwa na chochote lakini kama hauna
AMANI utoshelevu wa hicho kitu akita kuwa na maana sana zaidi kwakua
kinacholeta radha katika yote ni AMANI, wakati mwingine tunaweza fananisha
AMANI kama chumvi katika chakula chochote unaweza ukaweka kila kitu lakini kama
chumvi haipo jua hapo hakuna radha utakayoipata kwa ukamilifu.
Amani kama angekuwa mtu basi watu wote wangependa
kuwa rafiki yao wa dhati kwani watu wote wanahitaji amani hata kama
mchawi,jambazi,chizi na wengine wengi wanahitaji amani na wanapenda maisha yao
yote yatawaliwe na amani.kutokana na mtazamo huu watu wengi wamekuwa wa kikiri
kuwa haiwezekani kama mwanadamu kutawaliwa na amani wakati wote ungalipo hapa
duniani kwani wanaamini hapa duniani sio mahali salama sana kwani kuna
kukasilishwa,kuumizwa na hata kudhurumiwa hivyo watu wamekubaliana kuwa na amani iliyo na mipaka.
Watu wengi tumekuwa tukiishi na amani kanakwamba ni
haki yake kutokea halafu ikatoweka tumekubaliana na hali hii hivyo tumeona mtu
kuishi pasipo amani ni jambo la kawaida, na mtu kuwa mahali fulani au kufanya
jambo fulani pasipo amani basi panakuwa na mgawanyiko ulio katika mwili na
akili kwa maana hii akili na mwili vinakosa ushirikiano kamilifu basi kwa hali
hii mtu uweza kujigawa pasipo ridhaa yao binafsi.
Ningependa utambue kuwa amani ni haki yako ya kudumu
na wala sio ya muda fulani tu au yakutokea kwa majira fulani mathalani kipindi
ambacho unazo pesa za kukidhi mahitaji yako kwa wakati wako huo na sio hilo tu
bali pia au wakati ambao unahisi kupendwa na kila mmoja kwa kipindi fulani.Ni
kweli tunakuwa na mfano wa amani lakini sio amani yenyewe kwa kuwa kila amani
huwa kuna shina au misingi yake ambayo haiwezi kubomolewa na chochote kile.
Imkuwa si ajabu mtu kusema asubui
nilikuwa na amani yangu ghafla imetoweka sijui kwanini? Au mtu akisema
maneno haya…. mimi nilikuwa na amani zangu lakini ulipokuja tu amani yote
imetoweka, amani sio kitu cha kufikirika tu ambacho kinaishia kwenye akili ni
zaidi ya hapo kwani kina nguvu na uwezo mkubwa wa kumtawala mtu.
“Wana amani
nyingi waipendayo sheria ya bwana wala hakuna la kuwa kwaza….”
Hivyo ukifikia hatua ya kukwazika basi hiyo amani ya
kweli haipo ndani yako kwa ukamilifu wake.
Wako watu wakijishughulisha na mambo fulani au
kiburudisho fulani ili mradi aweze kusikia amani ndani ya moyo wake…..lakini
muda mwingi imekuwa sivyo kama alivyotegemea!!!!!!
Amani za watu wengi zimekuwa ni za vipindi fulani
kiasi kwamba watu uweza kusema kwamba je! Kwenye msiba kunauwezekano kuwa na
amani hasa kwa mtu unaye mpenda au aliyekaribu kweli unaweza kuendelea amani
iendelee kutawala ya moyo wako.Ninapozungumzia amani na zungumzia zaidi ya kuwa
na furaha au utulivu huwa amani haijaishia hapo bali imepitiliza zaidi ndani
sana na hakuna kipimo chake.
AMANI= MATUMAINI
+ ULINZI
Hii ndio tafsiri yangu ya neno Amani katika hili neno
lazima pawepo na muambatano wa matumaini na ulinzi kwa kile unachokitumaini
kuwa utakipa au kifikia.Mambo haya matatu uwa yanaenda pamoja na ndio
yanakamilishana yote kwa ubora sana.
Amani ubebwa na matumaini yaliyo ndani yako
yanayolindwa na katika kufanikisha jambo, hivyo shina la matumaini linategemea
liko wapi au limebebwa na nini? Na je uhakika wa kufikia katika yale
unayoyaendea.Tunapozunguzia ulinzi uwatunatoa maana ambayo inalandana na
Imani-kitu kinachokupa uhakika.Katika yote utayoyapitia amani haiwezi kuondoka
kwa sababu imebebwa na vitu hivyo viwili vilivyo na ukamilisho kwa ufasaha.
Ukiwa katika misingi hii lazima itakuwa inachipuka
kwa wakati wote katika hali mbalimbali iliyo ngumu au nzito unakuwa na AMANI
ISIYO NA MIPAKA ambayo inachipuka ndani yako na kukupa busara katika maamuzi
siku baada ya siku,kama ukiwa na amani ya kipindi tu ya ushawishi wa mwili
hauwezifika mbali kwakua ni ngumu kushamiri na kuwa na uimara wa nyakati zote.
Lazima uwe na amani ambayo hakuna kinachoweza
kuondoa iwe mchumba, rafiki, ndugu au wazazi bali inakuwa imeshirikiwa na nguvu
ya mbingu ndani yako ambayo yeye aliyoiweka ndio mwenye uwezo wa kuiondoa na
hakuna wa kuiondoa zaidi yake ukiona amani inaondolewa tu jua haijajikita
katika misingi ya matumaini pamoja na ulinzi(imani).
Amani isipo kuwepo ni wazi mahala hapo uwezi ukadumu
na vilevile amani isipokuwepo mahali hapo hauwezi ukapafurahia na pakaleta
burudiko ndani ya moyo wako.
Usiwe na amani isiyoimarika bali yenye mabadiliko
siku baada ya siku,amani inatabia ya
kuongezeka pale ambapo shida inapokuwa kubwa huwa aipungui kama kawaida ya
mambo ya dunia yalivyokuwa.hivyo amani yako inapotoweka pale ambapo mambo
yanapokukabili basi ujue hiyo amani ujaipokea kwa kristo bali inafanana na hile
ambayo kristo anaiachilia kwa watu wake.
Uwa amani hii ambayo Mungu anapoiachilia haitaji
huichochee bali ipo inatawala nakutembea katika mwili mzima una kuwa mtu wa
kicheko wa furaha na mawazo yaliyotulia yenye mwelekeo katika mwelekeo
uliosahihi katika mwelekeo ulio na ulinzi wa ki Mungu katika kuyafanikisha yale
yote yaliyo matumaini yako.
Na haiwezekani ukawa na amani ya namna hii kwa
kuombewa au kutabiriwa bali katika
kuliruhusu neno la Mungu katika mwili wako mzima kwa uhakika na kukufanya
vile linavyotaka katika kiwango chake na sio katika fikra zako bali katika
akili ya hilo neno kwa utoshelevu wake. “Mjue
sana Mungu ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujiaa…” Ayubu 22:21
Hauwezi kufanikiwa katika huduma yako na mambo
mengine ya kuinua ufalme wa Mungu kama tu una amani yenye mipaka(amani yenye
kawaida ya dunia) kwakua yenye sio kamilifu kumudu kila hali itayojitokeza
lakini amani ambayo haina mipaka hakuna jambo lililowa tokea au litakalotokea
likamtingisha mtu wa namna hii.
Amani
hii uwa uenda pamoja na ujasiri kwakua amani hii ndani yake hakuna hofu ndani
bali inakuwa ni amani yenye uhakika kwa kila kile kilichokusudiwa kwa kua hii
ni amani iliyo kuu kuliko amani yoyote(shwari kuu).Vilevile amani hiihaendani
na utashi wa mwili ndani yake hakuna asila,chuki,kisasi wala dharau. Hii ni
amani iliyombeba Mungu kwa utoshelevu wake hivyo matunda yaliyo ndani ya Mungu
ndiyo yaliyo ndani ya amani hii katika ubora wake, kwa maana nyingine amani hii
inaongozwa na Roho kwa utoshelevu wake uliosahihi zaidi hatua za Roho mtakatifu
ndio hatua zake.
Vilevile
amani inaenda pamoja sana na pendo la kristo uwa vinashikama pamoja sana
kwakua amani ufanyakazi mahali penye pendo la Mungu kwa utoshelevu kwakua amani
hii imebeba dhima ya kuujenga ufalme wake,kwakua amani yake inakuwa kwa ajili
yake na sio jambo lingine.
Amani
hii pia inatiwa nguvu na macho yako ya rohoni baada ya kutiwa
nguvu ili kuona kama vile Mungu anavyoona na tumani lizaliwe hapo na wala sio
mahala pengine kwa kua macho ya Mungu yamebeba ulinzi wa Mungu na utoshelevu
wake.Na utulivu na maamuzi yenye misingi iliyo bora yanatokana sana na AMANI
ISIYO NA MIPAKA!
Amani hii haina uhusiano na akili ya kibinadamu
kwakua haijashikamanishwa na mwili bali na roho iliyojaa Mungu. ukiona
unaihusisha na akili jua hiyo sio amani iliyombeba kristo bali itakuwa imebeba
kitu kingine!
Imeandaliwa na ;
Nelson, Cothey – 0764 018
535 or cotheyn@yahoo.com
KUWA NAYO AWE NAWE!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!