ILI KUPATA LAZIMA UPOTEZE!!!
I wakorintho 9:24-25
…………na
kila ashindanaye katika mchezo hujizuia katika yote.
I wakorintho 9:26-27
…………bali
nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe nikiisha kuwahubiri wengine;
mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa.
Katika dunia tuliyonayo mambo mengi tunayoyaona kuna
watu wamepoteza vitu vingi sana na wewe unafurahia matokeo ya watu kupoteza
mathalani wako watu wamepoteza muda wao,uhai wao, nguvu zao na ufahamu wao.
Katika ujumbe huu neno hili kupoteza nimelitua
katika mawanda mbalimbali mathalani hali ya kutoa kwa ujumla wake fedha, nguvu
na muda katika lililo jema, matendo ya kujigharimu kwa ajili ya wengine katika
hali njema.
Ni jambo la kushangaza sana watu wengi wanapenda
kupata sana lakini hawako tayari kupoteza pasipo kujua wakati mwingi msingi wa
kupata ni kupoteza. Kwa mkristo yeyote aliye wa kweli lazima kanuni hii haiweke katika utendaji wake
ilikupata ya rohoni lazima uyapoteze ya mwilini!
Pamoja na hayo lazima ujue kwamba unapoteza nini na
kwa namna gani unapoteza haya yote ni muhimu sana ili uweze kufanikisha yale
ambayo unatakiwa, na kuna siri kubwa sana katika kupoteza kwani hali hii ni
inaashiria kutoa kitu kimoja ili kiingie kitu kingine, na kawaida kinatoka kitu
kidogo na kuingia kitu kikubwa.
Ni kweli yako maumivu makubwa sana katika
kupoteza(kutoa) lakini hayo maumivu yatazimishwa baada ya kupata(gain) hii ipo
wazi hata pindi mkulima anapofanya kazi uwa vitu vingi anavipoteza nguvu, fedha
na mangine mengi lakini mwisho anakuwa na furaha kupita ile ya awali baada ya
kupata.
Watu wengi ujizuia sana ili wasipoteze hasa kitu
ambacho wanachokipenda sana kwakua hawajui nini kitatokea baada ya hapo lakini
ni vizuri ujue kwamba kujuzuia kupoteza wakati mwingi ni kujizuia kupata.
Yesu
alisema….inanibidi mimi niondoke ili aje huyu Roho mtakatifu atakaye wafundisha
na kuwa kukumbusha yote!
Japo yesu alikuwepo duniani katika lengo la ukombozi
na pindi alipomaliza ili mlazimu aondoke japo watu wengine wanamwitaji azidi
kuwa nao, lakini yeye alitambua kuwa ni vizuri yeye aondoke aje huyo Roho
atakayekamilisha.
Lazima akili yako ikubaliane kuwa kuna mambo mengine
ni muhimu kupoteza ili uweze kuwa katika namna nyingine hata kama itakugharimu
kwa muda fulani kwani ni muhimu ugharimike leo kwa pumziko la kesho kuliko kinyume
chake.
Kupoteza ni tabia ya Mungu mwenyewe yesu alisema….nautoa uhai wangu kisha nita
utwaa tena na baada ya kutoa uhai wake na kurejea tena hawezi kuwa vilevile
alivyokuwa vile alivyokuwa awali.
Usitegemee kuwa mkubwa sana kama ukiwa hauna tabia
ya kupoteza(kutoa na kusahau) kwakua vile unavyo jigharimu ndivyo utakavyo
stawi ( kujigharimu katika akili njema-maarifa sahihi) na kama hauta weza jambo
hili hawezi kuwa sawa na mtu unayemtamani, kwakua ipo siri kubwa katika
kupoteza na kusahau kabisa.
Usipendelee kushangaa tu vitu vilivyotokana na watu
katika kupoteza na wakawa watofauti bali ata wewe unaweza kujiunga nao katika
kupoteza kuliko kwema kwa hatua njema ya maisha yako.
Pia katika kupoteza lazima uwe tayari kutoeleweka na
watu wengine wanaweza uonekana kama wana kuhurumia sana bali kumbe ndipo wana
kuangamiza.
Imeandaliwa na ;