KATIKA GIZA KUNA KUSTAWI;
(Secrete
in the darkness)>siri iliyondani ya giza
Ni dhana iliyokosa mvuto/uhalisia wa kawaida kusema
kuwa katika giza kuna uwezo wa kustawi
Je! Katika mji huu atatoka mkombozi…. Japo ilikuwa
kama haiwezekani lakini ukweli katika hali hiyo ya mshangao na ndipo mkombozi
alipotokea.
Ni hali ya kawaida kuwa katika giza kuna mambo
mabaya yanatukia yakutisha na hata ya kufedheesha
ambayo hayakubaliki katika
jamii yetu pamoja na mambo hayo napenda utambue giza ni majira na hivyo utegemea
sana mtumiaji na sio usiku wenyewe.
Tumekuwa tukishuhudia wachawi wakitenda kazi nyakati
za usiku (giza) na ikisemekana kuwa hawa ni wana wa giza hivyo ufanya mambo
katika giza ili kuonyesha uasilia wake. Pia yako matukio kama ujambazi
usemekana sana ufanyika wakati wa usiku kuliko mchana.
Lakini na penda kusema hakuna wakati mzuri kama
wakati wa giza!!! Huu ni wakati vitu vingi uimarika na kuwa bora na tishio sana
Yesu! Alikuwa anaomba sana usiku kuliko
mchana…….japo alikuwa anauwezo kuomba popote na muda wowote na anga likapisha
maombi yake kwenda yanakotakiwa.
Giza ni kipindi kizuri sana kwani ni kipindi
kinachoashiria nuru inakaribia pasipo giza kuondoka basi nuru haiwezi kutokea.
Ni kweli katika muonekano mzuri hamna mtu angependa
kufanya mambo yake usiku kwani wana amini usiku ndio muda mzuri wa kupuzika kwa
ajili ya kesho kwa ajili ya kuendelea na shughuli nyingine……….lakini pamoja na
hayo sio wote wana kuwa katika usiku na wanapata fulsa ya kuiona kesho namna
vile wanavyotegemea.
Giza ni hali ambayo unaweza ukawa unamategemeo
lakini bado ukawa na mashaka kwakua hiyo kesho haiko mikononi mwako.
Hichi ni kipindi unaweza kuona jambo lako
haliwezekani au hauta weza kulifikia kwakua kila dakika unaona giza tu wala
haoni mwanga ukitokea kwa haraka kama vile unavyotegemea.
Unapokuwa katika kipindi hiki ni wazi unaweza
kujiona unaweza kuisi kama sio kuona uko wewe na usiku tu na wala hakuna mtu
mwingine aliye pembeni yako.
Hichi ni kipindi usipo kuwa makini sana unaweza
ukatamini kujiua au kutomea machoni pa watu na kamwe usionekane lakini yote
hayo ni kwasababu tu giza limekutana. Na penda sana hichi ni kipindi cha kuzidi
kuimarika sana na kuwa na nguvu sana.
Kweli katika kipindi watu wengi wanaweza kupata
ugonjwa wa moyo kwa namna ulivyolipokea jambo likakuingiza katika usiku wako,
japo na kubali giza ni mahali panapotisha sana na kwa kifupi akupendezi kwa
kuwa uwapo huko hakuna furaha yoyote inayo zaliwa na mwili ikawa na mwendelezo
usio koma.
Ikitokea kama bado haujauingia usiku/giza basi jua
bado hautaweza kuona fahari ya dunia na kusema nimeijua dunia na watu wake
pamoja na mambo yake. Kwa binadamu yeyote lazima aingie gizani lakini utatokaje
inategemea sana uwezo wa uelewa wa akili yako pamoja na wepesi wa
kubadilika sawa katika mwelekeo
unakotakiwa.
Hakuna nguvu iliyoimarika sana isiyozuiliwa kama
nguvu inayozaliwa katika giza kwakua nguvu inayozaliwa hapo inakuwa imebeba
ujasiri zaidi, uhalisi wake, kwakua kipindi hiki akili yako in aona giza tu
hakuna mwanga ambao unaweza kutokea.
Imeandaliwa na ;
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni