NAFASI YA SAUTI
YA MUNGU NDANI
YA MAISHA YAKO;
Kila utekelezaji wa sauti yoyote maishani mwako
inabebwa na nafasi ya huyu mtu kwako unamuelewaje!
Nafasi yake kwako! Kwakua
kila neno linakuwa na uzito likitegemea limetoka katika kinywa cha nani mathalani
neno la daktari aliwezi kuwa na uzito ulio sawa na neno la rafiki yako au adui
yako,jirani hama mtumishi wa Mungu yeyote.
Uzito wa utekelezaji unategemea sana yeye ni nani
kwako?
Umaana wa mtu utegemea namna unavyolitekeleza neno
au sauti yake katika maisha yako hapo ndipo udhihirisho kuwa umemuelewa,
unampenda na unamthamini tena katika utendaji ambao yeye amekusudia.
Ndani ya dunia tuliyonayo uwa tunasikia sauti
mbalimbali zipo zilizo na matumaini mema katika maisha yetu na pia zipo zenye
zinaleta shida katika moyo. Hakuna jambo linaweza kwenda pasipo mgongano wa
sauti mbalimbali zenye kukuonyesha mwanga katika jambo ambalo unalopitia.
Kila sauti uwa inakuwa imebeba dhima fulani,lengo
katika kutimiza kusudi lake,kutoelewa sauti kunapelekea kushindwa kupata
kuelewa kile ulichotakiwa kukipata lakini pindi utakapoelewa basi hapo unakuwa
na nafasi ya kupata yale yote unayotakiwa kuyapata.
I
samweli 3:1-11
Wakati samweli anaandaliwa katika utumishi japo
alikuwa anaishi katika nyumba ya Mungu lakini hakuitambua sauti ya Mungu na
pindi alipoitikia sauti na kuiza kusikiliza ndipo alipotambua kuwa ni Mungu
anazungumza nae.
Kila sauti unayoisikia inakuwa ina nguvu ya
ushawishi katika utekelezaji wa jambo fulani na pindi utakapoipa nafasi basi
yale makusudi yake ndipo yatakapotimia mathalani roho ya hofu utakapoikubali
basi hapo ni wazi hofu itatawala katika maisha yako.
NAFASI
YA SAUTI YA MUNGU NI UKOMBOZI WA MAISHA YAKO;
Kutoka
14:1-14
Japo kuna mchanganyo mkubwa ambao tunaona kwa Musa
ulikuwa ukivuta huku na huku katika kushawishi kuchukua maamuzi kinyume na
sauti ya Mungu. Hapo ndipo ishara kubwa ya kuonyesha nani ananguvu kwako.
Tunaona Musa anafanikiwa kuleta ukombozi juu ya
maisha yake na israel kwa ujumla mara baada ya kuweza kuvuka bahari ya shamu kwa
mkono wa bwana.
Siri kubwa hapa tunaona Musa aliipa nafasi kubwa
sauti ya Mungu kuliko kishindo cha wamisri walipokuwa wanakuja, makelele ya
israel kutaka kumlaumu Musa na kelele za bahari katika mawimbi yake, yote
katika kumtisha Musa dhidi ya kuisikiliza sauti ya Mungu! Lakini bado Musa
alitia bidii katika sauti ya Mungu.
Imeandaliwa na ;
Nelson, Cothey – 0764 018
535 or cotheyn@yahoo.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni