NGUVU YA MUUNGANIKO
Wewe uko vile inategemea sana na nini
ulichoungamanika nacho kwakua kile ulichoungamanika ndicho kina kutengeneza
wewe,wakati mwingine tunajirahumu sisi kumbe yote yanatutokea kulingana na kile
ulichoungamanika. Maisha ya ushindi furaha na ukombozi kwa ujumla yanategemea
sana kile ulichoungamanika.
Kile ulichoungamanika ndicho kinacho kutengeneza
wewe vile ulivyo,uwezi kuwa tofauti na kile ulichoungamanika nacho, hivyo
ukitaka kujikomboa pale ulipo kwanza jikwamue na muungamaniko ulionao ili
ujiungamanishe na kitu kingine.Kila muungamaniko wowote unaleta
furaha,kujiamini na hata kuwa na mategemeo yasiyo koma yaliyo na uhakika, watu
wanakuwa na kujiamini sana pindi wanatambua wana muungamaniko mzuri na mtu wa
ngazi anajua atapata nafasi mzuri kuyafikia mazuri.
Kwa mfano mtu ambaye ana muungamaniko na mkuu wa
kituo cha polisi uwa yuko na ujasiri mwingi hata anapokamatwa au mipango yake
kuzuiliwa anajiamini kwa kuwa kuna mtu akiwasiliana nae mambo yanakuwa sawa.
Mnaweza kuwa wote mnamatatizo yanafanana lakini kila
mtu atatoka hapo kutokana na muungamaniko,mathalani wanafunzi wanamaliza chuo
wakiwa wamefanikiwa stashahada na shahada mbalimbali lakini kutoka/kupata kazi
hapo inategemea umeunganika na watu walio katika nafasi zipi? Watu ulioungamanika
ndio wanaweza kukupa kile kitu walichonacho na kama hawawezi kukupa kitu
ambacho hawana.
Hivyo tunaweza kuona kwamba wapo mtu wanateseka sasa sio kwamba hawana akili au hawana vigezo
vya kukuwezesha kuwa na nafasi nzuri katika kazi na hatimae kuwa na maisha
bora.
HAKUNA
MUUNGANIKO WENYE MAANA SANA MBALI NA MUNGU NDANI YA MAISHA YAKO,
Katika muungamaniko huu wa wewe na Mungu vilevile
utegemea namna ilivyoungamanika ndivyo itakavyo kuwa, namna mlivyoungamanishwa
vizuri ndivyo utakavyo kuwa vizuri,Kuwa na muungamaniko na watu wengi sio mbaya
kwakua katika maisha tuliyonayo tunawahitaji watu kwa kiasi kikubwa kwa kuwa
wao wanakutegemea wewe na wewe unawategemea hivyo sote tunategemea ni kama vule
viungo katika mwili wa binadamu vyote vina umuhimu wake na hakuna kiungo chenye
maana sana kuliko kingine japo kwa haraka haraka unaweza kuona kiungo Fulani
ndicho cha maana lakini sio kweli mathalani unaweza sema tumbo ni muhumu sana
kwa kua linatunza chakula na hatimae kupelekea mwili mzima kuwa nguvu lakini
mdomo ukifunga usipitishe chakula hapo ndipo unaweza kutambua kuwa
kunakutegemeana
Watu
wanapenda kuunganishwa katika shughuli mbalimabali ili mradi tu aweze kufanikisha hazma yake.
Mtu anaye kuungamanisha halafu ukaweka matumaini
yote kwa mtu huyo ni wazi utafika kipindi ambacho utajuta hata kwanini
umeunganishwa katika kazi hile au sehemu hiyo.
Ni kweli Mungu anatumia watu katika kutenda hapa
duniani lakini haina maana kutoithamini nafasi yake katika maisha yako na
ukampa alie kusaidia.
Ni vizuri kutambua misaada yaweza kutokea popote ila
upande wa Mungu yuko mwenyewe na ana njia zake za kumpata bila hivyo uwezi
kupata.
Mbali na Mungu muungamaniko wowote mwisho wake ni
AIBU tu hakuna usalama mwingine.
Ni vizuri utamfute Mungu kwanza halafu yeye akuungamainishe
basi hapo utakuwa salama ila ukijiungamanisha mwisho itakupelekea maumivu
lakini Mungu yeye ajuaeye moyo wa kila mtu atakuungamanisha na mtu naye
atafanyika Baraka na wala sio jeraha la moyo.
Imeandaliwa
na ;
Nelson, Cothey – 0764 018
535 or cotheyn@yahoo.com
KILA LA KHERI…………..RAFIKI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni