Jumamosi, 2 Agosti 2014

IKO WAPI NAFASI YA MUNGU!!!




NAFASI YA MUNGU NDANI YA MWAMINI;






Unapomzungumzia Mungu katika nafasi yake ndani ya maisha ya mwamini ni kitu muhimu sana kwani nafasi unayompa ndio udhihirisho mkubwa wa vile unavyompenda unavyomjua na unavyomtambua.

Ukitaka kuona mtu anaumia sana ni pale tu atakapotambua nafasi ambayo aliitegemea umpe au aliyonayokwako sio ile unayompa.na vilevile ukitaka kuona fahari kwa mtu inakuja pale tu anapoona ile nafasi anayostahili ndio uliyompa.

Kunatofauti kubwa kati ya kumpa nafasi rafiki mpenzi au wazazi na kumpa Mungu nafasi ambayo anaikusudia yeye mwenyewe, kumbuka nafasi ya mtu inakuwa pale katika muonekano lakini Mungu nafasi hakuna mtu anaweza kuiona isipokuwa yeye mwenyewe ndio anaiona kwakua nafasi yake ipo katika hali ya kuonekana na isiyoonekana.

Ukweli kunatofauti kubwa kati ya kwenda kanisani, kutoa sadaka na hata kufanya mambo ya kimungu ya kushangaza na kumpa nafasi ndani ya maisha ya mwamini, tunapozungumzia kumpa nafasi Mungu ndani ya maisha yako uwa sizungumzii swala la kujikabidhi kwa Mungu katika maombi yako pindi unaposafiri,unapokuwa kanisani au unapolala.

Jambo lolote unalolifanya haijalishi ni kubwa au dogo thamani ya jambo hilo linaweza kuwa la maana tu kutokana na thamani inayompa Mungu mathalani yesu alipokuwa hekaluni mama mmoja mjane alitoa kiasi kidogo cha fedha kuliko wote na pia ibrahim alitoa isaka katika moyo wake kabla ajadhihirisha katika mwili watu wote hawa walihesabiwa sawa( utoaji uliokamilifu) mbele za Mungu pasipo kuangalia tofauti walionyesha katika utoaji bali Mungu aliitambua kuwa nafasi kubwa waliompa Mungu katika maisha yao.

Mungu kitu anachokitaka sana ni nafasi ya juu katika maisha yako na mengine yafuate lakini sio ufanye vyote lakini yeye ukampa nafasi ndogo ndomana Mungu anasema mtu anaye nifuata na kuangalia nyuma basi anistahili na mtu yeyote anayempenda mama au baba au chochote kuliko yeye basi huyo mtu anistahili.

Dunia ya sasa tumekuwa tukiipa nafasi kubwa muonekano uliomzuri kwa mtu kuliko kujali na kutoa nafasi stahiki ambayo Mungu anayostahili. Hivi sasa watu wanawaogopa wachumba au watumishi wa Mungu kuliko Mungu mwenyewe.

Ukweli ni kwamba hatuwezi kufanya ibada ilisafi kama tu hatuja mpa Mungu nafasi anayostahili kwakua ukimpa yeye nafasi ya kutosha ndio yeye atakupa yale unayostahili na yeye ndio anaweza kukuwezesha kumwabudu Mungu katika usahihi wake.

Kufanya mambo ya kimungu pasipo kumpa nafasi ya kutosha ni kufanya mambo yake pasipo na uhakika wa kule uendako, sawa na mwenye macho anatmbea gizani usalama wake unakuwa mdogo kuliko vile unavyofikiri.

Ukitaka kuona uzuri wa wokovu na umaana wa wewe kuokoka basi mpe Mungu nafasi ya kutosha katika maisha yako ili yeye atawale maisha yako ili aweze kukuibua yule aliyemkusudia na sio tu unavyofikiri tu.
Kusudi la Mungu katika maisha ya mwamini ni kumpa nafasi ya juu katika maisha yako pasipo kuangalia itakuje au inakuaje.na hakuna aibu utakayoipata kama tu umeamua kwa kweli kumpa nafasi anayostahili Mungu.


Imeandaliwa na;
                     Nelson, Cothey – 0764 018 535 or cotheyn@yahoo.com


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni