TATIZO SIO UNA NINI BALI UNAKITUMIAJE?
Watu wengi wamekuwa wakifurahi sana pindi wanapokuwa
na kitu mathalani hela, kazi, mwenzi wa maisha au chochote ambacho unafikiri
kinaweza kuwa msaada kwako. Siku zote watu wengi wamekuwa na furaha pindi
wanapokuwa wamekipata kitu ambacho wanafikiri kuwa ni kitu kizuri lakini mwisho
wake kile kitu kinaweza kuwa na sura tofauti au kikawa kibaya ni vile kutokana
na vile unavyokitumia.
Hata gari lolote lenye thamani kiasi gani usipojua
namna ya kulitunza na kulitumia bila shaka hiyo furaha yako itakuwa ni
yakitambo tu na kama ujajiandaa vizuri kinachofuata hapo ni mauivu na mateso na
kujutia kwanini nilikuwa na kitu kama kile baada ya kutoona faida yake tena.
Kuna wengine wanaweza pata mwenza mzuri sana hata
watu wakakusifia lakini si ajabu ukakuta mara hampo pamoja tena yote hayo
yanatokana na namna mlivyo mtuza au kumtumia ndivyo ikapelekea hayo matokeo
yake
Unaweza pia kuwa na mtu ambaye ni msaada mkubwa sana
kwako katika mambo yanayokukabili lakini kama hautamjua jinsi ya kumtumia
utaona maana yake ya yeye kuwa naye katika biblia imeanadika kuwa ukimpokea
nabii kama nabii utapata thawabu ya kinabii na usipo mpokea nabii kama nabii ni
wazi hautapata thawabu ya kinabii.haijalishi una nini au una nani kama tu
hautajua jinsi ya kumtumia hautaona maana ya yeye kuwa pamoja nawe.
Na niujinga kuwa na thamani halafu kutoitumia
thamani hiyo japo inawezekana kwa kujua au kutojua inawezekana umedharau,
umeona hakuna umuhimu na hatimae ikawa vile ilivyo, japo kuwa kumekuwa na
tatizo kubwa sana kwa watu kuwa na kitu kizuri halafu kutojua kukitumia mwisho
kikaweka mateso katika maisha yako.
Ndio maana israeli japo katika mambo mengi wlio kuwa
wakiyafanya kwakuto tambua thamani ya musa wanawaisraeli walipombiwa pindi
utakapo gongwa na nyoka basi mtazame nyoka wa shaba basi utapona wapo
waliomtazama na wapo ambao hawakumtazama na kila mtu alipata matokeo sawa na
maamuzi yake.
Ndomana hata yesu alikuwa na wanafunzi wake wapo
walikubali kutembea nae na kummthamini katika mazingira yoyote na wapo ambao
hawakumthamini bali walithamini mambo yake walikuwa nae na kuyapata sawa na
walivyomuona na alivyokuwa kwao lakini petro alionyesha kumtambua yesu kwa
ukamilifu na ndomana akasema………..twende wapi wakati kwako kuna uzima!
Kilaktu kina kuwa na maana sana endapo utajua namna
ya kukitumia na hapo kuna kuwa na wewe maana ya kuwa na hicho kitu unaweza kuwa
na chochote hauwezi kukifurahia tu kwakua unacho bali ni pale utakapojua jinsi
ya kukitumia hapo ndipo utakuwa huru na kitu hicho.
Unaweza ukafikiri kuwa nina Mungu sana kama ujajua
namna ya kumtumia hautakuwa na furaha na maisha yako na Mungu, kwakua
hautatofautiana mtu ambaye hana Mungu, hautaji ufurahie tu kwakua una Mungu
lakini furahia sana utakapoona ukifaidika na huyo Mungu kwa maana hilo ndilo
jambo ambalo Mungu analitegemea na ndilo lenye manufaa kwako na sio jambo
jingine.
Hata yule mwenye hazina uwa huiachilia pindi
utakapoitambua ile hazina aliyonayo na kama huta itambua ni ngumu tu kuiachia
hiyo hazina kuja kwako kwakua hautaipokea vile anavyotegemea au kusudia.
Tafuta sana mtu kuwa na amani na wewe iliuweze
kumjua yeye kabeba hazina gani na namna gani ya kuipata hile hazina iliyoko
ndani lasivyomnaweza kucheka na kufurahi sana lakini kamwe hauwezi kupata
hazina iliyoko ndani yake. Hivyo usifurahi kuwa una mtu tu bali furahia kwakua
una vipata vile vilivyoko ndani yake maana ndio vinavyoweza kukusaidia na sio
yeye mwenyewe kwa namna anavyoonekana.
Imeandaliwa na ;
Nelson, Cothey – 0764 018
535 or cotheyn@yahoo.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni