Jumatatu, 18 Agosti 2014

UPWEKE



UPWEKE;



Yesu alisema…..sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu tena.(yohana 14:18)

Hili ni neno ambalo linahusiana sana na neno KUPOTEZA, palipo kupoteza pana ukiwa basi panapelekea kushamiri kwa upweke. Katika moja ya janga linalotishia sana katika ulimwengu ni upweke ni neno lenye herufi chache sana lakini ni neno lenye nguvu sana na katika utendaji wake uwa matokeo yake uwa makubwa.

Upweke ni vile unavyofikiri na sio vile ilivyo kwakua vile ilivyo inategemea vile akili yako inavyoamini na kukubaliana na sio mazingira yenyewe.

Hili si neno zuri au jambo zuri kusikia au kuona mtu amekuwa mpweke au hali hii imekukuta wewe binafsi kwani hali inayotesa na kama kifungo ambacho haujui utatoka lini.(kina kuwa kama kifungo cha maisha)

Upweke uwa ni matokeo ya kupoteza mtu(kufariki),lengo kutotimia(matarajio yako kwenda sivyo) au kupungua katika hali fulani ambayo umekuwa ukizoea kutendewa mathalani unaweza ukaishi na mtu kwa namna mtu alivyo badilika mpaka unaona unaishi katika hali ya upweke.

Hii hali haibishi hodi(maana haitaji ujiandae kwanza) wala haingalii maskini au tajiri vilevile haingalii mrembo au sio mrembo kwa kifupi hakuna kitu kinahusiana na jambo hili uwa kina mkuta yeyote na kwa mahali popote haijalishi ni wakati wa kufurahi au wa kuuzunika.

Ni wazi mahali palipo na upweke lazima pacha wake wawepo MOYO ULIOSHUKA, AKILI ILIYOKOSA MWELEKEO NA UKOSEFU WA RAHA NDANI YA MOYO.

Japo jambo hili limekuwa likitokea watu wengi na umekuwa ukishuudia na pengine hata kuwatia moyo lakini tambua litakapo kukuta alina uzoefu au ufundi bali linatesa na lina maumivu ambayo haujawai kuyasikia mpaka pale utakapo kumbana na hali hiyo uso kwa uso ndipo utatambua makali yake na ukatiri wake na hapo ndipo utaweza kutambua kwanini watu hali hii inapowatokea uzimia, ujinyonga,kujiua au wengine kuishi maisha ambayo ukuyategemea hapo awali mathalani ulevi, umalaya hata uvutaji wa bangi kutokana kuondokana na upweke.

Wakati mwingine watu hali hii inapowakuta uchukua maamuzi mabaya kutokana na mtazamo ambao wanaona mathalani aibu ndio umenifika,maringo yangu yamefika mwisho,heshima yangu imeondoka,faraja yangu haipo tena,sasa mateso yanakuwa maisha yangu na mwingine uweza sema furaha/fahari yangu haipo tena.

Unapokuwa na fahari yoyote kama vile nyumba nzuri magari ya kifahari na mali nyingine za kuvutia na za ajabu lakini pindi unapokumbwa na hali hii ya upweke utaona wafungwa walio gerezani wana nafuu kuliko wewe kwani kipindi hiki kinaondoa fahari yote unayofikiri itakuwa ya maana kwako.

Ni vizuri kutambua kuwa hii ni hatua kama zilizovyo hatua nyingine kama wewe hauta achwa mpweke basi wewe utawaacha wapweke ndugu zako, rafiki na wakupendao au uwapendao.

Japo hali yoyote inaweza kutokea si semi ujiandae kwa hilo kwani hakuna mtu anajiandaa katika kuishi ya upweke na pindi unapotokea unaweza kuwa tofauti ya vile ulivyofikiria mathalani unaweka insurance ya nyumba au gari basi anakufa mtu upendaye ambaye ukuweza kutegemea wala kufikiria.

Hakuna maneno ya mtu ambayo yakaondoa upweke ndani yako wala “kampani” ya mtu bali hapo itakuwa ni vigumu kwako kujielewa na hata kuelewa watu.

Hakuna suluhisho lingine zaidi………..

MUNGU NDANI YAKO……………………

Yeye anaitwa Mungu wa amani basi na akupe amani!!

Anaitwa Mungu mwenye nguvu basi na akutie nguvu!!

Anaitwa Mungu wa faraja basi na afariji moyo wako!!

Anaitwa Mungu wa kibali basi na akupe kibali tena!!


  Imeandaliwa na ;                                                                                                          
                    
                         Nelson, Cothey – 0764 018 535 or cotheyn@yahoo.com




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni