NGUVU YA MAAMUZI;
Ni jambo la kawaida kusikia neno hili maamuzi kwakua
kila mtu anamaamuzi binafsi ya kufanya hili na kuacha hili na yapo maamuzi
ambayo unaweza kuingiliwa na yapo maamuzi ambayo uwezi kuingiliwa na mtu.
Neno
hili au jambo hili uwa tunalifanya kila siku mathalani unaweza kuamua kulala na
kuamua kutolala au kuamua kufanya jambo lolote au kutofanya jambo lolote na
pamoja na hayo yote ni vizuri kutambua kuwa katika maamuzi pia kunamatokeo ya
maamuzi pia hayo maamuzi yanaweza kukufurahisha au yasikufurahishe.
Ni jambo la kawaida mtu yeyote anaweza kuchukua
maamuzi mabaya lakini akategemea matokeo mazuri pasipo kujua matokeo ya jambo
yanategemea namna ulivyo ulivyochukua maamuzi mfano wako watu wanajuhusisha na
mapenzi lakini hawategemei kuwa huyo mwanamk(msichana) kuwa anaweza kupata
ujauzito.
Maamuzi sahihi ni muhimu sana katika kufanikisha
jambo katika ubora wake kwani jambo lolote unaloweza kulifanya pasipo kuwa na
maamuzi yaliyo sahihi ni wazi kuwa hapo ufanisi uwezi kutokea kwakua kutakuwa
na maandalizi yasiyokuwa na ubora na yenye nguvu.
Hakuna kitu muhimu kama maamuzi thabiti katika jambo
lolote unalolifanya kwani ni kitu pekee ambacho kitakupa kusonga mbele pasipo
na kuyafikia yale unayo ya kusudia, kwakua maamuzi yatakupa nguvu na kuimalika
zaidi katika yale yale unayotakiwa kufanya.
Waamuzi
14:1-4 (unaweza soma sura yote)
Katika andiko hili tunamuona samsoni anashikilia
maamuzi ambayo yeye anajua ni sahihi japo wazazi hawajui hayo maamuzi anayo
yachukua ni sahihi na kujaribu kumzuia katika yale maamuzi anayoyachukua…………….!
Tambua maamuzi wakati mwingi ni kama ukombozi wako
kwani hakuna jambo utakalo lifanya mbali na maamuzi ya kweli ambayo likawa na
mafanikio yanayotisha au kushangaza. Ni muhimu kuwa maamuzi yako yasibebwe na
kitu kingine isipokuwa wewe binafsi ndio ulio asili ya huo uamuzi na hitimisho
la kweli.
Siku zote tamani kuona matunda mema yaki zaliwa na
maamuzi yako na sio jambo lingine na maamuzi yawe na ushawishi wa ndani na sio
wa nje kwani wa ndani ndio utakupa mwendelezo wa kudumu pasipo kuchoka wala
kukata tamaa kwani Mungu ataimalisha moyo wako katika jambo jema lililo bebwa
na moyo wako.
Kama mtu wa Mungu wa kweli lazima utie bidii katika
maamuzi yako kufikia kwenye hatima yako iliyo njema hata pasipo kuangalia kushoto
wala kulia bali macho yako yaone mwisho wenye ustawi wa kishindo.
Imeandaliwa na ;
Nelson, Cothey – 0764 018
535 or cotheyn@yahoo.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni