THAMINI AGANO;
Yapo maneno ambayo jamii yetu hivi sasa wanayatumia
sana kama ishara ya udhihirisho wao katika UPENDO, maneno hayo ni AHADI na
AGANO, sasa hivi mtu asipomwambia mwenzi wake kuwa nakuhaidi au naweka agano
langu kwako kuwa nitakuwa nawe tu na si mwingine.. japo neno hili uwanja wake
katika kutumika ni mpana sana lakini wengi wao katika jamii wamelitumia katika
wenzi wao katika kuonyesha UPENDO wa dhati.
Agano alipo kama kifungo tu bali ni neno ambalo
linakukumbusha na kuimarisha katika lile ulilosema katika kukusudia katika hali
njema au mbaya. Huwa hatuweki agano kwakua tunafurahi sana bali tunaweka baada
ya moyo wako kuridhia pasipo shurutisho na mtu mwingine bali inakuwa ni wewe
binafsi katika akili timamu.
Ningependa neno hili ulitumie kama KIAPO na sio makubaliano tu,
ambayo hayana uimara katika utekelezaji wake.
Katika ulimwengu wa sasa hakuna jambo zuri
linafanyika pasipo agano, utasikia watu wanasema tuliagana vipi na wewe
unafanya nini….au ndo umepuuzia agano au nikueleweje! Japo agano kinaweza kuwa
kama kifungo huru ambacho unatakiwa ukifanye katika hali ya kupenda na sio hali
ya kusukumwa pasipo kupenda.
Hata katika ulimwengu wa mausiano hakuna yanaendelea
pasipo kuwekeana agano kiasi kwamba inakuwa pindi utakapokuwa na mausiano
pasipo kuwekeana agano basi unakuwa na mausiano sio ya kisasa, hivyo unaonekana
kuwa uko nje ya dunia inayoenda na wakati. Sitaki kusema kuwa kufanya agano ni
kubaya la hasha! Ni kitu kizuri japo kuwa unaweza kufanya jambo lililo jema
hata pasipo kufanya agano na mtu.
Ni kawaida kwa mtu yeyote unayempenda ni muhimu
kuweka agano kama ishara ya moyo wako umetua hapo katika pumziko la
kudumu(milele) na kamwe hauna pakwenda mahali pengine kwa kuwa umeshatua katika
mahali salama. Wakati mwingine kuweka agano katika mtu unayempenda hiyo ni
ishara unamfurahia, umelizika nae, unamwihitaji na ndie pekee anayeleta furaha
yake kwako mathalani katika kipindi uchumba ahadi nyingi utokea hapo…….na neno
la mwisho kwa mtu anaye ambiwa uwa usema asante! Nashukuru!
Japo na hali ya uzinto yanayopewa hayo maagano hayo
na kuhusishwa na hisia kwa karibu sana lakini bado kudumu kwake kunapewa nafasi
ndogo sana tofauti na wahusika wenyewe wanapoweka agano lao(wanamatazamio ya
kuendelea,kustawi na kumea).
Katika yote lipo agano ambalo ndani yake alina
tashwishi ni salama sana………….
THAMINI SANA AGANO
LAKO NA MUNGU!!!!!!!!
Tunapozungumzia agano la maana na linalo lipa na
lilsilochoka ambalo aliwezi kukukangusha hata siku moja ni agano lako na Mungu,
hili ni agano hutakaa ulijutie na hata kulifikiria vibaya kwani limebeba kweli
yote.
Napindi utakapolielewa hili agano na kuishi nalo
vizuri ndilo litakuwa chanzo kikubwa cha maagano mengine kuimalika na kuwa na
mafanikio katika maisha yako ya sasa na ya baadae.
Bora uyasahau maagano yote na hata kuyachezea au
kuyapuuzia lakini kamwe sio agano la wewe na Mungu, hili linaweza likaleta NURU
katika maisha yako au GIZA ndani yako.
Mwanadamu na Mungu yako maagano mengi sana lakini
nitaongelea agano moja tu amabao wenye akili walilizingatia wakawa salama na
ambao hawa kulizingatia hawakuwa salama.
NITAKUSIKILIZA WEWE TU!!
Hili ni neno linalofurahisha moyo wa Mungu bali hata
katika mazingira mengine katika watu mathalani uchumba, rafiki au ndugu hili
neno linalovutia sana na lina ushawishi hata katika masikioni, na kamwe hili
neno alichoshi.
Ni kweli katika kusema inawezekana lakini shida
inakuja pale utekelezaji wake mara baada ya kusikia hapo ndipo utajua yule
aliyadhamiria na asiyedhamiria katika
kutamka hilo neno kwa ufasaha wake, hii hatua maelfu wengi wameshindwa na kuonyesha kweli wameshindwa kuonyesha
kweli walikuwa wana maanisha katika kile walichokuwa wakisema.
Pamoja na hayo kuna vitu viwili muhimu sana
kunakuanza kumsikiliza na kuendelea kusikiliza vyote hivi vinakamilisha kusikia
kuanza bila kuendelea ni ishara yakutomaanisha kwa kile kitu unachokiendea.
Agano linatekelezwa wakati wowote tena katika
mzingira yote pasipo kujali wakati huu agano linatekelezeka na wakati huu agano
alitekelezeki na katika wakati mgumu hapo ndipo ishara ya kuwa wewe unaiheshimu
sauti yake……….mathalani ibrahimu
alipofanikiwa kumsikiliza Mungu kuliko chochote………ndipo Mungu akasema.. kwakua
ukunizuilia mwanawako hakika kukubariki nitakubariki. ( mwanzo
22:1-yote)(1,15-17).
Hii iko wazi kuacha kumsikiliza kwa sababu mazingira
yalikuwa hayaruhusu hiyo ni sawa na kusaliti na ishara ya kuwa umejitenga na
yeye hata kama unamkiri usiku na mchana.
Mathayo 15:8, watu hawa wananiheshiu kwa midomo yao
tu ila mioyo yao uko mbali nami;
Mungu adanganywi kwakua yeye mwenyewe hajawai
kudanganya na hata kaa adanganye neno lake ni amina na kweli.
Hili agano limwbeba vitu vingi sana;
i)kupuuzia wasemayo watu
ii)kupuuzia usemayo moyoni mwako kinyume na sauti
yake
iii)ishara ya kujitoa kikamilifu kwa ajili yake tu.
Imeandaliwa na ;
Nelson, Cothey – 0764 018
535 or cotheyn@yahoo.com
KUMSIKILIZA
NDIO ISHARA PEKEE YA KUONYESHA UMEMKUBALI!!!!!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni