HOFU YA MUNGU;
Ni hofu ya Mungu pekee inayokuwezesha kuishi maisha
ya furaha, ushindi,nguvu na ujasiri. Haya maisha hayana kuigiza wala hayana
mkumbo ni maisha yanayo jitambua na kuona fahari ya kweli ya maisha pamoja na
Mungu.
Japo neno hili watu wamelitafsiri vibaya kutokana na
namna lilivyo HOFU lenye maana ya kuogopa, kutisha kushangaza hata
kustajabisha, hivyo watu uhusianisha neno hili na hali yao na Mungu katika
kumuogopa sana
Mungu kanakwamba mtu katili, anatisha, hanahuruma na hali hii utaikuta
pale watu wanapoenda kanisani wanakuwa wapole sana na wenye unyenyekevu wa nje.
Na sio hapo tu bali hata katika misiba watu huwa na hali ya ukimya sana
wanatulia kila mtu akiwa muogopa Mungu kama kitu ambacho huwezi kushinadana
nacho.
Ndani ya biblia neno hili HOFU YA MUNGU(KUMCHA
MUNGU) limepewa nafasi kubwa sana kiasi kwamba mtu yeyote ambaye anamcha Mungu
amekuwa ana nafasi ya pekee na Mungu kama ishara kubwa mtu anampenda Mungu,
anamjua Mungu na anaishi kwa matakwa ya Mungu tu.
Ayubu
1:1
Napia tunaona Mungu vile asivyopendezwa na mtu
ambaye hamchi yeye, hivyonishara ya kwamba kwa tu ambaye anamcha yeye basi
anakuawa na nafasi nzuri kwa Mungu
Warumi
3:18
Japo kuwa sio wote lakini wengi wao
wamekuwa katika kutimiza taratibu za binadamu zinazo muhusu Mungu, na
kwakufanya hivyo wamepata kibali kwa watu na watu kuwaita kuwa ni wanamcha
Mungu.
Na watu wengi wamekuwa wakisumbuliwa sana
kuona/kupata maana ya neno hili KUMCHA MUNGU ilivyo halisi.
-kwa maana ya kumcha Mungu zipo maaana nyingi lakini
hizi ni maana kama msingi katika kukupa mwanga tayari kutembea na Mungu.
i.ni
kutembea katika maisha yako huku ukitambua na kuthamini uwepo wake pamoja nawe!
Ni vile unafanya kwakua unampenda na kuona kuwa
fahari yako ni Mungu kujisikia vizuri katika uwepo.
Hii ni nidhamu popote ambayo unafanya kwakua
unamtambua na kumuheshimu Mungu na sio kitu kingine.
Mwanzo 39:9(b)( ni
vizuri usome sura nzima)
………..nifanye
ubaya huu mkubwa nimkose Mungu wangu!
Siku zote unajiona mbele za Mungu na wala sio mbele
za watu kutokutekeleza kwako si vile unaogopa watu bali ni vile UNAMUHESHIMU
MUNGU!
Ni nidhamu binafsi iliyo nzuri na yenye udhihirisho
wa kweli kweli unamoenda Mungu na unaheshiu uhusiano wenu.
ii.ni
kutembea katika maisha yako huku ukiwa ni kivutio na furahisho la moyo wa
Mungu!
Mtazamo wa maisha yako kwa Mungu yakaonekane kuwa ni
burudiko katika moyo wake maisha yako yakaonyeshe yanamuelewa Mungu, na
kumthamini Mungu katika utekelezaji na sio hisia tu.
Furaha yako inajengwa na furaha ya Mungu ndani yako
na sio jambo lingine…..FURAHA YA BWANA NDIO NGUVU YAKO!
Imeandaliwa na ;
Nelson, Cothey – 0764 018
535 or cotheyn@yahoo.com
KILA LA KHERI…………..RAFIKI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni